Aisee ,umenikumbusha niitafute bonge la movie hiko kipande cha Jarumani kumuona dogo alafu akapiga kimnya umenikumbusha miaka kama 15 nyuma ,
Kitaani natembea ghafla nikaona dogo anakuja mbio kachanganyikiwa ,kumbe ni mwizi na walikua wanafukuza kimnya kimnya waue , huruma tu ya ubinadamu ikaniingia ,
Nilimuona dogo anaingia kwenye kichaka fulani huku shahidi nikiwa mimi tu ,njemba kufika ndio nikazidi kujua nia yao ni uhai walitafuta huku wakitweta haiwezekani mabata yetu kila siku yaibiwe,
Ndipo mmoja akaniuliza hujamuona dogo kavaa tisheti nyekundu hapa,
Nilikataa kata kata kabisa yani huku dogo najua kabisa alipo.