maziwa fresh yananijambisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

maziwa fresh yananijambisha

Discussion in 'JF Doctor' started by Chokochoko, Sep 20, 2012.

 1. Chokochoko

  Chokochoko JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  jamani kuna0tatizo linanisumbua nikinywa maziwa fresh najambajamba ovyo mpaka imekua kero kutwa nzima usiku kucha
  mpaka naona aibu embu nijuzeni anaejua uhusiano wa kujamba na maziwa ukoje au ninamatatizo mengioe?
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu wewe km mie nikinywa maziwa fresh yaani tumbo linajaa gesi mnoo, ni gesi kwa kwenda mbele hebu ma dr mtuhabarishe tatizo ni nini?
   
 3. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Chokochoko, Pole.. .una umri gani na tatizo hilo lilianza ukiwa na umri gani?..je vipi maziwa mgando, na chakula kingine chochote, mfano mayai; nyama nk?
   
 4. Chokochoko

  Chokochoko JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  kwenye vyakula vingine sipati hilo tatizo ni maziwa tuu, na hivi mimi ni mzazi nakunywa maziwa kila siku namhofia mtoto0na hiyo mijambo
   
 5. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  una kitu wanakita "lactose intolerance". dawa ni kuacha kutumia maziwa.
   
 6. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Chokochoko, nadhani utakuwa na tatizo tunaloliita "Lactose Intolerance"

  Lactose Intolerance, ni kushindwa kwa mwili kuvumilia aina ya sukari inayoitwa Lactose, na hii hutokana na kukosekana kwa enzyme inayoitwa Lactase...Tatizo hili hutokana na

  1. Kurithi: Kuzaliwa ukiwa na tatizo hili(ukosefu wa enzyme hii ya lactase)..mtu aliyezaliwana tatizo
  hugundua/hugunduliwa mapema, hasa wakati wa utoto pale chakula pekee ni maziwa.

  2. Magonjwa katika utumbo: Magonjwa yanoharibu sehemu chakula kinapofyonzwa(absorption villi) mfano Celiac sprue
  nk..

  3. Upungufu wa Lactase enzyme: Lactase ezyme(inayobadilisha sukari ya Lactose) hupungua kikawaida toka utotoni na
  kubaki katika kiwango kidogo ukubwani na hii tunaiita (Adult type hypolactasia).

  DALILI;
  Mara nyingi dalili za tatizo hili huwa ni tumbo kujaa gesi, tumbo kuuma,kutoa hewa chafu, na wakati mwingine kuharisha mara baada ya mtu mwenye tatizo kutumia maziwa au vyakula vyenye maziwa!

  MATIBABU/TIBA;
  Lactose Intolerance hutibika kwa kujua chanzo/kiini chake ni kipi kama ambavyo nimeeleza hapo juu..yaani

  1. EPUKA kutumia maziwa au vyakula vyenye maziwa mfano(Icecream, milkshakes,n.k)...

  2. Iwapo ni ugonjwa katika utumbo, tiba kulingana na ugonjwa huo itatolewa.

  3. Kutumia vyakula vingine vyenye kuwa na madini ya calcium, mfano(MAZIWA MGANDO/YOGURT, samaki, mboga za
  majani kama vile spinach)...Hii ni kwa sababu maziwa ni chanzo kikubwa cha Vitamin D,na madini ya calcium ambayo
  husaidia kuimarisha mifupa na meno...hivyo upungufu wa madini haya huweza kusababisha, mifupa kuvunjika kwa
  urahisi kuliko kawaida.

  MAZIWA YA MGANDO;
  Haya unaweza kutumia na hayana shida yeyote hii ni kutokana kuwa maziwa yanapochachuliwa(fermented) huwa na aina ya HARMLESS bacteria(probiotics) ambao wao wenyewe wana enzyme ya lactase hivyo kusaidia katika kuibadilisha sukari ya lactose.
   
 7. i

  issabela Senior Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Muone dokta ndodi kila siku anakataza watu wasinywe maziwa
   
Loading...