Kumekuwa na mtazamo kuwa maziwa ya kwanza ambayo mama huyapata mara baada ya kujifungua si maziwa yafaayo kwa mtoto. kutokana na mtazamo huu wanawake wengine huyakamua na kuyamwaga mpaka yanapotoka maziwa ya rangi nyeupe.
- Tunachokijua
- Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa jambo hili halina ukweli wowote.
Maziwa ya njano ni maziwa ya mwanzo, mazito yenye rangi ya njano ambayo hutoka siku chache za mwanzo baada ya kujifungua.
Maziwa ya kwanza ya mama kwa kitaalamu huitwa colostrum, ndiyo maziwa muhimu zaidi kuliko maziwa yoyote yale mama atakayokuja kuyatoa.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa haya ni maziwa ya kwanza ambayo hufanya kazi kama chanjo ya kwanza kabisa kwa mtoto. Maziwa haya ni chakula kamili chenye virutubishi vingi, na pia yanatoa kinga maalum dhidi ya maradhi.
Maziwa ya njano humsaidia mtoto kutoa kinyesi cha mwanzo chenye rangi ya kijani au nyeusi ambacho humfanya mtoto aumwe tumbo siku za mwanzo kama hatanyonya.