Mkutano wa James Mbatia na Waandishi wa Habari Wazuiwa kwa Maelekezo kutoka Juu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,550
217,832
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba Mkutano ulioandaliwa na James Mbatia , kiongozi aliyedaiwa kutimuliwa NCCR MAGEUZI , Umezuiwa.

Mbatia alipanga kukutana na Waandishi katika Hotel ya Regency Park Mjini Dar es Salaam leo saa 7 mchana .

Taarifa zaidi zinadai kwamba Mkutano huo umezuiliwa kwa Maelekezo kutoka Juu .
 
Mbatia kipenzi cha Jiwe, nashangaa Chadema mnavyo mshobokea huyu jamaa nikikumbuka mwaka juzi alivyokuwa akitamba yeye na Selasini wakitukana Chadema na kununua viongozi wao kwa fedha walizopewa na Jiwe

Mtu aliyekuwa upande wa Jiwe siwezi kumtetea kwa lolote lile kwenye masuala ya utawala wa sheria,
 
Mbatia kwa sasa hana chake tena huko NCCR- MAGEUZI. Akubali yaishe na maisha yaendelee. Kama bado anafurukutwa na siasa za upinzani/mageuzi, basi aanzishe chama chake au arudi tu nyumbani..... kule wanakoendelea kulamba asali kwenye buyu....
 
Hivi kwanini ccm inasimamia mapinduzi ya NCCR ?
Kwani CCM ndio iliyompindua? Msitake matatizo yenu kuipakazia CCM, maana wewe mtani wangu kwa akili yako unaweza kusema hapa kuwa hata Mbowe kuwa madarakani muda mrefu bila kubadili na kuleta mawazo mapya Ni CCM iliyomuweka hapo, Hata kushindwa kwenu kujenga ofisi utasema Ni CCM Ndio chanzo, Hata kutafuna kwenu Ruzuku zote na michango ya akina Sabodo utasema Ni CCM Ndio ilisema mtafune, Hata vijana wenu kukosa adabu na kuwa na matusi midomoni mwao utasema Ni CCM Ndio imechangia, Nasema hivi pambaneni na Hali zenu hukohuko msitake kuisingizia CCM
 
Mbatia kipenzi cha Jiwe, nashangaa Chadema mnavyo mshobokea huyu jamaa nikikumbuka mwaka juzi alivyokuwa akitamba yeye na Selasini wakitukana Chadema na kununua viongozi wao kwa fedha walizopewa na Jiwe

Mtu aliyekuwa upande wa Jiwe siwezi kumtetea kwa lolote lile kwenye masuala ya utawala wa sheria,
uko sahihi , hapa hatetewi Mbatia , inatetewa Sheria tu , Kama Mahakama ilizuia akina Selasini kufanya Mkutano , imekuwaje wakaufanya ?

Shetani hana rafiki , tukiacha Mahakama ikapuuzwa , kesho yatakuja mazito zaidi.
 
Acha watu wajifunze kwanza ndio watajua umuhimu wa utawala wa sheria
Watu wanaoshangilia utawala mbovu na kukejeli wahanga wa uonevu linapowakuta acha wapambane kivyao ili wapate adabu
 
Mbatia kipenzi cha Jiwe, nashangaa Chadema mnavyo mshobokea huyu jamaa nikikumbuka mwaka juzi alivyokuwa akitamba yeye na Selasini wakitukana Chadema na kununua viongozi wao kwa fedha walizopewa na Jiwe

Mtu aliyekuwa upande wa Jiwe siwezi kumtetea kwa lolote lile kwenye masuala ya utawala wa sheria,
Hatumshabikii....
 
Historia inaonyesha kuwa kila yakitokea machafuko, migogoro, usaliti ama hata mapinduzi ndani ya vyama makini vya upinzani, basi nyuma yake tambua yupo "main sponsor" ambaye ni CCM.

Makada wa CCM kwa kutumia vyombo vya dola ndiye muhusika mkuu wa hujuma dhidi ya demokrasia ya kweli hapa nchini. Chama hiki kilidhamiria kuifuta CDM, japo kilishindwa kufanya hivyo, bado kimeacha alama ya kihuni mpaka hivi sasa kwa kile kinachoitwa kundi la COVID 19 ndani ya Bunge.

Ukiangalia yaliyotokea kwa CUF na NCCR Mageuzi ndipo utatambua kuwa shetani hana rafiki. CCM imeshindwa ushindani katika medani huru za kisiasa, kilichobakia ni kutumia ghiriba, hujuma na mbinu za kihuni ili izidi kubakia madarakani.
 
Mbatia kipenzi cha Jiwe, nashangaa Chadema mnavyo mshobokea huyu jamaa nikikumbuka mwaka juzi alivyokuwa akitamba yeye na Selasini wakitukana Chadema na kununua viongozi wao kwa fedha walizopewa na Jiwe

Mtu aliyekuwa upande wa Jiwe siwezi kumtetea kwa lolote lile kwenye masuala ya utawala wa sheria,

Kabisa, maana huyo Mbatia na Lipumba waliitwa kabisa na dhalimu baada ya kuwa na kitisho cha watu kususia uchaguzi. Baada ya kuitwa na Magufuli wakawalisha maneno. Mbatia akaanza hujuma za wazi dhidi ya CDM. Kila alipoenda akawa anaonyesha kuwa CDM wanataka madaraka ili wauze nchi kwa wazungu! Siwaelewi kabisa wanacdm wanaomsupport huyo Kibaraka.
 
Back
Top Bottom