1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,304
Mazungumzo yasiyosikika ni asilimia tisini ya mazungumzo yetu yote yanayosikika kila siku katika maisha yetu.
Mazungumzo yasiyosikika ni yale tunayoongea wenyewe kwenye bongo zetu, tunapanga tunapangua tunakumbuka hili tunawaza hili yote haya kimya kimya lakini wakati huo uko unafanya jambo lingine au unasikiliza mazungumzo mengine au unaongea Mko kwenye mkusanyiko wa watu, kanisani, msikitini, kwenye kutano au kwenye chombo cha usafiri kuna wazungumzaji wachache wanaongea mnawasilikiliza kwa makini mko kimya, lakini kiuhalisia kila mmoja yuko busy akilini mwake anaongea yake.
Mazungumzo yasiyosikika ni mengi mno na kama kila mmoja angetaka kuyaongea kwa sauti inayosikika basi dunia ingejaa mwangwi mkubwa mno yani ni kama vile walokole wanaposali kwa sauti.
Mazungumzo yasiyosikika ni yale tunayoongea wenyewe kwenye bongo zetu, tunapanga tunapangua tunakumbuka hili tunawaza hili yote haya kimya kimya lakini wakati huo uko unafanya jambo lingine au unasikiliza mazungumzo mengine au unaongea Mko kwenye mkusanyiko wa watu, kanisani, msikitini, kwenye kutano au kwenye chombo cha usafiri kuna wazungumzaji wachache wanaongea mnawasilikiliza kwa makini mko kimya, lakini kiuhalisia kila mmoja yuko busy akilini mwake anaongea yake.
Pasingetosha mkuu, ingekuwa kitim tim halafu tusingesikilizana, sidhani kama kuna binadamu anaekosa kuwaza, ujue hapo ni lazima. Kuwaza sio mabaya au hali ngumu tu kuna kuwaza maendeleo, mipango ijayo, mafaniko n.k.Yani sijui ingekuwaje kama ingekuwa tunawaza kwa sauti
Hebu pata picha hii umemdate mtu mmeenda vizuri sana mpaka ikafika siku ya siku! Unakuwa na hamu naye kweli mnapanda kitandani unamaliza ufundi wako wote halafu mwenzako yuko kimya baridi kabisa unafikiri anawaza nini kwa wakati ule? Hawezi kuwa mkweli kukwambia aslani
Naomba niwaalike hawa ndugu Young Kibaka, neo1, witnessj, lazalaza, yang, Infoepadia, Madame B christine ibrahim atoto Preta ustadhjuma etc
hivi hamna njia ya kufanya haya mazungumzo ya kimya kimya yakapungua wakati huyahitaji..mfano mwanafunz yupo class unakuta wakat wa somo haya mazungumzo ya kimya kimya yamemtawala..hii inapoteza umakin wa masomo
Mazungumzo ya kimyakimya ndo ya kweli kuliko yanayosikika, maana heart/soul hauna unafiki hata chembe! Pale binadamu anapoanza kutaka kutamka jambo basi na uwongo hujitengeneza hapohapo/ Mtu unaanza kupigwa sound!
ila mhh mi hii hali ianitokeaga sana nikiwa ibadani yaan unakuta mawazo yamehama..nikisikia amen duh nashtuka narud kwenye kusikiliza..!ila unakuta mambo mengi yameshanipitaKikwao inaitwa lack of concentration, wale wanaofanya meditation wanalijua vizuri hili yaani unapoanza tu kumakinika akilini inakuja live stream ya matukio, mipango na changamoto mbalimbali kichwani...unajikurupusha na kurudi kwenye umakini lakini mara yanakuja mengine.... Kuna watu hufikia kutoka jasho kwa ajili ya kupambana na hii hali
ila mhh mi hii hali ianitokeaga sana nikiwa ibadani yaan unakuta mawazo yamehama..nikisikia amen duh nashtuka narud kwenye kusikiliza..!ila unakuta mambo mengi yameshanipita