Mbatia aibua madudu mitihani darasa la 7!

Mbatia aibua madudu mitihani darasa la 7!

Jamani hivi chama chetu makini kimeishiwa kabisa wabunge wanao weza kuona mapungufu kama hayo? Ifike wakati Mwigulu ukosoe serikali kuliko kutujaza chuki dhidi ya Chadama kila kukicha!Wengine wanadiriki kusema Mh.Mbatia anatafuta umaarufu!Bila shaka watu hao wanasomesha watoto wao katika shule za watakatifu kwahiyo hawaoni tatizo lililoko mbele.
 
mbatia hatafuti sifa bali ndiye mpinzani pekee w serikali aliyesoma vzr Tanzania anajua elimu n nn n wp kwny makosa ,,,
hao wngn wny secondary za kilatino za hk Italy hawajui shida za mtoto w kitanzania wao n kelele n maandamano

Unajua Mbatia kasoma Wapi, sory nijibu ili alafu nije najibu lako vizuri au Tusi kubwaaa...
 
Siku za nyuma (enzi za mwalimu) shule binafsi walikuwa wanaenda vijana waliofeli ambao wazazi wao wanaelewa umuhimu wa elimu lakini pia wana uwezo. Enzi za leo shule binafsi wanaenda watoto wa wanaoelewa elimu bora ni nini, wana uwezo wa pesa, pia watoto wenye uwezo darasani maana mchujo ni balaa. Matokeo ya equation hii ni kwamba walimu wote wenye uwezo wako shule binafsi wanalipwa vizuri na wako highly motivated. Siku ya mwisho shule za binafsi performance yake nzuri wakati shule za umma performance very poor. Walimu wa umma wanalipwa pay sawa na posho ya siku moja ya mbuge, mazingira ya kazi kama jela, hamna kiongozi anayewasikiliza. Umewahi kuona diwani wa darasa la saba akimgombeza H/Master/Mistress mwenye degree kwenye shule ya kata? Hadithi ni nyingi sana halafu unategemea Big Results! Nakubaliana na Mwinjilisti Kamala Kasyupa kwamba wasomi wa Tanzania kwa hiyari yao wameamua kukubali kuwa ma-housegirl/boy wa wanasiasa.
 
Ha ha haaaa..... Makosa mengi sana hutokea katika idara za serikali hasa "typing errors". Hii inachangiwa na watumishi kufanya kazi kwa mtindo wa "Bora liende" ili mradi mishahara wanapokea na vijisemina wanahudhuria. Ni kulipualipua tu na mara nyingi hakuna mtu anaye hakiki.
 
Sishangai kutokea makosa hasa kwenye masuala sensitive kama mtihani. Kuna watendaji wa serikali wameaminiwa kuamua masuala nyeti bila kuhasisha watu wengine. Si ajabu kukumbana na "typing errors" kwenye documents muhimu za serikali ikiwemo mitihani na barua mbalimbali tena zikiwa zimesainiwa. Zinapitishwa tu ili "mradi liende". Hakuna tena uzalendo kabisa kwa sasa kwenye idara nyingi za serikali hasa Elimu. Mbatia is right!
 
Tell your head of the Nation that ''BIG RESULT NOW without BIG SALARIES NOW is a BIG PROBLEM NOW''.
 
Ofcourse huo mtihani kipanga kama mimi ningeufanya lisaa limoja. Hata uwezo wao mdogo yani mtihani wa la saba masaa mawili. Poor prof
 
Mbatia na yeye asitafute umaarufu au asipige kelele ktk swala la vitabu tu au mitihani tu. Aende Mufindi huko akaone shule haina madawati wamebumba udongo ndo madawati wanakalia wanafunzi na kuandikia. We unadhani hapo itapatikana elimu kweli?

Alafu Hawa viongozi wa chama cha madawa wanajisifu eti miaka 50 ya uhuru eti wamefanya makubwa. Makubwa wapi au makubwa katik swala la ufisadi na kushindwa kisimamia serikali na mashirika yote vzr ndo maana twaona tumekua lango la madawa na tumekua lango la bidhaa feki yani tumekua hivyo hivyo.

Bwana Ntuzu nadhani tumpe hongera huyu kijana kwa kuweza kuliona hilo la mitihani. Ushauri wako kuhusu kutokuwa na mazingira mazuri ya kusomea ni muhimu sana na akipatikana mtu mwingne mwenye uchungu au ujasiri basi anafanya hivyo kwa kuendelea kuibua mengne. Tusitarajie Mbatia atafanya kila kitu.
 
Jamani wana jf, tufikie mahali tutamke ule ukweli tu. Mh. Mbatia si kwamba amekomalia elimu ya msingi tu. Ameona badala ya kuhangaika na mengi atufungue macho hata kwa hili moja tu. Hebu twende na thread yetu tusitoke nje. Swali ni kwamba, hivi kweli serikali hii sikivu hivi, yenye mikakati mizuri kama Big rezalts naooo! Wow! What a big say. Keli hii, nakubali ni Big results now. Mtihani, Dr. Shukuru, umetungwa, umeprintiwa, kwa kodi zitu. Haukuhakikiwa, ukapelekwa kwa watahiniwa, Wilaya mbalimbali wala sio Dar tu. Hizi zote ni gharama za kodi yangu. Mpaka sasa, hiyo Big Results Now, haijakuona hufai???????? Mimi ni mdogo saana Tz lakini nasema; HUFAI, HUFAI, HUFAI. Funika tu uso uondoke. Acheni kufuturisha watu, nendeni kwenu tuu. Mpeni nafasi Mh. Rais aweke watu wenye uwezo mmeonyesha; HAMFAI.
That is a product of your Big rezalts naooooo.
 
Ndugu yangu Ntuzu Ntuzu, Tatizo la madawati Mufindi ni la serikali kuu kwaeli? Mufindi ndo wilaya ya kwanza Tanzania kwa kuzalisha mbao, tuna msitu mkubwa pale wa Taifa (SAOHILL) kwa nini halmashauri husika isijiwekee lengo kwa kila mwaka kutengeneza madawati kwa ajili ya shule zake?

Kuna mkurugenzi pale, Kuna mwenyekiti wa halmashauri, baraza la madiwani, pia kuna maafisa mipango wa halmashauri, kazi yao ni nini kule?

Na hii sii kwa halmashauri moja hapa Tanzania, ni halmashauri zote unazozijua wewe.
 
Last edited by a moderator:
yani upeo wako wa kufikiri ndio unafikia hapo??? Kwa akili yako unadhani mbatia ndio the most educated mpinzani???
Vipi kuhusu prof. Lipumba, prof. Safari, prof. Baregu, dr. Slaa, dr. Kitila, zitto, etc etc
Jipange dogo sio unaropoka tu hovyo hovyo..[/QUOT

Hata mimi nimemshangaa sana huyo dogo kwa jinsi alivyokurupuka nakujikuta akiropoka asichokijua hata kidogo, Duh!! Hili nalo ni janga kuwa na vijana wa aina hii ktk Taifa linalohitaji mabadiliko ktk nyanja zote.
 
Nilishawahi kumbana na simultaneous equations Mara mbili nilipokuwa standard seven.
 
Mbatia na yeye asitafute umaarufu au asipige kelele ktk swala la vitabu tu au mitihani tu. Aende Mufindi huko akaone shule haina madawati wamebumba udongo ndo madawati wanakalia wanafunzi na kuandikia. We unadhani hapo itapatikana elimu kweli?

Alafu Hawa viongozi wa chama cha madawa wanajisifu eti miaka 50 ya uhuru eti wamefanya makubwa. Makubwa wapi au makubwa katik swala la ufisadi na kushindwa kisimamia serikali na mashirika yote vzr ndo maana twaona tumekua lango la madawa na tumekua lango la bidhaa feki yani tumekua hivyo hivyo.

Wewe binafsi kuhusu hayo matatizo ya Mufindi, ulichukua hatua gani? Wabongo bwana, tumekalia kulalamika tu bila sisi wenyewe kuchuka hatua! Bora heri huyu Mbatia, mchango wake tunauona ktk masuala ya elimu.
 
mbatia hatafuti sifa bali ndiye mpinzani pekee w serikali aliyesoma vzr Tanzania anajua elimu n nn n wp kwny makosa ,,,
hao wngn wny secondary za kilatino za hk Italy hawajui shida za mtoto w kitanzania wao n kelele n maandamano

Nchi ya wauza unga itaheshimu vipi elimu?
 
Back
Top Bottom