Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao
Bondia Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei.
Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la WBO ada ya dola lakimi mbili $200,000 kabla ya makataa aliyopewa ya tarehe 3 Julai.
Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.
Kufuatia kauli hiyo ya shirikisho la ndondi la WBO, Mayweather hatambuliwi tena kama mshikilizi wa taji hilo.
Mmarekani mwenza Timothy Bradley.
Yamkini Mayweather alikuwa ameiahidi WBO kuwa akimshinda Pacquiao,angevua mataji yote ya vijana ilikuwapa mabondia wapya fursa ya kuwania mataji hayo lakini hadi kufikia sasa hajafanya hivyo.
Taarifa yao iliyochapishwa katika mtandao wa wboboxing.comimesema kuwa ''hatukukuwa na lingine baada ya Mayweather kushindwa kutekeleza matakwa yetu.kwa hivyo hatutamtambua mayweather kama mshikilizi wa ukanda huo wa Welter''
Hata hivyo Mayweather, ambaye ndiye anayeshikilia mataji ya WBA na WBC ana hadi julai tarehe 20 kukata rufaa ya kauli hiyo.
Mayweather anatarajiwa kuandaa pigano lingine mjini Las Vegas tarehe 12 Septemba, japo haijabainika atazichapa dhidi ya nani.
Wakati hayo yakijiri WBO inapanga pigano la welter linalopangwa kufanyika tarehe 27 kati ya Bradley na Jessie Vargas.
Chanzo:BBC
 
Siwezi kuwasaidia Waafrica....Myweather

Kama ni kweli amepokonywa, ila vipi zile hela alizotutambia nazo wananyang'anya?
 
1436269112148.jpg
 
Nilishaacha kusoma web ya bbc swahili siku nyingi sana,yaani hawana weledi kabisa, wanachukua taarifa kwenye bbc world news wanaitupia google translate alafu wanaweka kwenye web yao.

Mfano kwenye hiyo taarifa Timothy Bradley ameingiaje hapo au anahusika nini na mambo ya money. Bbc swahili hovyo sana.
 
Back
Top Bottom