Mbatia na umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbatia na umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, Oct 19, 2009.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mbatia awapasha wanasiasa

  Imeandikwa na Waandishi Wetu;
  Tarehe: 18th October 2009


  MWENYEKITI wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, amewalaumu wanasiasa kwa kudai kuwa wanafanya suala la mgawo wa umeme kuwa la kisiasa wakati ni la kitaalamu.

  Mbatia amedai kuwa, wanasiasa ni chanzo cha mgawo unaondelea nchini hivi sasa kwa kuwa hawathamini mawazo ya watalaamu.

  Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, vitendo vya wanasiasa hao vinaathiri sana uchumi wa nchi, na kwamba,wajasiriamali wengi wanapata hasara. Amesema, wanasiasa hao badala ya kutafuta suluhisho la kudumu la tatizo la umeme, wanalumbana.

  Mbatia amesema watanzania wanahitaji umeme na si malumbano, na kama kuna waliokosea kuingia mikataba wachukuliwe hatua, na umeme upatikane.

  Amesema jijini Dar es Salaam, kuwa, mgawo unaoendelea sasa umedhihirisha kwamba wanasiasa hawaheshimu mawazo ya wataalamu. Ameonyesha kusikitika kuona watanzania wanaumia, uchumi unadidimia lakini fikra za wanasiasa zipo kwenye migogoro.

  Kwa mujibu wa mtaalamu huyo wa masuala ya umeme na maji, wataalamu wa nishati hiyo hawana kazi kwa sababu wanawaangalia wanasiasa wanalumbana kuhusu suala hilo.

  “Tuwaachie wataalam watupe suluhisho la umeme hili suala si la kisiasa,” amesema Mbatia na kuhoji iweje nchi iwe na hazina kubwa ya gesi lakini bado kuna tatizo la umeme.

  Amesema, Uholanzi ina gesi kidogo lakini inaitumia vizuri kupata nishati ya uhakika.

  Mbatia amesema, sambamba na tatizo la umeme kufanywa la kisiasa, ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa pia umechangia kuwepo kwa mgawo wa nishati hiyo.

  Mwanasiasa huyo amesema, ni dhana potofu kuamini kwamba, mitambo ya kampuni ya Dowans ni suluhisho pekee la tatizo la umeme nchini.

  Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) juzi lilitangaza kwamba, makali ya mgawo wa umeme yataongezeka kwa kuwa, kiasi cha cha nishati hiyo kinachoingia kwenye gridi ya taifa kinazidi kupungua.

  Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano Tanesco, Badra Masoud, wakati mgawo unaanza kulikuwa na upungufu wa megawati 65 katika gridi ya taifa, baadaye kukawa na upungufu wa megawati 90, lakini hadi juzi kulikuwa na upungufu wa megawati 150 kwa kuwa uzalishaji katika mitambo ya Kihansi, Kidatu, na Pangani unazidi kupungua.

  Hivi katribuni, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, alisema, kama mitambo ya Dowans ikifanya kazi, tatizo la umeme nchini litakwisha. Zitto aliishauri Serikali iitaifishe mitambo hiyo, Serikali imekataa.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema, Serikali ikifanya hivyo itakiuka Katiba ya nchi .

  Jumla Maoni (2)

  Maoni

   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mpuuzi mwingine huyu..
  Kupanga mipango ya upatikanaji vyanzo vya umeme ni swala la wanasiasa. Ndio kazi wanayoifanya bungeni kupokea bajeti ya serikali kila mwaka. Ndio kazi tulowakabidhi CCM ktk uongozi wa nchi hii kutokana na ahadi zao kisiasa. They are responsible kwa patikanaji na ukosekanaji wa umeme.

  Matakwa ya watalaam ni lazima yafuate sheria zinazoambatana na utawala uliopo na sera zao ktk vipaumbele vya ununuzi au uagizaji wa mitambo na sii kutumia mahitaji yetu kuwa sababu ya kukiuka taratibu, ilani na sheria, ni muhimu kuelewa nafasi ya Wanasiasa.

  Ikiwa kweli wataalam ni boira zaidi ya wanasiasa basi hatuna haja ya kuwa na serikali kwani watalaam wanaweza panga kila kitu na wakaweza kuendesha vilevile pasipo kuzingatia sera za chama.
  Kiongozi yeyote asiyefahamu nafasi ya wanasiasa hakika sii mzima wa akili kwani mawazo yake yeye mwenye hayana Utaalam kwa nini asiwaachew Wataalam wazungumze.. yeye si mwanasiasa imekuwaje naye azungumze kuhusu umeme, yeye ana utaalam gani?.
  Upuuzi mtupu!
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  NCCR Mageuzi hivi ni ka-NGO kinacho deal na nini ? nimesahau?
   
 4. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni mwandisi na wewe ni mtukanaji
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ukisahau, sahau hata uamuzi wako wa kukiita chama cha siasa NGO
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kumbe ni NGO inayojishughulisha na siasa? asante kwa kunikumbusha.
   
 7. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hata ukijitahidi vipi hutabadili ukweli, najua chimbuko la mawazo yako hasi
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Waridi,

  Mkuu mimi sii mtukanaji isipokuwa mtu akiongea utumbo ni lazima tumkosoe.. na maelezo ya mtu yanapoitwa Upuuzi sii tusi hata kidogo.

  Kumbuka Rutabanzibwa (mtaalam) alipokataa kuweka sahihi ununuzi wa Richmond mbona hamkusema kitu, na sidhani kama kuna top technocrat ktk sector hiyo zaidi ya mkurugenzi wa wizara lakini what happened..

  Tunayosikia magazetini ni maneno ya Tanesco wahitaji na wadau wake kwa nini Mbatia asimuulize mkurugenzi wa wizara ya nishati wa sasa hivi anasema nini kisha kuwakilisha mawazo yake maanake huyu ndiye mtaalam wa serikali au sio.. Umeona mahala wakimhoji hata siku moja.

  Yule Rutabanzibwa, kazibwa kweli sikuona cha Mbatia kusimama kumtetea mtaalam huyo leo keshia wapi hata sielewi..
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,914
  Trophy Points: 280
  ruzuku
   
 10. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kwa uelewa wangu mimi ni chama cha siasa [kwakuwa hakijafutwa kwenye daftari la msajili] ambacho sehemu yake ya kuendesha siasa ni pale habari maelezo na ukumbi wa mikutano wa pale makao makuu ya chama.
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Didi he complete his Engineering degree?
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,808
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  No. He never did! and that is why he is saying:


  bu**sh**
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  So never call him Muhandisi I even dont think the ERB recognise him as an Engineer either graduate or professional!
   
 14. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NCCR mwaka huu sitegemei kama kitapata hata kiti kimoja cha Mwenyekiti Serikali za mitaa. Baada ya kwenda kuhamasisha chama chake anafukuzana na wanasiasa na umeme wa mafisadi.
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wizi mtupu......
   
 16. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni kweli Mlimani hakumaliza kwa sababu za kisiasa, lakini amahitimu uhandisi sasa nchini Uholanzi, kwa hiyo ni MWANDISI
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  matatizo ya umeme wa kisiasa bongo hauhitaji hata degree kuelewa nini cha kufanya, issue ni kwamba watu (CCM) hawataki tu kuendeleza nchi.
   
 18. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hiyo kweli ni changamoto kwamba anao wajibu huo pia. Lakini NCCR si peke yake, uchaguzi ukimalizika turudi hapa na takwimu kuthibitisha ubashiri wako wenye makosa
   
Loading...