Mbatia liangalie hili suala kwa umakini

Mbatia liangalie hili suala kwa umakini

Kambamiti

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
291
Reaction score
165
Katika umoja huu wa UKAWA upande wa NCCR mpaka sasa ndio wamesikika hadharani kutoa maneno na kuonesha pingamizi kwa baadhi ya mambo katika Umoja huu.

Kwa mfano miezi iliyopita tumesikia matamshi toka kwa viongozi wachache na wajumbe wa chama chako.

Vile vile katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa, wananchi wa Mtwara mjini walishuhudia CCM kushinda katika sehemu nyingi ambazo UKAWA hawakusimamisha mgombea mmoja. Ikumbukwe kwamba kwa Mtwara UKAWA walikubaliana kufanya hivyo. Hata hivyo, mwishoni NCCR iliamua kusimamisha wagombea kwa baadhi ya mitaa ambayo tayari walikubaliana kuachia chama kingine. Hivyo, ikapelekea CCM kushinda katika mitaa hiyo.

Jana Mbatia kama mwenyekiti ametoa kauli ile. Hapa sasa ndipo wananchi tutajiuliza, je, ndani ya UKAWA ni NCCR tu ndio wanakwazika na huu mchakato? Je, NCCR wana nia ya dhati na huu UKAWA? Je, NCCR ina uongozi dhaifu kushindwa kukabiliana na changamoto za huu umoja ndani ya chama chao? Je, CCM wamepata kichochoro cha kujaribu kuuvuruga huu umoja?

Bado NCCR mna muda wa kuangalia haya mambo kwa mapana kwa manufaa ya sisi WATANZANIA. Tumaini letu ni UKAWA.

Mh. Mbatia yaangalie haya kwa jicho lako la busara na karama za uongozi ulizopewa.
 
Mimi sioni tatizo la mbatia, kuna viongozi ndani ya cdm ni tatizo sana. Wanafikiri wananchi tayari wameshawakubali na ni wao ndio vimungu mtu. Hatuwezi kuishinda ccm kamwe kwa kutosamee yaliyopita na kukaa pamoja ill kupanga jinsi ya kuishinda ccm. Ukiwambia Zitto ana mchango mkubwa sana, tusahau yalitokea tushirikiane nae, wanajenga kiburi kama wameshachukua nchi. Bila ya ushirikiano ccm hatuiwezi katu.
 
MKUU hii imekaa vizuri mno. Ila Mhs Mbatie lazima ajue kuwa kama akiendelea na maneno ya namna hii basi HISTORIA itakuja kumhukumu tu. Ana njia nyingine za kuweza kuafikiana na vyama vyenzake na si kuanza kushaout as if amepigwa mkuki! Na kama nionavyo bado kuna nafasi ya chama chake kusaidiwa angalau kipate wabunge zaidi ktk uchaguzi ujao. Ila hapa inatakiwa busara ya hali ya juu.
 
Mimi naona kama vile NCCR wana matatizo kwa sababu hatujasikia viongozi wa vyama vingine wakitoka hadhalani na kutoahizi shutuma.

Hebu angalia kwa mfano jimbo la seremgeti eti wanataka wapewe wakati kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 walipata sijui kijiji kimoja tu wakati cdm wameikimbiza ccm ile mbaya. lakini wamekomaa eti wanataka wapewe jimbo la serengeti.

kuna kijana mmoja alikuwa anasema mambo kuhusu ukawa wakamfukuza lakini leo mbatia ameanza kusema yale yale ya DEO meck

sijui kama mbatia anataka kukunjua makucha ama laa
 
MKUU hii imekaa vizuri mno. Ila Mhs Mbatie lazima ajue kuwa kama akiendelea na maneno ya namna hii basi HISTORIA itakuja kumhukumu tu. Ana njia nyingine za kuweza kuafikiana na vyama vyenzake na si kuanza kushaout as if amepigwa mkuki! Na kama nionavyo bado kuna nafasi ya chama chake kusaidiwa angalau kipate wabunge zaidi ktk uchaguzi ujao. Ila hapa inatakiwa busara ya hali ya juu.

Mkuu nafikiri ungewasaidia kwa kuwaambia watoke maofisini wakakitangaze chama chao kwa wananchi kama viongozi na makada wa chadema. Hivyo hivyo na vyama vingine kwenye umoja huu nao waende kwa wananchi kutoa elimu ya uraia na kuhimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kuliko kusubiria miujiza siku ya uchaguzi.
 
mimi naona kama vile NCCR wana matatizo kwa sababu hatujasikia viongozi wa vyama vingine wakitoka hadhalani na kutoahizi shutuma.

Hebu angalia kwa mfano jimbo la seremgeti eti wanataka wapewe wakati kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 walipata sijui kijiji kimoja tu wakati cdm wameikimbiza ccm ile mbaya. lakini wamekomaa eti wanataka wapewe jimbo la serengeti.

kuna kijana mmoja alikuwa anasema mambo kuhusu ukawa wakamfukuza lakini leo mbatia ameanza kusema yale yale ya DEO meck

sijui kama mbatia anataka kukunjua makucha ama laa

Unakunjua makucha kutokana na ulivyowekeza. Nawaasa sana wabunge wa nccr Kigoma kuendelea kubaki kwenye ukawa na m/kiti wao namwombea mungu angalau ashinde ubunge jimbo la Vunjo na huko ndo kuwekeza. Sasa wanachama wachache na hivyo hivyo wabunge hayo makucha utayakunjulia wapi na kwa jeuri ipi?
 
Sio siri kauli na maneno ya Mbatia yanaudhi harafu mwanzo sikufikiri kama huyu bwana angeweza kuja kuwa tatizo, sana sana nilimuhofia Lipumba kumbe ndio yuko smart kuliko, Ubunge wa zawadi waweza kuwa ni sababu
Fanyeni muwezavyo ila mi ccm NOOOOOO! Kura yangu Ukawa
 
Mbatia ni pandikizi, sawa sawa na Mrema. Bora utusaidie kuibomoa UKAWA.

Mnakumbuka utabiri kuwa ukawa itasambaratila kabla ya uchaguzi
 
Wakati wenzao wa chadema wakijenga chama vijijin wao wanapanga jinsi ya kunufaika na kubinga bingo tu,then wanataka usawa,wenzao wame invest sana,wasijilinganishe
 
mimi naona kama vile NCCR wana matatizo kwa sababu hatujasikia viongozi wa vyama vingine wakitoka hadhalani na kutoahizi shutuma.

Hebu angalia kwa mfano jimbo la seremgeti eti wanataka wapewe wakati kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 walipata sijui kijiji kimoja tu wakati cdm wameikimbiza ccm ile mbaya. lakini wamekomaa eti wanataka wapewe jimbo la serengeti.

kuna kijana mmoja alikuwa anasema mambo kuhusu ukawa wakamfukuza lakini leo mbatia ameanza kusema yale yale ya DEO meck

sijui kama mbatia anataka kukunjua makucha ama laa

alafu kupata ushindi serkali ya mitaa sio kigezo cha chama kuchua jimbo
kama ingelikua hivyo basi ccm wngelishinda uchaguzi wa 2010 kwa 90% tena na zaidi tumia busara zak i mkuu sipi kwenye kundi la ukawa ila napenda umoja wa vyama kuiondoa ccm madarakani

mungu ibariki act yangu
 
Nccr kuna tatizo. kama hakitakuwa kivuri cha ukawa basi jimbo la kasulu mjini na vijijini yataondoka. uchaguzu serikali za mitaa apa kasulu mjini, viongoz wa ukawa walikaa na machali eakapanga jinsi kila chama kitakavyoweka mgombea. mpango huu badae uliujumiwa na na diwan mke mwema akishirikiana na viongozi wa juu wa nccr hasa nyambabe. matokeo yake upinzani ulishindwa. kwa upuuz woote wa viongozi wa nccr basi ajue chama kinazikwa kama TLP
 
Mimi sioni tatizo la mbatia, kuna viongozi ndani ya cdm ni tatizo sana. Wanafikiri wananchi tayari wameshawakubali na ni wao ndio vimungu mtu. Hatuwezi kuishinda ccm kamwe kwa kutosamee yaliyopita na kukaa pamoja ill kupanga jinsi ya kuishinda ccm. Ukiwambia Zitto ana mchango mkubwa sana, tusahau yalitokea tushirikiane nae, wanajenga kiburi kama wameshachukua nchi. Bila ya ushirikiano ccm hatuiwezi katu.

Watanzania tunataka mabadiliko, wakati ni sasa, kama zitto alikuwa anataka mabadiliko asingebomoa Chadema angetulia na madaraka alikuwa nayo tena Naibu katibu mkuu Chadema! Huwezi kuleta mabadiliko kwa kuanzisha chama wakati vyama vipo, uongo! Zitto akijiunga ukawa itakufa yupo kwa ajili ya masilahi yake.
 
Zitto ni mpenda mabadiliko! ila hapendi kuburuzwa, na hicho ndicho kinachowaogopesha cdm. Cdm mnataka kutumia vigezo vya matokeo ya serikali za vijiji kugawa majimbo! unadhan zzk na act wangekubali. kigezo gani kilitumika kugawana vjj! hao wenyeviti mnaowaongelea hata wanachama wa act walipigia kura ukawa kwa sababu act ilikua bado haijaanza kujitangaza! kwa hiyo mm naona wangetafuta nzuri ya kugawana majimbo hata kama haitalingana lakini kuwe maridhiano mazuri. chama kimoja kisione kua chenyewe ndio ukawa kuliko vingine safari itakua ngumu!
 
Tatizo la Chagadema ni wanafiki sana na kujiona kama wao ndo waPinzani pekeyao na wanaweza kuitoa ccm pekeyao,ebu tuone Ukawa ikivunjika kama watapata hata wabunge wawili,Ukawa ikivunjika hii saccos itabakia kama TLP
 
Back
Top Bottom