Mazungumzo na Dr. Slaa: Maswali na Majibu

Status
Not open for further replies.
Mh. Dr Slaa nina maswali mawili naomba ukipata muda unisaidie;

1.Watu wengi wametoa mawazo yao humu JF na nje ya JF kuhusu Jengo la Makao Makuu ya chama wakisema lililopo sasa pale Kinondoni halina hadhi kwa levo ya chama ilivyo sasa, chama kina majukumu mengi tofauti na mwaka 2000, kina idara nyingi kwa hiyo na watendaji na ofisi lazima ziongezeke, mbali ya watendaji wa ndani kinapata wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Najua chama kina mambo mengi na kati ya hayo mengi kina priorities zake lakini suala la nyumba hata kwa ngazi ya kifamilia huwa linapewa uzito wake, je mmefikia wapi ktk hili.

2. Media ni nyenzo muhimu sana katika utendaji kazi wa siasa huwezi kueneza sera wala ujumbe bila kuwa na media. Je chama kina mikakati gani ya kuanzisha Chadema Television, Radio au Gazeti la chama kuliko kuendelea kutegemea vyombo ya watu binafsi au serikali ambavyo huchagua habari wanazozitaka. Nakumbuka ulishawahi kuligusia hili kipindi fulani kuwa tutegemee mabadiliko makubwa mwezi July naona july ndiyo hii, ni hatua gani mmeshafikia. Kwenye eneo hilo hilo chama kina mpango gani wa kupata mwanahabari(permanent) ambaye atakuwa yuko sambamba kila mnapofanya mikutano au maandamano na kusambaza matukio(live) zikiwemo picha kwenye mitandao na media zingine, kwa hili sina budi kumpongeza Mh. Regia lakini anahitaji mtu wa kumsaidia. Ni hayo tu asante nawatakia mafanikio mema.
 

Effective, Responsive Leadership.....
 

Nimekuelewa vizuri sana mkuu wangu japo majibu yako hayajajitosheleza....

Naomba Dk. Slaa anijibu maana bado namuona yupo online napa...

 
Malaria Sugu,
kwani hiyo OIC wamekatazwa kufungua ubalozi wao hapa Tanzania? Kwani lazima nchi iwe mwanachama ili wafungue ubalozi? Kuhusu mahakama ya kadhi hili swali ungewauliza CCM kwa kuwa wao ndio walioliweka kwenye ilani yao. Pia nyie kama waislamu si muanzishe? Eti kuna ubalozi wa Vatican, mbona kuna ubalozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya watu wa Irani na hauusemi?
 
Dr Slaa mimi maswali yangu ni haya;
1. Kuna mkakati gani wa CHADEMA kuwa na makao makuu yenye hadhi ya chama chenu? CUF wamelimudu hili nawapongeza sana.
2. Ni lini huyu muhuni Shibuda mtamuondoa ndani ya chama kwa sababu kwa kanuni za CHADEMA ameshapoteza uhalali wa kuwa kwenye kambi ya wapenda mabadiliko?
3. Pamoja na ukweli kwamba Dar es salaam ndio mkoa unaoongoza kwa kuwa na wajinga wengi je kuna mikakati gani ya kuhakikisha chama kinafanya vizuri kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa? chama cha CUF eneo hili wamejipanga vizuri sana.
Ni hayo tu nitarudi.
 


Dr Slaa kipenzi cha watanzania yupo vijijini anawaelimisha watanzania ili wajue dhuruma ya chama cha MGAMBA CCM dhidi ya watanzania.

Nadhani hawa wenye maswali ya kipuuzi Dr angetuachia sisi maana hawana maswali yenye tija kama alivyosema Dr. Slaa, yeye aendelee na majukumu makubwa ya kujenga nchni na chama.
 

kwa hilo swali la kwanza namsaidia, makao makuu ya chama na yenye hadhi ni kuiteka mioyo ya watanzania wanaoonewa tu, hakuna mako mazuri km ya wananchi.
 




Nape uja kila siku tatizo ni shule hawajampereka basi, ila moyo wa kazi anao.
 
Ndugu zangu wa JF tupunguzeni lugha za matusi. Let's acts in a more civilized manner.

Hili suala huwa tunapiga nalo kelele sana na ni aibu kubwa kweli...hata kama mtu amekuudhi,tuvumiliane ili tuwe na meaningfully discussion

Respect Sir/madame, we would have answered them in a different way but I think yours makes so much sense. We need lots of matured minds really.Keep up the same spirit!
 
ukimya wa watu hapa JF leo na hasa kwenye jukwaa la siasa sijaona thread mpya zinazoanzishwa ovyo ovyo, hii ni ishara kuwa watu wanakupenda na wapo kimya wakitafakari, ni kiongozi gani mwingine tena mwenye wadhifa wa uraisi anaweza kuja jukwaani na kuulizwa maswali na kila raia? Dr. nakuombea kwa Mungu uwe na moyo huo huo siku zote.
 
Dk. Slaa wa tz tunakukubali,tunakuunga mkono,wewe ndio mtu sahihi unaeweza kuivusha Tz hapa ilipo.
Pamoja tusonge mbele najua wapo watu wanaopiga vita harakati hizi ukombozi kwa propaganda zao za udini,ukabila,ukanda,n.k lakini kamwe hawataweza!
Hawez kuzuia mabadiliko hasa pale wakati unapokuwa umefika kama ilivyo sasa!
Nakutakia kila kheri nami naendeleza harakati popote ninapokuwa!

Uhuru wa kweli,
Mabadiliko ya kweli. Peopleeeesss.........
 
kwa hilo swali la kwanza namsaidia, makao makuu ya chama na yenye hadhi ni kuiteka mioyo ya watanzania wanaoonewa tu, hakuna mako mazuri km ya wananchi.
Mkuu huo sasa ni ushabiki ambao Dr Slaa haupendi, labda hujui kama Dr Slaa hapendi upambe usiokuwa na maana, nasubili jibu kutoka kwa Rais wangu ninayemtambuwa Dr Slaa.
Chadema ni chama kikubwa lazima kiwe na ofisi zenye hadhi yake.
 
Naona Dr. Slaa kawa kimya muda mrefu kweli na maswali yazidi kuongezeka....

Ila inaonekana bado yupo online.....
 
Naona Dr. Slaa kawa kimya muda mrefu kweli na maswali yazidi kuongezeka....

Ila inaonekana bado yupo online.....
Mkuu inawezekana yupo online kwa kutumia simu, maana alisema Laptop yake muda wowote itazimika chaji imemuishia na alipo hakuna umeme, kwahiyo nahisi anasoma kwanza maswali ili akija afanye majumuisho. ni mawazo yangu tu mkuu,.....
 
Naona Dr. Slaa kawa kimya muda mrefu kweli na maswali yazidi kuongezeka....

Ila inaonekana bado yupo online.....
Bila shaka anachukua notisi kama si kujaribu kusolicity mambo ambayo yanaikera jamii, kupitia maswali anayoulizwa hapa. Na kwa upande mwingine, kama kiongozi hapaswi kukurupuka tu na kutoa majibu ambayo yanaweza kuwa risasi ya kummaliza kesho. Ukumbuke huyu ni public figure, chochote atakachosema kwa kukurupuka kesho kitakuwa kwenye magazeti na title ya CHADEMA wamesema... hata kama atakuwa ametoa mawazo yake binafsi. So tumpe muda inawezekana pia anawasiliana na wenzake kujua msimamo wa chama.
 
leo malaria sugu kaongea na rais wa tanzania..bila hata chenga moja..

Inawezekana umechelewa mtani.....

Kulikuwa kuna upupu wa kufa mtu na hali ya hewa ilishaanza kuchafuka kwa kasi.....Thread ilishafika page ya 10 thank God Silencer akatokea na kusafisha hali ya hewa kuondoa takataka zote.....
 

- Saafi sana mkuu Jenifa, kumbe nilikuwa nakuona kwa wasi wasi wamejaaa, saafi sana!, SALUTE!

Willie @ NYC, USA.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…