Mazishi ya Raila Odinga, viongozi mbalimbali wamehudhuria ikiwemo Rais Ruto

Mazishi ya Raila Odinga, viongozi mbalimbali wamehudhuria ikiwemo Rais Ruto

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Kenya Dr. William Ruto

View: https://www.youtube.com/watch?v=YT87RClirPI

Miongoni mwa Waliohudhuria mazishi ni

  • Rais wa Kenya - Samweli Ruto
  • Naibu Rais Kenya - Prof Kithure Kindiki
  • Mama Aida Odinga na Familia ya Odinga
  • Rais Mstaafu wa Kenya - Uhuru kenyatta
  • Rais mstaafu wa Nigeria - Oluṣẹgun Ọbasanjọ
  • Musalia Mudavadi - Prime cabinet Secretary, Kenya
  • John Mulimba - Waziri wa mambo ya nje, Uganda
  • Ruhakana Rugunda - Waziri mkuu mstaafu, Uganda
  • Aimé Boji - Waziri wa bajeti, Kongo
  • Jesca Magufuli - Mtoto wa Hayati John Pombe Magufuli (Rais awamu ya tano)
Sehemu ya hotuba ya Rais Ruto

Rais Ruto amesema taifa la Kenya linabubujikwa na machozi na msingi wa Kenya umetikiswa kutokana na hatua za waombolezaji kutoka na kifo cha shujaa mkubwa wa nchi, mwanaume aliyetengezwa kwa mapambano, mwanaume anayetambuliwa kama Rais wa watu, Mheshimiwa Raila Odinga.

Anasema alijuana na Odinga mwaka 1997 alipokuwa mbunge wa North Eldoret na baadae wakashirikiana katika kipindi cha katiba mpya na baadae kushirikiana katika kuunda chama cha ODM.

Ameendelea kwa kusema yeye ni miongoni mwa wanafunzi wa kweli na watiifu wa Raila Odinga, na anajivunia kuwa miongoni mwa watu waliowafunza naye na leo hii amekuwa Rais wa Kenye.

Anasema pia kuwa hata kama Raila angeshinda Urais mwaka 2022 asingeshtuka sana kwani wote ilani zao zilikuwa zinafanana yaani ilikuwa ni mashindani baina ya mwalimu na mwanafunzi wake.

Anasema anafurahi pia kuwa chama cha ODM ni sehemu ya serikali yake. Anajivunia uamuzi walioufanya yeye na Raila kumchagua waziri wa fedha John Bad ambaye amefanya makubwa katika wizara hiyo.

Amewahakikishia chama cha ODM kuwa watakuwa sehemu ama wataunda serikali ijayo baada ya uchaguzi. Aidha amewataka pia kuhakikisha wanakuwa imara kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Amewaonya wale watakaokitumia chama cha ODM kwa malengo yao binafsi huko nje, amesisitiza haitokubalika.

Amesema alimuahidi Odinga kuwa serikali itamgharamia matibabu popote pale atakapotaka kwenda kutibiwa.

Amemshukuru Waziri mkuu wa India Modi kwa mchango wao na hali na mali kwa Odinga kwa kipindi chote hicho.

Sehemu ya Wasifu wa Baba

Familia yake inamuelezea kama mtu aliyekuwa na misimamo na asiyekata tamaa huku akiipambania demokrasia ya taifa hilo na wakati wote alikuwa akipambania uhuru wa bara la Afrika.

Mbali na kufanikiwa kisiasa familia inaeleza kuwa pia Raila alikuwa mjasiriamali na mfanyabiashara mzuri na aliyefanikiwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo kuanzisha biashara ya familia.

Awali alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi akifundisha katika idara ya uhandisi makenika kuanzia 1970 hadi 1974. Anasifiwa kwa kuwa mtu aliyeamini makubaliano ya mtu mmoja mmoja.

Raila aliamini vyama vya siasa ndivyo vinavyoweza kuleta demokrasia ya kweli na mara kadhaa alikuwa akipinga matokeo katika mahakama kuu za Kenya huku akiunda majukwaa mbalimbali ya kisiasa nchini humo.

Kama kiongozi Raila aliamini katika mazoezi, tukuwa na ubinafsi, kujitoa sadaka, collective leadership, utu, uwazi, nidhamu, na kufanya kazi kwa bidii huku alifurahia bara la Afrika

Raila alikuwa na watoto wanne ambao ni Fidel, Rosemary, Raila Juniour na Winnie. Alikuwa na wajukuu Safi Odinga, Alive Odinga, senai Odinga, Lion Amolo Odinga, Wanji Garamongi.

Sehemu ya hotuba ya mke wa Raila Odinga

Mke wa Raila anasema hakuwahi kuwaza kama kuna siku ataiongoza familia yake kwenye mazishi ya mumewe, aidha ameishukuru serikali ya Rais Ruto kwa kumuaga Raila kwa ukubwa.

Amemshukuru pia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na kumtaja kama rafiki wa kweli wa Odinga na Familia yake nzima. Aidha amemshukuru Rais mstaafu wa Nigeria Obasanjo na viongozi wengine mbalimbali waliofika.

Ameeleza kuwa katika miaka yao 52 ya ndoa kumekuwa na milima na mabonde laikini kama ilivyokuwa kwa familia nyingine walijifunza kuishi na hali zote. Aidha Raila alitumia muda mwingi kwenye siasa kuliko hata familia yake.

Anaeleza kuwa watu wengi walipongeza kwa kuolewa na mhandishi na hakujua kuwa kama anaolewa na Mhandisi wa siasa ambaye aliendelea kuifanyia uhandisi Kenya, kisha baadae aligundua kuwa ni mtu wa tofauti sana.

Rais Mstaafu wa Nigeria Obasanjo

Amemuelezea Raila kama mtu aliyekuwa na mapenzi ya kweli kwa nchi yake na Afrika na ndiyo sababu iliyopelekea uhusiano wao kuwa imara mara dufu. Amemshukuru pia Rais Ruto kwa yote aliyoyafanya kufanya siku ya mazishi ya rail kuwa makubwa kama iiyovyokuwa.

Amemtaka Rais Ruto kuhakikisha anatoa nafasi katika serikali yake kwa chama cha ODM na vyama vingine vya siasa ili kuwaleta pamoja Wakenya wote.

"Kwangu mimi nimepoteza kaka, rafiki, mfariji, na mfanya kazi mwenzangu" - Rai Mstaafu, Obasanjo



Long Live the King, Live Long the Crown


Soma pia
 
Back
Top Bottom