Ryan Holiday
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 3,497
- 5,955
1. Ndugu H. Polepole leo ameanza kuelezea bei ya mtungi wa gesi wa Kilo 20 Cuba ambayo ni 2000/= TZS na kusisitiza hapa Tanzania tunapigwa na Mafisadi, huku Gesi tunayo lakini mtungi ni 60,000/= TZS. Amefanya hivyo kwa kujibu hoja za Bwana Ezekiel Kimwaga aliyemkejeli Ndugu Polepole na kusema muongo kuhusu bei halisia ya mitungi ya gesi Cuba kupitia Press yake aliyoifanya tarehe 29-08-2025.
2. Pia amelezea kuhusu Jiografia ya nchi ya Cuba, kwa kutaja Miji mikubwa, Miji ya Utalii, Miji ya Kihistoria, Balozi na maeneo nyeti ya nchi ya Cuba na huku akifafanua kwa undani kuonyesha Nchi ya Cuba anaielewa kiundani zaidi. Huku akihitaja miji kama Matanzas, Havana (La Habana), Santa Clara, Bayamo, Cienfuegos, Santiago de Cuba, Camagüey, Guantánamo na mingineyo.
3. Pia amegusia kuwa Cuba ni nchi yenye uchumi wa kijamaa (socialist economy) na ndio nchi iliyowekewa vikwazo vigumu na Nchi ya Marekani. Lakini nchi ya Cuba ndiyo rafiki mkubwa wa nchi za Afrika kutoka ukanda wa Western Hemisphere -- akisisitiza Ndugu Polepole.
4. Pia amesisitiza na kupinga vikali swala la Raisi Samia Suluhu Hassan kugombea tena awamu hii, huku akisema hakutakiwa kugombea. Huku akisema Samia akipata Uraisi hata waheshimu na kuwasikiliza raia wake.
5. Amesema Mama samia analazimisha uongozi na kwenye kampeni alipaswa kuwasema akina Salim Mwalimu ambao ndio anagombea nao, sio kuwasema Chadema ambao hawapo kwenye uchaguzi amewapiga pini na kusema wameweka mpira kwapani.
6. Amesema Tanzania ina viongozi wabaya ambao hawaelewi maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.
7. Pia amegusua ujenzi wa bandari kavu ya Kwala --- huku akisema tumesha chelewa ilitakiwa iwepo miaka 5 nyuma. Huku akisema Bandari kavu inatakiwa iwepo Morogoro na Dodoma, ilikupunguza msongamano wa Malori barabarani na kuongeza mzunguko wa mapato nchini.
Next Press -->Jumatano, Saa 3:00 Usiku -----> Kaa tayari.
"Ukombozi huanza akilini"
Link Below