Mbatia hoi bin taabani Vunjo

Mbatia hoi bin taabani Vunjo

Majasho

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2009
Posts
413
Reaction score
220
Mambo yamezidi kuwa mabaya kwa Mbatia jimboni Vunjo baada Ya wana ukawa kuanza kupigana baina Ya Chadema Na Nccr Mageuzi Kwenye Mkutano wake uliofanyika stendi Ya njia panda, Himo.

Tukumbuke kwamba takribani mwezi mmoja uliopita madiwani wa Chadema wanaogombea kata za Vunjo waligoma kumfanyia kampeni mgombea wa ukawa James Mbatia kwa madai kwamba anaua Chadema Vunjo Na kwa sababu aligoma kuwaachia Chadema kata 8 jimboni humo. Nccr Mageuzi waliweka wagombea udiwani katika kata zote 16 za jimbo hilo bila kuwaachia Chadema ilihali wenyewe walimwachia Mbatia agombee ubunge.

Mbowe alivyokuja Vunjo siku chache zilizopita Alitoa maelekezo kwamba kufanyike kura za maoni katika kata zote za jimbo la Vunjo baina Ya wagombea udiwani wa Nccr Na Chadema Na atakayeshinda apeperushe bendera Ya chama hicho.

Kura hizo zilibidi zifanyike Leo katika kata zote, Mbatia akisimamia uchaguzi huo katika kata Ya Njia panda wana Chadema walimuona live akiipendelea Nccr kitu kilichowapandisha hasira wana Chadema Na kuanza vurugu. Mbatia kuona ngumi Zinarushwa alikimbilia Kwenye Gari lake huku bodigadi wake akitumia nguvu za ziada asidhurike. Vijana walimrushia Matusi Ya nguoni Mbatia Na kumwambia hawamtaki.

Majeruhi walipelekwa polisi ili wapate pf3 ili wakimbizwe hospitalini, lakini wakati wakiwa polisi wagombea ubunge Augustino Mrema wa TLP Na Shirima wa CCM walitinga hapo polisi. Viongozi wa Nccr Na wao walifika polisi Na kuanzisha vurugu Mpaka polisi wakalazimika kupiga risasi hewani kuwatawanya watu.

Pia, kata Ya kirua Vunjo kusini nako ngumi zilitawala baada Ya wana Chadema kuona Nccr wakipendelewa ili mgombea wao apite.

Nitaendelea kuwajuza kilichotekea Kwenye kata nyingine Pindi habari zitapozipata.

Mbatia Mwenyewe alienda kujificha Kwenye ofisi Za chama hicho Njia Panda huku Vijana wa Chadema wakiendelea kumporomeshea Matusi
Na kusema hawamtaki aonekane Vunjo.
 
Mbatia hayuko hoi. Atashinda. Wa CCM ndie amechanganykiwa mpaka anataka kuua watu kwa risasi. Soma hapa:


Polisi yamhoji mgombea ubunge (CCM) Vunjo kwa kutishia bastola

Polisi mkoani Kilimanjaro, imemshikilia kwa zaidi ya saa tatu, mgombea ubunge wa Jimbo la Vunjo, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Innocent Meleck, baada ya kudaiwa kumtishia kwa bastola, muongoza watalii, Oscar Mosha (28), akiwa katika klabu ya usiku ya Pub Alberto ya mjini Moshi. Meleck (32), anadaiwa kufanya tukio hilo, akitumia bastola aina ya Bereta, iliyosajiliwa kwa namba H 56420, usiku wa Oktoba 2, akiwa ameongozana na baadhi ya wapambe wake.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, aliiambia Nipashe jana kwa njia ya simu kwamba, mgombea huyo alikuwa amekwenda kwenye klabu hiyo kwa ajili ya starehe na wakati akiwa ndani alifuatwa na mmoja wa wateja wa klabu hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Oscar ambaye alimweleza kuwa ameegesha gari lake vibaya na kuzuia magari mengine kutoka, jambo lililomuudhi. Ni kweli tukio hilo limetokea juzi saa 7:00 usiku katika klabu maarufu ya Pub Alberto, na huyo Innocent aliisalimisha bastola yake kituo kikuu cha polisi mjini Moshi, baada ya kufikishwa hapo.

Tumewahoji na tumewaachia kwa masharti ili kupisha uchunguzi zaidi, alisema Kamanda Ngonyani. Alisema, Innocent alipohojiwa na polisi kuhusu madai hayo, alidai kupigwa na kuumizwa sehemu ya jicho lake na hivyo alipatiwa fomu namba tatu ya matibabu (PF3) na kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi). Wakati mgombea huyo akidai kupigwa, mlalamikaji alidai kutishiwa kwa silaha na Innocent baada ya kumtaka akaliondoe gari lake ili apishe gari jingine lililokuwa likitaka kuondola eneo hilo.
 
Aisee ungekuwa binti ungeshatundikwa mimba 5 kwa umbea. Hata kama hayo unayosema ni ya kweli ww yamekuuma nn? Shame on you hebu nadi hizo pombe zakp ya ukawa tuachie wenyewe
 
Mwaka huu mbatia atafanyia kapeni chumbani kwake kama hajui vurugu za wana cdm amuulize zitto yaliyo kuwa yanamkuta hadi sasa hivi zitto kapata nafuu baada ya cdm kumpokea lowassa aliye kuwa na shutuma ndipo wafuasi wao wakaambiwa wafanye siasa za kisitarabu
 
macho_mdiliko

Mkuu usipindishe ukweli kwamba kuna vurugu Vunjo na Mbatia amezomewa kata ya Mwika Kusini
 
Last edited by a moderator:
Aisee ungekuwa binti ungeshatundikwa mimba 5 kwa umbea. Hata kama hayo unayosema ni ya kweli ww yamekuuma nn? Shame on you hebu nadi hizo pombe zakp ya ukawa tuachie wenyewe

Natoa habari Mkuu, Na wewe kama yanakuuma kwa nn unachangia au we ndugu wa Mbatia nn umeshikwa pabaya
 
macho_mdiliko

We kwanini usianzishe thread yako? Unakusudia kuficha nini?
 
Last edited by a moderator:
Mnapingana wenyewe jipangeni leteni taarifa iliyo sahihi
 
Hawawezi kumpa,jamaa bogasi sana,siasa hawezii!Kama mwenyekiti ameshindwa kukisimamia chama chake,watu wake walitaka kugombea ubunge wameonewa sana kwa kava ya chadema
 
Mwaka huu mbatia atafanyia kapeni chumbani kwake kama hajui vurugu za wana cdm amuulize zitto yaliyo kuwa yanamkuta hadi sasa hivi zitto kapata nafuu baada ya cdm kumpokea lowassa aliye kuwa na shutuma ndipo wafuasi wao wakaambiwa wafanye siasa za kisitarabu

Mbatia anajua fika hawezi kushinda jimbo la Vunjo
 
me ukawa nawashangaa ivi uukiachiwa kiti ndo tuseme una uhakika wa kushinda au?
 
Mbatia kam kakibaraka Ka ukawa tena bora wakapige chini 2 maana kanafiki sana
 
macho_mdiliko


Mkuu umeandika kishabiki na utumbo mtupu. Jaribu basi kufananisha matukio walau. Tukio la kina Mbatia ni kwingine na hili lako unalosemea lipo kwingine.

Tuzungumzie kwanza tukio lililoletwa ma mtoa mada! Kama vipi pita mbali kule
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom