Mbatia hoi bin taabani Vunjo

Mbatia hoi bin taabani Vunjo

Mbatia jimbo la Vunjo ni lake kwani Mrema keshakata tamaa amebakia kuwa mpambe wa mgombea wa ccm, kila siku usiku hukutana kupanga mipango ya mrema kumuuzia wafuasi wake au jamaa amrejeshee gharama zake mapema amsaidie kupiga Fitna nyingi kwa Mbatia, Lakini Ukweli na hali harisi ni Mbatia tu ambaye anakubalika zaidi ya wagombea wote.
 
Mbatia hana jipya Vunjo

Mrema na ccm wana jipya gani? Ujue mda mwingi usiku huutumia kupanga mbinu za kumhujumu Mbatia badala ya kunadi sera zao, Mrema sasa kaandaa gharama alizotumia mpaka sasa kampelekea mgombea wa ccm amrejeshee pesa zake ili amuuzie kura za watu wake kisha yeye azuge zuge kuwa yupo kwenye uchaguzi hadi mwisho lakini Ukweli Mrema hagombei tena bali sasa kaamua kuuunga mkono mgombea wa ccm.
 
Mi nadhani hakuna haja ya kumtupa Mrema. Wana vunjo wote bado wanamkubali sana na amejitahidi kutatua matatizo ya wananchi kwa asilimia 90. Sasa kwa nini wamtoe, ushabiki au. Nini hasa ambacho Mbatia safari hii ataweza kufanya. Hana lolote alishindwa kutimiza ahadi kipindi kile alichokuwa mbunge mpaka akakataliwa leo hii ana jipya gani tena.
Wana vunjo wala msidanganywe kabisa. Achaneni na huyo mchumia tumbo.
Chama chake nccr chenyewe kinamshinda na kinasambaratika leo ataweza ya Vunjo.

Huwez kumlinganisha mropokaji autwae mbatia na mzee wetu mrema

Mrema pamoja na uzee wake hua hanunuliki na haburuzwi huwa n mtu wa maamuz sahihu
Refer. Ukawa walivyokimbia na kuwasaliti wananchi wao waliowatuma kuwawakilisha wakati ule wa katiba
Alafu wanabak kulalamika
 
Mbatia Bungeni safari hii imekula kwake

Nasikia ameshakata tamaa na bunge
Saiv anajitahid kukitetea chama chake kipya kiitwacho chadema
Bila shaka atateuliwa na mbowe kuwa katibu mkuu
Maana kule hakunaga uchaguz wala demokrasia
 
aisee wengi sujui mmezoea kutukanwa daaa hivi unapajua moshi au wao sio WA kukurupuka kwa maneno mengi yasiyo na tija, mwaka huu kikwete hayupo so bunge ataliona kwenye tv tu

Acha uongo Vunjo wengi wapo busy hawafiki huku JF kujibu uongo wako lakini ukweli wa hali harisi ni kwamba Mrema yupo hoi sasa kaamua kuungana na mgombea wa ccm kumhujumu Mbatia.
 
Kama alimshindwa mdee,atamueeza Mrema?Jamaa hamna kitu paleee
 
Mbatia ameshikwa pabaya kila mahali. Ndani ya chama na viongozi wenzake na nje ya chama. Ananuka

Mbatia atakosa kila kitu
kuanzia uenyekiti wa chama
Mpaka ubunge

Baada ya uchaguz mwenyekiti wa chadema atakuwa n lowasa najuwa atamkumbuka kwa kumpatia ukatibu mkuj wa chadema
Wakati huo magufuli atakuwa ikulu zaman tu
 
Sisi vunjo tunaenda na Magufuri na mbunge wetu wa CCM ndugu shirima
 
Mbatia jimbo la Vunjo ni lake kwani Mrema keshakata tamaa amebakia kuwa mpambe wa mgombea wa ccm, kila siku usiku hukutana kupanga mipango ya mrema kumuuzia wafuasi wake au jamaa amrejeshee gharama zake mapema amsaidie kupiga Fitna nyingi kwa Mbatia, Lakini Ukweli na hali harisi ni Mbatia tu ambaye anakubalika zaidi ya wagombea wote.


Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni Mdee alimwita yeye kuwa ni Fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na CCM hivyo kuwataka wapiga kura wa jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.

Soma habari kamili

Na Happiness Katabazi
JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam John Utamwa , jana ilishindwa kutoa uamuzi wa ama hati ya madai katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge(NCCR-Mageuzi) dhidi ya mbunge Jimbo hilo Halima Mdee(Chadema) ifanyiwe marekebisho au la kwa maelezo kuwa bado hajakamilisha kuandaa uamuzi huo.

Wakili wa Mbatia, Mohamed Tibanyendera aliikumbusha mahakama hiyo kuwa jana kesi hiyo ilikuja kwaajili ya mahakama kutoa uamuzi huo na kwamba pande zote mbili zipo tayari kwaajili ya kupokea uamuzi huo.

Hata hivyo kwa upande wake Jaji Utamwa alisema hataweza kutoa uamuzi huo jana kwasababu bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo hivyo akaiarisha kesi hiyo ya uchaguzi hadi Septemba 29 mwaka huu, ambapo atakuja kuitolea uamuzi.

Hatua hiyo ya mahakama kutaka kutoa uamuzi kuhusu hati hiyo ya madai, kunafuatia pingamizi lilowasilishwa na wakili wa Mdee, Edson Mbogoro la kuiomba mahakama hiyo imwamuru mlalamikaji aifanyie marekebisho hati yake ya madai na kuyaondoa baadhi ya madai ambayo Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni Mdee alimwita yeye kuwa ni Fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na CCM hivyo kuwataka wapiga kura wa jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.

Mdee anadai tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake na Mbatia ndani ya hati hiyo ya madai zinamletea kinamkera na hataweza kuziandalia utetetezi na kusisitiza kwa kuomba mahakama hiyo imwamuru Mbatia aondee hizo tuhuma kwenye hiyo hati ya madai.

Novemba 25 mwaka 2010 Mbatia alifungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee(CHADEMA) kuwa ndiye aliyeshinda na ataliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Chanzo:Chazeti la Tanzania Daima la Septemba 22 mwaka 2011.
 
Back
Top Bottom