Mazungumzo kuhusu ujenzi wa kiwanda cha gesi yaanza

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
SERIKALI ya Tanzania imeanza mazungumzo na mkusanyiko wa kampuni za gesi nchini kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi (LNG plant).

Miongoni mwa majadiliano yanayoendelea hivi sasa ni pamoja na yale yanayofahamika kama Host Government Agreement (HGA) ambayo ni baina ya serikali na mkusanyiko wa kampuni hio zilizokubaliana kuendeleza mradi huo.

Majadiliano hayo yanafanyika baada ya kimya cha muda mrefu tangu kutolewa kwa taarifa za kugunduliwa kwa kiwango kikubwa cha gesi kwenye bahari kusini mwa Tanzania.

Mshauri wa Kitaalamu, Ofisi ya Ushauri wa Mafuta na Gesi katika Ofisi ya Rais, Dk Emma Msaki anazitaja miongoni mwa sababu zilizochelewesha kuanza kwa mradi huo kuwa ni pamoja na kushuka kwa bei ya mafuta duniani na kugunduliwa kwa aina nyingine ya gesi (shale gas).

Dk. Emma alikuwa mmoja wa watoa mada hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa waandishi wa habari 24 kutoka nchi za Uganda, Ghana na Tanzania waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo katika uandishi wa habari za mafuta, gesi na madini.

Mafunzo kwa waandishi hao, ni sehemu ya mradi maalumu unaoendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa kushirikiana na International ICT Journalism nchini Ghana (Penplusbytes) na African Media of Excellence cha Uganda kwa ufadhili wa shirika la kimataifa kuhusu usimamizi wa rasilimali (Natural Resource Governance Institute- NRGI).

Ujenzi wa kiwanda hicho utafanyika kwa ushirikiano wa kampuni zilizofanikiwa kugundua gesi kwenye Bahari ya Hindi, kusini mwa nchi. Washirika katika mradi huo ni pamoja na Statoil na mshirika wake ExxonMobil, Kampuni ya Royal Dutch Shell na mshirika wake Ophir Energy, pamoja na Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC).

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alithibitisha kuhusu kuwepo kwa majadiliano hayo alipoulizwa na Raia Mwema juu ya taarifa hizo ambapo alisema kuwa kinachoendelea hivi sasa ni majadiliano mbalimbali, yakiwemo kuhusu HGA (Host Government Agreement).

“Wawekezaji lazima wawe na makubaliano ya kisheria kulinda mitaji hiyo mikubwa,” aliandika Profesa Muhongo katika majibu yake kupitia ujumbe mfupi wa simu.

Kwa mujibu wa Waziri Muhongo, mradi huo wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi nchikavu (LNG) utakuwa ndio uwekezaji mkubwa zaidi kuwahi kufanyika hapa nchini ambapo unakadiriwa kugharimu kati ya dola za Marekani milioni 30 mpaka 40.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil, Genevieve Kota Kasanga, naye anakiri kampuni yao kuwa katika majadiliano hayo na kubainisha kuwa gharama ya ujenzi wa kiwanda hicho ni kubwa hivyo inahitajika yawepo makubaliano kati ya wadau ambao ni serikali, kampuni za gesi na wadau wengine kwenye biashara ya gesi.

Katika mahojiano yake na Raia Mwema kwa njia ya simu, Genevieve anasema kampuni zinawekeza fedha zao nyingi, zikiwemo za mikopo, hivyo ni lazima kuzingatia hatari za kibiashara mara baada ya ujenzi kukamilika na kuanza kazi. Inaelezwa na wataalamu kwamba matayarisho yake ni tofauti sana na miradi mingine iliyozoeleka nchini.

Gesi asili itakayotumika ni kutoka kilometa kati ya 100 hadi 200 ndani ya bahari ambapo yatajengwa mabomba ya kusafirisha gesi kutoka kwenye visima hivyo vya baharini hadi nchi kavu.

Miongoni mwa masharti yaliyowekwa na serikali ya Tanzania katika mikataba ya awali ni pamoja na kiwanda hicho cha LNG kujengwa nchi kavu badala ya kuwepo huko huko baharini.

Hatua hiyo imelenga kulinufaisha zaidi taifa na watu wake ambapo mradi huo sasa unatarajiwa kubadili uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa.

Miongoni mwa manufaa ya muda mrefu yanayotarajiwa kupatikana ni pamoja na matumizi ya ndani ya gesi, mapato ya moja kwa moja kutokana na gesi, kodi, ajira na ushiriki wa wananchi katika sekta hiyo.

Katika kuhakikisha taifa linanufaika kupitia matumizi ya gesi yake, serikali pia iliweka sharti la asilimia kumi ya gesi inayozalishwa kubaki nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani.

Kampuni ya Statoil inalithibitisha sharti hilo kupitia maelezo yake yaliyopo kwenye tovuti ya kampuni hiyo ikisema; “Statoil itatenga asilimia kumi ya gesi itakayozalisha kwa ajili ya soko la ndani (DSO).”

Raia Mwema
 
Halafu bado mwezi wa kwanza Tanesco wanataka kupandisha bei ya umeme, mimi sioni kabisa faida ya hii gesi kwa watanzania
 
Tanesco nao vp
 
Back
Top Bottom