Mazao ya kulima kwa mkoa wa Kilimanjaro

dadi5

Senior Member
Jun 24, 2015
104
218
Habari, waheshimiwa naomba msaada kwa wenyeji wa mkoa wa kilimanjaro natarajia kuhamia mkoani humo kwenye mwezi wa 5. Naomba kujua mazao yanayolimwa katika mkoa huo pamoja na upatikanaji wa mashamba. Asanteni.
 
Huko labda ufuge mbuzi na shamba utalipata wapi walishabanana vijishamba ni vidogo sana
 
Habari, waheshimiwa naomba msaada kwa wenyeji wa mkoa wa kilimanjaro natarajia kuhamia mkoani humo kwenye mwezi wa 5. Naomba kujua mazao yanayolimwa katika mkoa huo pamoja na upatikanaji wa mashamba. Asanteni.

Mzee maeneo ya wachaga ni shida kidogo kupata maeneo ya kulima, kwani wao wenyewe ni wakulima wazuri tu. Pia hata ukipata shamba la kukodisha bei iko juu kwani watu wa huko wanaijua pesa. Huko kilimanjaro ni tofauti na mikoa ya pwani ambapo watu wanafanya kazi kwa kujivuta mno. Ukifika utajaribu kuangalia lakini napata shaka na wewe kupata shamba kwa urahisi. Ila kama ni mazao mengi yanakubali, kama mahindi, mihogo, maharage nk. Huko inakolimwa migomba kwenye mteremko wa mlima kilimanjaro wala usijisumbue kwani maeneo yameshajaa na hakuna mwenye shamba hata la heka 3 wote wana vijiplot, wenyewe wanaita vihamba.
 
Asante mkuu wacha nitafute kitu kingine cha kufanya
 
Asante mkuu wacha nitafute kitu kingine cha kufanya
Usikate tama, mashamba yapo yanakodishwa watu wanalima maeneo ya Sanya, kahe, KB nk
Sio wachaga wote wanafanya kilimo, wengine wanafanya biashara so wanakodisha mashamba wapate pesa ya business so wewe ukifika hapo Moshi usiwe na haraka, tulia kwa muda study taratibu utaziona ramani fursa unayaitaka.
 
Ukitaka maeneo ya kahe niambie, nina heka 20 huko na zina visima, pia ya mpunga ukitaka nitasaidia mkuu.
 
-Mazao yanayokubali kilimanjaro ni Mengi sana
1.Kahawa inakubali-Ila kwa sasa ni kama limetelekezwa 2.Maharage na mahindi yanakubali pia maeo ya machame, marangu, rombo, sanya juu
3.Kitunguu kinalimwa maneo ya kahe na Rundugai 4. Nyanya na Tikiti zinalimwa pia maeneo ya kahe pamoja na kitunguu 5.Parachichi pia zinakubali maeneo ya sanya juu 6. Mpunga unalimwa sana maeneo ya chekeleni/ Lower moshi

-Kuhusu upatikanaji wa mashamba
Mashamba ya kununua kwa kilimanjaro ni nadra sana kupata, labda itokee mtu anashida mnoo, na ndugu woote wameshindwa kumsaidia. Mashamba ya kukodi yapo inategemea na eneo na zao unalotaka kupanda. Kwa mfano maeneo kama ya mashine tools, au Masama shamba la mahindi la kukodi eka 1 kwa msimu mmoja ni kati ya tsh 100,000-150,000. Maeneo ya kahe ambapo watu wengi wanalima, nyanya, vitunguu, na tikiti eka 1 wanakodisha kwa msimu kwa tsh 150,000-300,000 kwa eka 1 kwa msimu mmoja, yapo mashamba ambayo tayari yanavisima mengine hayana, lakini kwa kahe chanzo ya maji kipo, kuna mto hivyo watu wengi wananunua pump na mipira kwa ajili ya umwagiliaji

KILA LAKHERI

Back
Top Bottom