Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 788
- 1,015
Ni kweli kama taifa na hata mataifa mengi ya Afrika tulihuzunika na kusikitika mno tulipompoteza Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa JMT awamu ya 5.
Bado tunapomkumbuka tunatamani angekuwepo leo , lakini kweli MUNGU ni mkubwa na mwema sana, hiki kitu amekiweka kwenye kanuni ya uumbaji wake, mbegu ili iote huanguka na kufa kwanza na kisha huzaa mbegu nyingi kama yenyewe lakini isipo kufa basi itabaki moja kama ilivyo.
Jambo hili ndilo faraja pekee tunayopata baada ya kumpoteza JPM , leo tunapoona bunge limecharuka, vijana wasomi tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha, wamethubutu na kutenda kwa kutumia vizuri elimu tulizowapa kuwahoji na kuwashikisha adabu mafisadi katika taifa hili wanaotugeuza watanzania kama watumwa wao, kwa kula jasho letu bila huruma huku wananchi masikini wakiteseka na hata kufa kwa dhiki mbalimbali.
Hakika mbegu aliyoipanda hayati JPM leo imemea , tuimwagilie na kuitunza mazao hayo yatufae kama taifa la Tanzania.
#Kazi iendelee !