Mbatia: Umbea Ulichochea Yaliyonikuta!

Mbatia: Umbea Ulichochea Yaliyonikuta!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,309
MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia amesema yaliyomkuta kwenye yake ziara mkoani Mtwara ambako amelazimika kuikatisha,yametokana na umbea aliouita ni wa mwaka 2013.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, alisema hayo jana kwenye Ofisi za Bunge Dar es Salaam.

"Unasemaje (anamuuliza mwandishi), ngoja nikwambie kilichotokea kimetokana na umbea tu wa mwaka mpya 2013, wewe tambua hivyo na sitazungumza lingine zaidi,"alijibu kwa kifupi akionyeshakukwepa kulizungumzia suala hilo zaidi.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini viliripoti kuhusu Mbatia akiwa na wabunge wa chama chake, Moses Machali (Kasulu Mjini ) na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) walilazimika kujifungia ndani ya ofisi za NCCR- Mageuzi wilayani Mtwara Mjini.

Hatua hiyo ilifuatia baada ya baadhi ya wananchi kuamua kumrushia chupa tupu za maji, huku wakimfuata kabla ya kuizingira ofisi hiyo wakiimba nyimbo za kumshtumu kuwa ni mamluki.

Ilielezwa kuwa, hali ilikuwa tete eneo la ofisi hiyo hasa baada ya giza kuingia, kwani wananchi walianza kurusha mawe juu ya ofisi hiyo na wengine kujaribu kuvunja mlango na kurusha vitu vinavyodiwa kuwa ni baruti zinazotumika kuvulia samaki .Hali hiyo ilisababisha polisi waliofika kumuokoa kutumia mabomu ya machozi.

Mapema mwaka huu baadhi ya wananchi wa Mtwara waliandamana wakipinga gesi kusafirishwa kuletwa Dar es Salaam.Badala yake, walitaka mtambo wa kuzalisha umeme uwepo mtwara.
 
Kama serikali yenye dola bado imeshindwa kuwashawishi, kuwaelewesha na kukubaliana na wana Mtwara, yeye alifikiri angeweza vip angali alishatofautiana na matakwa ya wana Mtwara? Wakati mwingine tusipende kuwajaribu watu.
 
Walitumwa kuwashawishi wanamtwara walegeze kamba.
 
Huyu si mamluki alitumwa akapime urefu wa maji. Kina cha maji hakipimwi kwa miguu yote miwili unaingiza mguu mmoja kwanza:majani7:
 
Tumpe heshima ni mwenyekiti wa chama
 
Jambo moja naloona TLP, UDP na NCCR wajihi wa wenyeviti wao kweli unafanana na kushabihiana. Wamefanikiwa sana kuvifanya vyama vyao viwe kama wao kitabia, kifikra na kimwenendo.
 
Pole mr Politician; wanamtwara wana hasira na maamuzi yatakayowaachia maumivu, kwani baadae tutawaita Mburura halafu sisi wa Dar wajanja!
 
MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia amesema yaliyomkuta kwenye yake ziara mkoani Mtwara ambako amelazimika kuikatisha,yametokana na umbea aliouita ni wa mwaka 2013.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, alisema hayo jana kwenye Ofisi za Bunge Dar es Salaam.

"Unasemaje (anamuuliza mwandishi), ngoja nikwambie kilichotokea kimetokana na umbea tu wa mwaka mpya 2013, wewe tambua hivyo na sitazungumza lingine zaidi,"alijibu kwa kifupi akionyeshakukwepa kulizungumzia suala hilo zaidi.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini viliripoti kuhusu Mbatia akiwa na wabunge wa chama chake, Moses Machali (Kasulu Mjini ) na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) walilazimika kujifungia ndani ya ofisi za NCCR- Mageuzi wilayani Mtwara Mjini.

Hatua hiyo ilifuatia baada ya baadhi ya wananchi kuamua kumrushia chupa tupu za maji, huku wakimfuata kabla ya kuizingira ofisi hiyo wakiimba nyimbo za kumshtumu kuwa ni mamluki.

Ilielezwa kuwa, hali ilikuwa tete eneo la ofisi hiyo hasa baada ya giza kuingia, kwani wananchi walianza kurusha mawe juu ya ofisi hiyo na wengine kujaribu kuvunja mlango na kurusha vitu vinavyodiwa kuwa ni baruti zinazotumika kuvulia samaki .Hali hiyo ilisababisha polisi waliofika kumuokoa kutumia mabomu ya machozi.

Mapema mwaka huu baadhi ya wananchi wa Mtwara waliandamana wakipinga gesi kusafirishwa kuletwa Dar es Salaam.Badala yake, walitaka mtambo wa kuzalisha umeme uwepo mtwara.

pole sana ndugu mbatia kwa mkasa huo, jamani inapofikia suala la usalama wa binadamu unatishiwa inabidi tuungane na kulaani hali au kitendo hicho regardless of our political difference.
 
Jamani Mbatia ni mbunge wa viti maalumu.Unafikiri kazi yake ni ipi,lazima alipe fadhira kwa aliempa ubunge.
 
WA DSM MJANJA UNGEKUWA UNAKULA VICHWA NA MIGUU YA KUKU WA KICHINA?????:majani7:
 
Huyu mbunge wa viti maalumu ana jichanganya mwenyewe maana kwa sasa inabidi amtumikie muajiri badala ya wananchi!
 
Back
Top Bottom