Mbatia kutimuliwa UKAWA?

Mbatia kutimuliwa UKAWA?

Status
Not open for further replies.
HALI inazidi kuwa mbaya ndani ya Kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kufuatia taarifa za mgogoro mkubwa uliopo kati ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.

Chanzo cha mgogoro huo ambao unafukuta, ni madai ya Slaa ya kutomwamini Mbatia anayedai ni pandikizi anayetumiwa na serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuvuruga umoja huo.

Inaelezwa, Slaa anamshutumu Mbatia kuwa ni Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, hivyo ni hatari kwa ustawi wa umoja huo, na kuna uwezekano akasababisha kusambaratika kwake iwapo ataendelea kuwepo.

"Ukiwa nje huwezi kuona hali halisi ya mambo, kwa tulio ndani ndio tunaona kila kitu, huu umoja hauwezi kufika popote maana watu hawaamiani hata kidogo na kuna migogoro kila kukicha"

"Sasahivi Slaa anashinikiza Mbatia aondolewe UKAWA, anadai akiachwa atavuruga mpango wa kwenda ikulu" kilisema chanzo chetu kilichopo ndani ya kambi ya UKAWA.

Chanzo hicho kilisema, msimamo huo wa Slaa umewapa wakati mgumu vongozi wengine wa kambi hiyo na wanaona wakimtosa Mbatia watasababisha mgawanyiko wa wanachama, hivyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza Katibu Mkuu huyo.

"Slaa hapendi kumuona Mbatia akiwa UKAWA, ila Mbatia ni muhimu zaidi kuliko Slaa kwenye umoja huu maana anawakilisha chama na iwapo chama chake kitatoka kutasababisha mpasuko, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza katibu mkuu, ila wakimpuuza unamjua mambo yake, ataanza vurugu ndani ya chama" kilisema chanzo chetu.

Aidha, mbunge mmoja wa CUF akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, baadhi ya wanachama wa UKAWA wanamshutumu Mbatia kuwa mmoja wa walioshinikiza kambi hiyo kususia mchakato wa Katiba mpya na kushawishi wasirudi bungeni.

"Kuna mambo yanatia mashaka sana na leo viongozi wetu wanajuta, uamuzi wa kususia bunge la Katiba haukuwa sahihi, vongozi wetu walipotoshwa kususia bunge. Naamini kama tungebakia bungeni na kushindana kwa hoja, kingeeleweka"

"Mbatia alikuwa kinara wa kusisitiza tusirudi na kuna taarifa feki zilikuwa zinakuja ambazo zilionekana wazi mchakato ungekwama, lakini tumeona kilichotokea, CCM na baadhi ya wabunge wa UKAWA wakaendelea na wameandika walichotaka, na kwa hali ilivyo katiba wanayotaka wao itapita" alisema mbunge huyo kutoka Zanzibar (jina tunalihifadhi).

Mbunge huyo alisema, hali hiyo inaonyesha wazi kuna watu ndani ya kambi hiyo wanatumika na CCM, na mbinu ya kushawishi UKAWA wasirudi bungeni ilikuwa ni maagizo maalum yenye lengo la kuwapa nafasi CCM kupitisha mambo waliyotaka kwenye Katiba mpya.

Taarifa zaidi zinasema, jambo jingine ambalo linampotezea imani Mbatia kwa baadhi ya viongozi wenzake, ni uhusiano wake na kigogo mmoja mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ingawa mwenyewe mara kadhaa amekuwa akikana madai hayo na kushusha lawama kwa CCM kuhusika kusambaza madai hayo.

Inaelezwa, Mbatia amekuwa karibu na kigogo huyo na wamekuwa wakikutana mara kwa mara nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salam kwa lengo la kupeana maelekezo ambayo hawana shaka yanalenga kufanya hujuma kwa kambi hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema, kambi ya UKAWA ipo kwenye wakati mgumu ukiachilia mbali mgawanyiko uliopo katika suala la kuteua mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, kuna hali ya kutoaminiana na kila mmoja anamuona mwenzake ni msaliti.

"Kabla hawajaungana Chadema waliwahi kukishutumu CUF kuwa ni tawi la CCM (CCM B), Wenje (Ezekiel Wenje) aliwahi kuwashutumu CUF kuwa ni chama cha mashoga, Chadema hao hao walishamuita Mbatia ni mbunge wa Rais Kikwete kwa kuwa aliteuliwa na Rais hivyo ni mbunge anayefuata maagizo ya CCM" alisema John Malingumu mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

Mchambuzi huyo aliongeza kuwa, kila mmoja ndani ya kambi hiyo ameungana na mwenzake kwa malengo binafsi, ila hakuna mwenye imani na mwenzake.

"Pale kuna unafki mkubwa, kila mmoja amebaki na historia yake kichwani ya mambo ambayo walifanyiana kabla hawajaungana, utakumbuka pia Chadema waligoma kuunda Kambi ya Upinzani na CUF, haya yote hayajafutika ingawa wanajifanya yote yamepita, ni uongo"

Hata hivyo, hali hiyo ya kutoamiana iliwahi kukemewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Prof. Mwesiga Baregu ambapo alisema, migogoro na migawanyiko inatokana na hali ya kutoaminiana huku wengine wakitengwa na kuitwa wasaliti.

“Matokeo ya hali hii ndiyo yanayozalisha mivutano isiyokuwa na tija, huyu kasema hivi yule naye anasema vile, hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake na kibaya zaidi watu ndani ya chama hawaaminiani, utasikia leo huyu katajwa msaliti, kesho yule, utafika wakati vyama vyetu havitakuwa na msafi, wanachama wote watakuwa wasaliti,” alisema Profesa Baregu.

Sidhani kama ni kweli
 
Mmh... tatizo humu watu ni wajuaji MNO
habari hii inaweza kuwa na ukweli ila sasa inavyowasilishwa ni ujinga ule ule wa sababu za ZITTO kuondoka CHADEMA badala waseme ukweli utasikia mara anatumiwa mara vile, watu wanakuwa wanatafuta huruma tu za kijinga.
 
Kama hivi slaa mgombea urais chadema,cuf kugombea urais kwa tiketi ya chadema sijui nani atagombea kupitia ukawa.

Kwani UKAWA wameshachagua mgombea wa Urais?

Au mnahorojoa tu mkuu?

cc FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Hakuna jambo linafanikiwa kwa kufanywa na watu au makundi yasiyoaminiana, kuepuka mgawanyiko na migogoro ni lazima kila mwanachama ashiriki kwa manufaa ya UKAWA.
 
Mimi naaweza kuamini huyyu. Mbatia ni pandikizi na ni mcheza sinema. Ile ishu ya yule mwenyekiti wake alieonekana jina lake kwenye wajumbe waliopigakura imeishia wapi ile kesi?

Simuamini Mbatia hata kidogo na ninawasiwasi yale ya kuweka jjina la makamo wake wa kule Zanzibar amechangia miakwamia.

Pale wamegawana mkwanja mrefu na hata saiv ukimuona ambari anacheka tuu
 
Siku moja ukweli ukijulikana uliopo ndani ya chadema kuhusu mabele malando na mwesigwa baregu hamtaamini wote hao ni watumishi wa serikali ukawa zungukeni sana baada ya uchaguzi mkuu ndiyo mtayajua haya wakati huo mtakuwa peupe kama karanga.

kwani kuwa mtumishi wa serikali,ina manisha huwezi kuwa mpinzani wa chama tawala.hi ni kwa nchi ya mapunguani kama Tanzania pekee.mbona mimi mtumishi wa serikali na nipo chama kingine si ccm.
 
Duuu...ama kweli zimwi likujualo halikuli uka kwisha. Kila marefu yana ncha....
 
1. ukisoma sehem nilizo highlight red, habari hii ya kutunga

- Wewe unasema upo ndani, kwanini usiwe source ya habari? unasema chanzo hicho kilisema, kwahiyo wewe hujitambuwi nimzushi.

2. mgorogoro kwamujibu wa title ya hoja yako unahusu Dr slaa, ukawa na mbatia

-CUF, CHADEMA na Baregu wanaingiaje? maana unasema DR Slaa, maana yake sio Chama, kama nichama migogoro

hushughulikiwa kitaasisi siyo kiindividual, Slaa kama individual hawezi fanya mamuzi ya chama bila kupitia vikao stahiki

vya maamuzi waliwepo wanasheria kubadili makubaliano ya UKAWA.

Uzushi na mawenge mawenge kama haya tusubiri tuone unajim wako kama utatimia. wengine waritabiri kufa kwa wanasiasa, kinyume chake akafa mnajimu na akina shibuda wanadunda mpaka leo.

Mkuu namimi nilitaka kumshushia kama ulivyomshushia ila kwa vile umekidhi haja ya moyo wangu Basi lamba.......liji -LIKE likubwa mno.
 
HALI inazidi kuwa mbaya ndani ya Kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kufuatia taarifa za mgogoro mkubwa uliopo kati ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.

Chanzo cha mgogoro huo ambao unafukuta, ni madai ya Slaa ya kutomwamini Mbatia anayedai ni pandikizi anayetumiwa na serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuvuruga umoja huo.

Inaelezwa, Slaa anamshutumu Mbatia kuwa ni Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, hivyo ni hatari kwa ustawi wa umoja huo, na kuna uwezekano akasababisha kusambaratika kwake iwapo ataendelea kuwepo.

"Ukiwa nje huwezi kuona hali halisi ya mambo, kwa tulio ndani ndio tunaona kila kitu, huu umoja hauwezi kufika popote maana watu hawaamiani hata kidogo na kuna migogoro kila kukicha"

"Sasahivi Slaa anashinikiza Mbatia aondolewe UKAWA, anadai akiachwa atavuruga mpango wa kwenda ikulu" kilisema chanzo chetu kilichopo ndani ya kambi ya UKAWA.

Chanzo hicho kilisema, msimamo huo wa Slaa umewapa wakati mgumu vongozi wengine wa kambi hiyo na wanaona wakimtosa Mbatia watasababisha mgawanyiko wa wanachama, hivyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza Katibu Mkuu huyo.

"Slaa hapendi kumuona Mbatia akiwa UKAWA, ila Mbatia ni muhimu zaidi kuliko Slaa kwenye umoja huu maana anawakilisha chama na iwapo chama chake kitatoka kutasababisha mpasuko, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza katibu mkuu, ila wakimpuuza unamjua mambo yake, ataanza vurugu ndani ya chama" kilisema chanzo chetu.

Aidha, mbunge mmoja wa CUF akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, baadhi ya wanachama wa UKAWA wanamshutumu Mbatia kuwa mmoja wa walioshinikiza kambi hiyo kususia mchakato wa Katiba mpya na kushawishi wasirudi bungeni.

"Kuna mambo yanatia mashaka sana na leo viongozi wetu wanajuta, uamuzi wa kususia bunge la Katiba haukuwa sahihi, vongozi wetu walipotoshwa kususia bunge. Naamini kama tungebakia bungeni na kushindana kwa hoja, kingeeleweka"

"Mbatia alikuwa kinara wa kusisitiza tusirudi na kuna taarifa feki zilikuwa zinakuja ambazo zilionekana wazi mchakato ungekwama, lakini tumeona kilichotokea, CCM na baadhi ya wabunge wa UKAWA wakaendelea na wameandika walichotaka, na kwa hali ilivyo katiba wanayotaka wao itapita" alisema mbunge huyo kutoka Zanzibar (jina tunalihifadhi).

Mbunge huyo alisema, hali hiyo inaonyesha wazi kuna watu ndani ya kambi hiyo wanatumika na CCM, na mbinu ya kushawishi UKAWA wasirudi bungeni ilikuwa ni maagizo maalum yenye lengo la kuwapa nafasi CCM kupitisha mambo waliyotaka kwenye Katiba mpya.

Taarifa zaidi zinasema, jambo jingine ambalo linampotezea imani Mbatia kwa baadhi ya viongozi wenzake, ni uhusiano wake na kigogo mmoja mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ingawa mwenyewe mara kadhaa amekuwa akikana madai hayo na kushusha lawama kwa CCM kuhusika kusambaza madai hayo.

Inaelezwa, Mbatia amekuwa karibu na kigogo huyo na wamekuwa wakikutana mara kwa mara nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salam kwa lengo la kupeana maelekezo ambayo hawana shaka yanalenga kufanya hujuma kwa kambi hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema, kambi ya UKAWA ipo kwenye wakati mgumu ukiachilia mbali mgawanyiko uliopo katika suala la kuteua mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, kuna hali ya kutoaminiana na kila mmoja anamuona mwenzake ni msaliti.

"Kabla hawajaungana Chadema waliwahi kukishutumu CUF kuwa ni tawi la CCM (CCM B), Wenje (Ezekiel Wenje) aliwahi kuwashutumu CUF kuwa ni chama cha mashoga, Chadema hao hao walishamuita Mbatia ni mbunge wa Rais Kikwete kwa kuwa aliteuliwa na Rais hivyo ni mbunge anayefuata maagizo ya CCM" alisema John Malingumu mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

Mchambuzi huyo aliongeza kuwa, kila mmoja ndani ya kambi hiyo ameungana na mwenzake kwa malengo binafsi, ila hakuna mwenye imani na mwenzake.

"Pale kuna unafki mkubwa, kila mmoja amebaki na historia yake kichwani ya mambo ambayo walifanyiana kabla hawajaungana, utakumbuka pia Chadema waligoma kuunda Kambi ya Upinzani na CUF, haya yote hayajafutika ingawa wanajifanya yote yamepita, ni uongo"

Hata hivyo, hali hiyo ya kutoamiana iliwahi kukemewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Prof. Mwesiga Baregu ambapo alisema, migogoro na migawanyiko inatokana na hali ya kutoaminiana huku wengine wakitengwa na kuitwa wasaliti.

“Matokeo ya hali hii ndiyo yanayozalisha mivutano isiyokuwa na tija, huyu kasema hivi yule naye anasema vile, hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake na kibaya zaidi watu ndani ya chama hawaaminiani, utasikia leo huyu katajwa msaliti, kesho yule, utafika wakati vyama vyetu havitakuwa na msafi, wanachama wote watakuwa wasaliti,” alisema Profesa Baregu.

acha uzushi na uzandiki wewe!!
 
UKAWA ni mti wenye matunda mema kurushiwa mawe ni kawaida .mmeshindwa kuwafukuza wezi wa pesa za umma mnakuja kutunga taarabu humu mpelekieni mzee Yusufu.
 
"Matokeo ya hali hii ndiyo yanayozalisha mivutano isiyokuwa na tija, huyu kasema hivi yule naye anasema vile, hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake na kibaya zaidi watu ndani ya chama hawaaminiani, utasikia leo huyu katajwa msaliti, kesho yule, utafika wakati vyama vyetu havitakuwa na msafi, wanachama wote watakuwa wasaliti," alisema Profesa Baregu.

Asante Mjukuu wa Nape!. CCM Oyeeee, na zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM!.
 
Siku moja ukweli ukijulikana uliopo ndani ya chadema kuhusu mabele malando na mwesigwa baregu hamtaamini wote hao ni watumishi wa serikali ukawa zungukeni sana baada ya uchaguzi mkuu ndiyo mtayajua haya wakati huo mtakuwa peupe kama karanga.

Shikamoo Dada?
 
HALI inazidi kuwa mbaya ndani ya Kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kufuatia taarifa za mgogoro mkubwa uliopo kati ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.

Chanzo cha mgogoro huo ambao unafukuta, ni madai ya Slaa ya kutomwamini Mbatia anayedai ni pandikizi anayetumiwa na serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuvuruga umoja huo.

Inaelezwa, Slaa anamshutumu Mbatia kuwa ni Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, hivyo ni hatari kwa ustawi wa umoja huo, na kuna uwezekano akasababisha kusambaratika kwake iwapo ataendelea kuwepo.

"Ukiwa nje huwezi kuona hali halisi ya mambo, kwa tulio ndani ndio tunaona kila kitu, huu umoja hauwezi kufika popote maana watu hawaamiani hata kidogo na kuna migogoro kila kukicha"

"Sasahivi Slaa anashinikiza Mbatia aondolewe UKAWA, anadai akiachwa atavuruga mpango wa kwenda ikulu" kilisema chanzo chetu kilichopo ndani ya kambi ya UKAWA.

Chanzo hicho kilisema, msimamo huo wa Slaa umewapa wakati mgumu vongozi wengine wa kambi hiyo na wanaona wakimtosa Mbatia watasababisha mgawanyiko wa wanachama, hivyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza Katibu Mkuu huyo.

"Slaa hapendi kumuona Mbatia akiwa UKAWA, ila Mbatia ni muhimu zaidi kuliko Slaa kwenye umoja huu maana anawakilisha chama na iwapo chama chake kitatoka kutasababisha mpasuko, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa wakampuuza katibu mkuu, ila wakimpuuza unamjua mambo yake, ataanza vurugu ndani ya chama" kilisema chanzo chetu.

Aidha, mbunge mmoja wa CUF akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, baadhi ya wanachama wa UKAWA wanamshutumu Mbatia kuwa mmoja wa walioshinikiza kambi hiyo kususia mchakato wa Katiba mpya na kushawishi wasirudi bungeni.

"Kuna mambo yanatia mashaka sana na leo viongozi wetu wanajuta, uamuzi wa kususia bunge la Katiba haukuwa sahihi, vongozi wetu walipotoshwa kususia bunge. Naamini kama tungebakia bungeni na kushindana kwa hoja, kingeeleweka"

"Mbatia alikuwa kinara wa kusisitiza tusirudi na kuna taarifa feki zilikuwa zinakuja ambazo zilionekana wazi mchakato ungekwama, lakini tumeona kilichotokea, CCM na baadhi ya wabunge wa UKAWA wakaendelea na wameandika walichotaka, na kwa hali ilivyo katiba wanayotaka wao itapita" alisema mbunge huyo kutoka Zanzibar (jina tunalihifadhi).

Mbunge huyo alisema, hali hiyo inaonyesha wazi kuna watu ndani ya kambi hiyo wanatumika na CCM, na mbinu ya kushawishi UKAWA wasirudi bungeni ilikuwa ni maagizo maalum yenye lengo la kuwapa nafasi CCM kupitisha mambo waliyotaka kwenye Katiba mpya.

Taarifa zaidi zinasema, jambo jingine ambalo linampotezea imani Mbatia kwa baadhi ya viongozi wenzake, ni uhusiano wake na kigogo mmoja mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ingawa mwenyewe mara kadhaa amekuwa akikana madai hayo na kushusha lawama kwa CCM kuhusika kusambaza madai hayo.

Inaelezwa, Mbatia amekuwa karibu na kigogo huyo na wamekuwa wakikutana mara kwa mara nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salam kwa lengo la kupeana maelekezo ambayo hawana shaka yanalenga kufanya hujuma kwa kambi hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na mwandishi wa habari hizi wamesema, kambi ya UKAWA ipo kwenye wakati mgumu ukiachilia mbali mgawanyiko uliopo katika suala la kuteua mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, kuna hali ya kutoaminiana na kila mmoja anamuona mwenzake ni msaliti.

"Kabla hawajaungana Chadema waliwahi kukishutumu CUF kuwa ni tawi la CCM (CCM B), Wenje (Ezekiel Wenje) aliwahi kuwashutumu CUF kuwa ni chama cha mashoga, Chadema hao hao walishamuita Mbatia ni mbunge wa Rais Kikwete kwa kuwa aliteuliwa na Rais hivyo ni mbunge anayefuata maagizo ya CCM" alisema John Malingumu mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

Mchambuzi huyo aliongeza kuwa, kila mmoja ndani ya kambi hiyo ameungana na mwenzake kwa malengo binafsi, ila hakuna mwenye imani na mwenzake.

"Pale kuna unafki mkubwa, kila mmoja amebaki na historia yake kichwani ya mambo ambayo walifanyiana kabla hawajaungana, utakumbuka pia Chadema waligoma kuunda Kambi ya Upinzani na CUF, haya yote hayajafutika ingawa wanajifanya yote yamepita, ni uongo"

Hata hivyo, hali hiyo ya kutoamiana iliwahi kukemewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Prof. Mwesiga Baregu ambapo alisema, migogoro na migawanyiko inatokana na hali ya kutoaminiana huku wengine wakitengwa na kuitwa wasaliti.

“Matokeo ya hali hii ndiyo yanayozalisha mivutano isiyokuwa na tija, huyu kasema hivi yule naye anasema vile, hakuna mtu wa kumsikiliza mwenzake na kibaya zaidi watu ndani ya chama hawaaminiani, utasikia leo huyu katajwa msaliti, kesho yule, utafika wakati vyama vyetu havitakuwa na msafi, wanachama wote watakuwa wasaliti,” alisema Profesa Baregu.

Source
Uhuru na Mzalendo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom