MBARALI: Rais Samia aifutilia mbali Government Notice Na. 28 ya mwaka 2022 iliyowafukuza Wananchi wasilime Wala kufuga katika bonde la Usangu

View attachment 2754590

Habari Njema sana,

MAKAMU Mwenyekti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Upande wa Bara Abdulrahaman Kinana amewaambia wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuwa Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekubali ombi lao la kuendelea na shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo lililozuiwa kupitia tangazo la Serikali la GN 28, kama ilivyokubaliwa mwaka jana.

Tangu kutolewa kwa katazo hilo, wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa mchakato wa kufikia maamuzi hayo haukuwa shirikishi na kuiomba serikali kuliondoa katazo hilo ambalo linaathiri ustawi wa maisha yao na kipato chao kama mtu mmoja mmoja.

Akizungumza wakati akihitimisha kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, zilizofanyika katika Kijiji cha Chimala hapo jana Makamu Mwenyekiti Kinana alisema mgombea Ubunge wa CCM Bahati Ndingo, Madiwani wa CCM, Viongozi wa CCM na wananchi walimueleza amuombe Rais Samia waendelee kulima wakati suala hilo linazungumzwa.

“Nimemueleza Rais jana kuwa wananchi wa Mbarali wanaomba waendelee kulima kwa sababu msimu unaanza mwezi ujao (Oktoba) na Rais akasema sawa waendelee, kwa yale maeneo yote yaliyoruhusiwa mwaka jana Rais amekubali mwendelee kulima,” alisema.

Akizungumzia ombi la mgombea ubunge kuhusu ujenzi wa barabara iliyokaa muda mrefu kutoka Lujewa, Madibila hadi Mafinga, Kinana alisema atawasiliana na wahusika (Waziri wa Ujenzi) ili ujenzi wa barabara hiyo uanze kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Awali wakati akiomba kura Bahati Ndingo Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Mbarali, alitumia nafasi hiyo kuelezea masuala mbalimbali yanayoendelea katika wilaya hiyo yakiwemo maendeleo makubwa ambayo yamefanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia.

Bahati alikiiomba Chama na serikali kuangalia upya changamoto ya migogoro ya ardhi iliyopo ndani ya wilaya hiyo. Alisema asilimia zaidi ya 90 ya wananchi wa Wilaya ya Mbarali ni wakulima, hivyo ardhi ndio maisha yao na ndio uchumi wao.

Bahati alieleza kuwa tangazo la GN 28 linaathiri maisha ya wananchi wa wilaya hiyo na kuomba lipitiwe upya.

“Migogoro ya ardhi ndio inafanya wilaya hii iwe nyuma. Unapotuona hapa zaidi ya asilimia 90 ni wakulima, linapokuja suala la ardhi sisi hatuitafuti kwa kujengea maghorofa, hatutafuti ardhi kujenga nyumba tunatafuta kwaajili ya shughuli za kilimo” alisema.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Francis Mtega kufariki dunia Julai Mosi mwaka huu.

== ==

Cc: Balile
Cc: Mwakibinga

Hiyo ni rushwa pia!kwa nini tangazo litoke wakati huu?
 
Yaani ccm wamewafanya wananchi kama mazombi, kwani hiyo government notice iliwekwa na wachina au wa Kenya, au, chadema? Yale yale, unatengeneza tatizo, harafu unalitatua, na wananchi wanatakiwa wakinge meno nje, kushangilia!
 
Serikali ni taasisi kubwa sana ongeza umakini kiongozi
 
Zawadi kwa Mama Samia
IMG-20230920-WA0006.jpg
 
View attachment 2754590

Habari Njema sana,

MAKAMU Mwenyekti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Upande wa Bara Abdulrahaman Kinana amewaambia wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuwa Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekubali ombi lao la kuendelea na shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo lililozuiwa kupitia tangazo la Serikali la GN 28, kama ilivyokubaliwa mwaka jana.

Tangu kutolewa kwa katazo hilo, wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa mchakato wa kufikia maamuzi hayo haukuwa shirikishi na kuiomba serikali kuliondoa katazo hilo ambalo linaathiri ustawi wa maisha yao na kipato chao kama mtu mmoja mmoja.

Akizungumza wakati akihitimisha kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, zilizofanyika katika Kijiji cha Chimala hapo jana Makamu Mwenyekiti Kinana alisema mgombea Ubunge wa CCM Bahati Ndingo, Madiwani wa CCM, Viongozi wa CCM na wananchi walimueleza amuombe Rais Samia waendelee kulima wakati suala hilo linazungumzwa.

“Nimemueleza Rais jana kuwa wananchi wa Mbarali wanaomba waendelee kulima kwa sababu msimu unaanza mwezi ujao (Oktoba) na Rais akasema sawa waendelee, kwa yale maeneo yote yaliyoruhusiwa mwaka jana Rais amekubali mwendelee kulima,” alisema.

Akizungumzia ombi la mgombea ubunge kuhusu ujenzi wa barabara iliyokaa muda mrefu kutoka Lujewa, Madibila hadi Mafinga, Kinana alisema atawasiliana na wahusika (Waziri wa Ujenzi) ili ujenzi wa barabara hiyo uanze kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Awali wakati akiomba kura Bahati Ndingo Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Mbarali, alitumia nafasi hiyo kuelezea masuala mbalimbali yanayoendelea katika wilaya hiyo yakiwemo maendeleo makubwa ambayo yamefanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia.

Bahati alikiiomba Chama na serikali kuangalia upya changamoto ya migogoro ya ardhi iliyopo ndani ya wilaya hiyo. Alisema asilimia zaidi ya 90 ya wananchi wa Wilaya ya Mbarali ni wakulima, hivyo ardhi ndio maisha yao na ndio uchumi wao.

Bahati alieleza kuwa tangazo la GN 28 linaathiri maisha ya wananchi wa wilaya hiyo na kuomba lipitiwe upya.

“Migogoro ya ardhi ndio inafanya wilaya hii iwe nyuma. Unapotuona hapa zaidi ya asilimia 90 ni wakulima, linapokuja suala la ardhi sisi hatuitafuti kwa kujengea maghorofa, hatutafuti ardhi kujenga nyumba tunatafuta kwaajili ya shughuli za kilimo” alisema.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Francis Mtega kufariki dunia Julai Mosi mwaka huu.

== ==

Cc: Balile
Cc: Mwakibinga
Unatengeneza tatizo na kulitatua, pia ni aina mpya ya rushwa kwa wapiga kura. Hata hivyo haya yote yanajilikana kwa watu wote makini.
 
Wenzie wapo UNGA(United Nations General Assembly) wanatoa hotuba za kibabe na kutafuta connections za kidiplomasia, ye ye yupo mikoani anarembua macho, na kudanganya wananchi
 
UNGA yupo makamu wa Rais, Connections hazitafutwi UNGA zinatafutwa kwenye simu tu hapahapa Bongo,
 
View attachment 2754590

Habari Njema sana,

MAKAMU Mwenyekti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Upande wa Bara Abdulrahaman Kinana amewaambia wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuwa Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekubali ombi lao la kuendelea na shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo lililozuiwa kupitia tangazo la Serikali la GN 28, kama ilivyokubaliwa mwaka jana.

Tangu kutolewa kwa katazo hilo, wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa mchakato wa kufikia maamuzi hayo haukuwa shirikishi na kuiomba serikali kuliondoa katazo hilo ambalo linaathiri ustawi wa maisha yao na kipato chao kama mtu mmoja mmoja.

Akizungumza wakati akihitimisha kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, zilizofanyika katika Kijiji cha Chimala hapo jana Makamu Mwenyekiti Kinana alisema mgombea Ubunge wa CCM Bahati Ndingo, Madiwani wa CCM, Viongozi wa CCM na wananchi walimueleza amuombe Rais Samia waendelee kulima wakati suala hilo linazungumzwa.

“Nimemueleza Rais jana kuwa wananchi wa Mbarali wanaomba waendelee kulima kwa sababu msimu unaanza mwezi ujao (Oktoba) na Rais akasema sawa waendelee, kwa yale maeneo yote yaliyoruhusiwa mwaka jana Rais amekubali mwendelee kulima,” alisema.

Akizungumzia ombi la mgombea ubunge kuhusu ujenzi wa barabara iliyokaa muda mrefu kutoka Lujewa, Madibila hadi Mafinga, Kinana alisema atawasiliana na wahusika (Waziri wa Ujenzi) ili ujenzi wa barabara hiyo uanze kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Awali wakati akiomba kura Bahati Ndingo Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Mbarali, alitumia nafasi hiyo kuelezea masuala mbalimbali yanayoendelea katika wilaya hiyo yakiwemo maendeleo makubwa ambayo yamefanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia.

Bahati alikiiomba Chama na serikali kuangalia upya changamoto ya migogoro ya ardhi iliyopo ndani ya wilaya hiyo. Alisema asilimia zaidi ya 90 ya wananchi wa Wilaya ya Mbarali ni wakulima, hivyo ardhi ndio maisha yao na ndio uchumi wao.

Bahati alieleza kuwa tangazo la GN 28 linaathiri maisha ya wananchi wa wilaya hiyo na kuomba lipitiwe upya.

“Migogoro ya ardhi ndio inafanya wilaya hii iwe nyuma. Unapotuona hapa zaidi ya asilimia 90 ni wakulima, linapokuja suala la ardhi sisi hatuitafuti kwa kujengea maghorofa, hatutafuti ardhi kujenga nyumba tunatafuta kwaajili ya shughuli za kilimo” alisema.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Francis Mtega kufariki dunia Julai Mosi mwaka huu.

== ==

Cc: Balile
Cc: Mwakibinga
Hongera watu wa MBARALI
 
Back
Top Bottom