Mbarali wametoa kauli wengine je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbarali wametoa kauli wengine je?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiroroma, Jun 2, 2009.

 1. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Wakaazi wa Mbarali Mkoani Mbeya juzi wameamua kuwatolea uvivu kauli ya ukweli Kamati ya Bunge iliyotembelea shamba la Mbarali lililobinafsishwa katika mazingira ya kumpa mwekezaji asiye na tija kwa Taifa.Wakazi hao wemeweka bayana kwamba hawatapiga kura katika uchaguzi ujao,Kwa jinsi serikali ilivyowatendea.Je huko Kilombero, Basutu,Kahama,Chimala Ruvu,Mvomero na kwingineko ambako wananchi wamezulumiwa ardhi yao kwa kigezo cha uwekezaji watasemaje?Je wafugaji wa kimasai na kisukuma wanaohangaishwa huku na kule watasemaje?Elimu ya juu je?Wafanyakazi wanaopigwa dana dana ya kuongezewa mishahara wao watasemaje?Wamachinga wa Ilala ,Kiboroloni,Mbauda,Mwanjelwa ,Mwaloni wanatoa kauli gani?Je wakulima wadogo wadogo kule Lushoto,Mahenge,Igurusi walioahidiwa power Tillers je?Achalia mbali kauli ya maisha bora kwa kila Mtanzania.Mabango yaliyowekwa barabarani wakati ule tumeyahifadhi,Wanachi watayaweka kwenye vituo vya kupigia kura na alama ya kuuliza kulikoni???
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Maneno tu hayo mkuu, subuiri ,atokeo ya kura unaweza kushangaa kuwa huko Mbarali ndiko chama kinachoongoza serikali wanayoichukia ndicho kitaongoza kwa kupata kura nyingi
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  MN,

  Tatizo ni kwamba hata barua au matamko kama hayo hutayarishwa na wanasiasa badala ya kuacha ownership kwa wananchi wenyewe.

  Kama tunataka mabadiliko ni lazima tuwashirikishe wananchi; wao ndio waelemishwe kuhusu kupotea kwa haki zao na kama wanaona kuna dhuluma basi waandike hizo barua au matamko.

  Hizi barua za kuandikwa na kundi dogo huku wakijifanya wanawakilisha wananchi wote ndio zinadanganya watu na baadaye matokeo yanakuwa tofauti.

  Sina uhakika na hili la Mbarali lakini kwa taarifa kama hizi kwa sehemu zingine uzoefu ni kwamba zinaandikwa na kundi dogo na kunakuwa hakuna uwakilishi wa kutosha wa wananchi wa kawaida.
   
 4. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kiloloma, Chimala ni sehemu ya Mbarali na wananchi wa hapo ndio hasa wenye mgogoro na serikali kuhusu kuuzwa kwa shamba la Kapunga. Hata hiyo kauli ni wananchi hao wa Chimala.

  wakulima hao wadogo wilayani Mbarali, hususani wale wa Chimala wamehangaika sana kupigania hilo shamba la kapunga lakini serikali ilitia pamba masikioni, na hata ilipobaini kuwa mwekezaji huyo ni mbabaishaji bado imeendelea kumlinda.

  Baada ya kuuzwa kwa mashamba ya Mbarali na Kapunga, uchumi wa wilaya hiyo umeshuka sana, miji ya Rujewa, Ubaruku, Igurusi na Chimala imedorora kutokana na kupungua kwa mzunguko wa pesa uliokuwa ukichochewa zaidi na kilimo cha mpunga.

  Mathalani, kabla ya shamba la Kapunga kuuzwa, SACCOS ya wakulima wa Chimala ilifikia hatua ya kuchukua mkopo wa hadi shilingi bilioni tatu kutoka CRDB kupitia utaratibu wa stakabadhi ghalani, lakini hivi sasa hawana uwezo huo.

  Ni wazi hiyo kauli itakuwa ya wakulima wadogo wilayani humo na sio ya kikundi kidogo kwani hawajaanza leo kupigania haki yao, walianza tangu serikali kutangaza kuyauza mashamba hayo lakini walikandamizwa na viongozi walafi wa serikali ya CCM wakiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Dorolo, Mungai na Ngasongwa.
   
 5. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Toka lini kutokupiga kura kukabadilisha hali? ilitakiwa waseme hatutakipa CCM kura ndio tutawaelewa.Halafu ndugu zangu hawa wa vijijini musiwaamini hata siku 1,kanga na fulana hasira zote kwisha.Kumbukeni 95 hapohapo Mbarari mbunge aliopita alivunja rekodi kwa kupata kura nyingi nchi nzima(zaidi ya 90%)pamoja na juhudi za kina Mrema.
   
 6. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao wakazi hawajasikia "bailout' inakuja nini?Wanajuaje mwekezaji wao yupo 'accommodated' kwenye hiyo stimulus plan inayokuja?

  Watulie waache kelele!
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kanga na nguzo za umeme zikitandikwa barabarani,fulana na shilingi elfu kumi kila mmoja watatoa tu kura kunakazi sana angalau wameonyesha hasira zao
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mkoa wa Mbeya na Mbarali ni CCM dam dam!

  sasa nani wa kumlaumu?
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu hakuna kitu. Somo la Busanda liko kila mahali katika nchi hii. CCM watachukua na Biharamulo mashariki pamoja na fyongo zote wanazowafanyia Watanzania. Maadamu hao watu wote wamefanywa ndondocha kwa kutojua hatua za kuchukua pale ambapo watawala wao wamewatelekeza, watarudishwa kundini kilaini na kuipa CCM ushindi wa kishindo iwekwenye chaguzi ndogo, 2010 au 2015!!

  Kwa wale ambao tulikuwa vyuoni miaka ya 1990, nani aliamini kuwa ipo siku wanavyuo wanaweza kufaa jezi za kishenzi za kijani? Lakini baada ya kudanganywa na mikopo ya 100% mwaka 2005 kilitokea nini? Watanzania ni kama watoto wadogo. Unamchapa sana hata pale ambapo hajakosea au unamdanganya kuwa ukirudi mjini utamletea pipi ila baada ya muda mfupi bila kutimiza ahadi hata moja anakengeuka na kuanza kukuimbia nyimbo za shuleni kwao. Sina imani tena na watu wa dizaini ya Busanda!!
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280

  kususia uchaguzi sio suluhisho...
  Dawa ni kutoipigia kura ccm kwa kuwa imeshindwa kutukomboa kutoka kwenye lindi la umaskini
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwa vile bado wana hamu na sisiemu yao wacha wakome na shida zao.
  Tutaungana nao katika malalamiko yao watakapoonekana kuonyesha kwa vitendo kukerwa na vitendo vya mabosi wao sisiemu. Napo ni kwa kuwanyima kura 2010. Mbali na hivyo wasiwe na tegemeo lolote zaidi tu ya kuona wananyanyaswa katika nchi yao.
   
Loading...