Mbarawa ataka uchunguzi zaidi ufanyike Mradi wa Maji Chalinze

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amegeuka “mbogo” baada ya mkandarasi kutoka kampuni ya Shanx aliyekabidhiwa mradi wa maji Chalinze Mboga kudanganya vipimo vya ulazaji wa bomba huku akidai nyongeza ya gharama.

Waziri amekuta mitalo ya kulaza mabomba ikiwa mifupi mita 1.6 tofauti na makubaliano yaliopo kwenye mkataba ambao ni 1.8.

Pia amesema atakutana na mkandarasi na Dawasa ili kupitia upya maombi ya mkandarasi juu ya ongezeko la gharama za uchimbaji na ulazaji bomba.

Waziri Mbarawa amehoji gharama za uchimbaji na ulazaji bomba ya bilioni 3.9 kuwa ni kubwa, amesema ataunda tume itakayopitia upya mradi wa Chalinze Mboga
 
Tafadhali Mbarawa nenda Morogoro Kihonda Kilimanjaro kaibue madudu mengine tena makubwa, mabomba yaliyolazwa ni 4" lakini wameandika wamelaza 6" kwanini wanaihujumu serikali ambayo ndiyo imewapa ajira?
 
Back
Top Bottom