Mazoea yana taabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazoea yana taabu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by oba, Sep 10, 2011.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ajali ya kuzama kwa meli iliyotokea zanzibar ni matokeo ya serikali na wananchi kuishi kwa mazoea. Hivi inaingia akilini kwa meli yenye uwezo wa kubeba watu 610 kuwa inasafirisha watu karibu 1000 bila serikali kuchukua hatua yoyote?wananchi wanapanda meli na kujaa hadi chooni tupilia mbali ngazi za meli hiyo, hii kweli ni sawa?
  Hali hii ndivyo ilivyo ktk kila kona ya nchi, si kwenye mabasi, mitumbwi, daladala, bodaboda, baiskeli na hata guta- ujazo wa vyombo hivi unapita kiwango!ifike hatua serikali ione huruma juu ya roho za watu tunazopoteza kwa uzembe wa namna hii tena wa muda mrefu; NI MPUMBAVU TU NDIYE ANAYEWEZA KURUDIARUDIA KOSA LILE LILE HATA KAMA LINALETA MADHARA KWAKE.
  Nawasilisha!
   
Loading...