Kilongwe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 423
- 116
NB: Mods naomba ufute ile makala nyingine kwani nimehustle mno kuedit bila mafanikio.
Je umeshawahi kufikiria ni jinsi gani watu wananyohangaika kufika mtaani kwenu kama huo mtaa jina lake halieleweki au kukumbukika kirahisi? Chukulia mtaa wenu unaitwa "Kwa mporomosha matikiti", siyo tu hili jina ni refu, bali linajumuisha maneno ambayo yanachanganya sana "mporomosha" kwani sisi wengine tutaita "mpolomosha".
Majina ya Website ama kwa kingereza wanaita "Domain Names", kama ilivyo anuani za mitaa au nyumba zina maana kubwa sana kwenye ulimwengu wa Website. Uchaguzi wake ni moja ya vitu muhimu sana katika maisha ya website, jina lisiloeleweka, siyo tu litaweza kumpa faida mpinzani wako, bali kuwachanganya wateja na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wako kwenye mtandao.
Kabla hatujaendelea, lazima tujue ni kwa nini kuna majina ya website?
Inteneti ni netiwoki ya kompyuta ambazo zimeunganishwa na zina uwezo wa kuwasiliana kwa kutumia kanuni za inteneti ( Intenet Protocol au kwa kifupi TCP/IP) .Ili mashine hizi ziwasiliane zinatakiwa zijuane, sawa na sisi tunavyojuana huko mitaani. Kwa machine hizi zinatumia namba zinazoitwa IP (mfano: 123.12.123.12) kama utambulishi wa mashine kwenye intaneti. Kwakuwa ni ngumu sana kukumbuka lundo la hizi namba, hapo ndipo majina ya website yalipoibuka.
Majina haya ni herufi zinazosomeka zikiwa ni njia mbadala wa kuwasilisha IP. Kwa mfano, mtu unapoandika