Elections 2010 Mbatia apinga vikali na kulaani uatafiti wa Synovate

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia amepinga vikali utafiti uliofanywa na Synovate na kuonyesha vyama vya upinzani vikiongozwa na Chadena wanaungwa mkono zaidi dhidi ya CCM.
Ifuatayo ni sehemu ya mazungumzo yake kama alivyonukuliwa na mwandishi wa gazeti la mwananchi

''Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema kuwa kuchukua watu 1,994 ili kuwakilisha Watanzania wenye uwezo wa kupiga kura ambao ni zaidi ya milioni 20, ni makosa.

“Watu 1,994 hawawezi kuwasilisha Watanzania milioni 20 ambao wana sifa za kupiga kura, lakini pia kwa wakati tulionao labda wangekuja na utafiti unaoleta ufumbuzi wa hali ngumu ya maisha tungewaelewa,” alisema Mbatia.
 
watu Mil 20 hawakupiga kura, hakumbuki wangapi walipiga kura? less than 10Mil?
 
Synovate wakae kimya, hii ni janja ya CCM ili kuwaweka sawa wale wabunge wanaokipinga chama chao cha CCM. Uthibitisho ni pale baada ya kutoka tangazo hilo wabunge wa CCM wamerudi katika msitari baada ya kuombwa wasiendelee kukikandamiza chama chao. Ndiyo maana wamepitisha budget ya Uchukuzi kinyemela.
 
Siwalisemaga huyu jamaa kuwa kuna wana watu wanatoka nae!
 
wanaleta janja ya nyani hiyo..mkiukubali utafiti huu litakuwa ni kosa sababu wanawaweka sawa ili waje kuchakachua karibia na uchaguzi mkuu kwa kuonyesha wa ccm anaongoza kwa 70%,..hata hapo igunga subiri uone utafiti wao wahuni hawa...ccm branch at work
 
Ata Mhadhiri wa Chuo cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, amesema "Nimesikia nikashangaa sana, mwaka mmoja tu tumetoka kwenye uchaguzi, mtu anaenda kufanya utafiti kutaka kujua Rais anayekuja, hii kweli itakuwa ni innovation (ugunduzi au maendeleo) ya sayansi ya utafiti" alisema Bashiru
 
Viongozi na wanachama wa NCCR - MAGEUZI wanatakiwa walione hilo kwani huyu kiongozi ni sawa na wale viongozi wa ccm. Si mkweli na
mwenye chuki na ubinafsi, sasa maana yake ni nini. Anathibitisha kama ana sifa za uongozi ni ndumilakuwili. je? kutakuwa na uwezekano
wa kupiga kura moja ya urais kwa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani. wakati yeye kashaonyesha udhaifu wake kwa mgombea
urais wa chadema. Huyu ni mtu wa kung'ang'nia madaraka. anahiyari ccm iendelee na upinzani wakose. Msimamo uweleweke wazi kama
2015 vyama vyote vya upinzani vielekeze nguvu za pamoja kwa mgombea mmoja ambaye atatoka chadema na kusiwe na mgombea
mwingine wa urais kutoka katika vyama vingine viwili vikubwa vya siasa. Kwa muundo huo ccm itakuwa umefika wakati wake wa kuwa
mpinzani. kila kitu kiko wazi ushindi ni wa moja kwa moja, kinyume cha hapo ni kupoteza wakati. na huyo kiongozi wa juu wa NCCR-
MAGEUZI hiyo nafasi yake ichukuliwe na mtu mwingine kabla ya wakati wa uchaguzi. Mipangalio mingine ni vyama kukaa chini na kuweka
msimamo mmoja.
 
Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia amepinga vikali utafiti uliofanywa na Synovate na kuonyesha vyama vya upinzani vikiongozwa na Chadena wanaungwa mkono zaidi dhidi ya CCM.
Ifuatayo ni sehemu ya mazungumzo yake kama alivyonukuliwa na mwandishi wa gazeti la mwananchi

''Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema kuwa kuchukua watu 1,994 ili kuwakilisha Watanzania wenye uwezo wa kupiga kura ambao ni zaidi ya milioni 20, ni makosa.

“Watu 1,994 hawawezi kuwasilisha Watanzania milioni 20 ambao wana sifa za kupiga kura, lakini pia kwa wakati tulionao labda wangekuja na utafiti unaoleta ufumbuzi wa hali ngumu ya maisha tungewaelewa,” alisema Mbatia.

kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.
 
Ata Mhadhiri wa Chuo cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, amesema "Nimesikia nikashangaa sana, mwaka mmoja tu tumetoka kwenye uchaguzi, mtu anaenda kufanya utafiti kutaka kujua Rais anayekuja, hii kweli itakuwa ni innovation (ugunduzi au maendeleo) ya sayansi ya utafiti" alisema Bashiru

kwani huwa inatakiwa kusubiri muda gani ndo ufanye utafiti?
 
Mimi utafiti wangu unaonyesha Mhe. Mbatia ndiye anaongoza, sijui ni kwanini anatumia nguvu nyingi kuongea ikiwa ana-deserve kuwa nambari wani.
Hureeeee Mbatia.
 
Huwezi kufanya utafiti unaowajumuisha watu ambao tayari walisha gombea urais kama Dr. Slaa na Prof Lipumba na watu kama Sita na Mwinyi watu ambao hawajawahi kugombea urais, matokeo hayatakuwa sahihi.
 
Ingawa hatuuhitaji huu utafiti wakinafiki wa hawa sinavitu ila kutuletea kile alichosema huyu mwanasiasa aliyechoka Mbatia nikulilidhalilisha jamvi kupoteza muda wake kumjadili huyu kiumbe.
 
Back
Top Bottom