Kukuza uchumi wa nchi yetu ya Tanzania kupitia kilimo

Kelvin irDunk

New Member
Apr 2, 2024
3
0
Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu ya Tanzania. Kilimo kinahakikisha upatikanaji wa chakula nchini na pia tunaweza kukuza uchumi wa taifa kupitia kilimo. Zifuatazo ni njia za kukuza uchumi wa taifa kupitia kilimo:

Matumizi mazuri ya ardhi: Tanzania ni nchi iliyobalikiwa kuwa na eneo kubwa sana lisilokuwa na makazi ya watu na pia maeneo mengi hayatumiki kabisa. Serikali yetu inaweza kutumia eneo hili katika suala zima la kilimo.
Serikali ihakikishe kila mkoa una shamba la mazao na shamba hilo lisimamiwe vizuri na uongozi wa mkoa. Jambo hili litasaidia kuhakikisha uwepo wa chakula nchini.

Uanzishaji wa kilimo cha umwagiliaji: Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo mazao ya chakula yana msimu hali hii husababisha bei ya vyakula kupanda bei haswa baada ya msimu wa mavuno.

Hali hii inatokana na wakulima kujishughulisha na kilimo msimu wa mvua tu. Msimu wa mvua ukiisha unakuwa msimu wa mavuno, mavuno ambayo hayawezi kukidhi haja ya nchi nzima. Hivyo kilimo cha umwagiliaji kitasaidia.

Matumizi ya vifaa vyenye teknolojia ya kisasa: Watanzania wengi wanaukimbia na kuudharau ukulima kutokana na vifaa vinavyotumika ambavyo vinamuumiza mkulima.

Wakulima wengi wanatumia majembe na vibarua katika kazi zao. Jambo hili husababisha kutoa mazao ambayo ni hafifu. Matumizi ya vifaa vya kisasa yatasaidia kupata mazao bora hata kwa viwango vya kimataifa.

Kutoa elimu na mtaji kwa wakulima wadogo: Wakulima wengi wa kitanzania hawana elimu ya kutosha juu ya kilimo. Wakulima wanaweza kupata elimu baada ya viongozi wa mikoa kuanzisha club za kilimo kwenye kila mkoa, ambapo viongozi wa club hizo watakuwa ni mabwana shamba ambao watahusika kutoa elimu kwa wakulima.

Kutafuta masoko ya mazao nje ya nchi:Kwa kua tutakuwa tunatumia teknolojia kwenye kilimo chetu,mazao yetu yatakuwa bora.

Hivyo viongozi wa nchi (waziri wa kilimo) ahusike kutafuta masoko mazuri ya mazao yetu nje ya nchi jambo hili litawahamasisha wakulima kufanya kazi kwa bidii kutokana na upatikanaji wa masoko yanayoridhisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom