Mayalla Paskali Vs Mwigulu Nchemba; Uhuru wa kutoa maoni

Mayalla Paskali Vs Mwigulu Nchemba; Uhuru wa kutoa maoni

Kijana wa Ifoza

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2025
Posts
506
Reaction score
979

1772709313832.png

1772709372233.png

Ndugu Mwigulu Nchemba kuvaa skafu za bendera ya Taifa si kwamba unaipenda nchi yako ama Mzalendo. Kama kweli unaipenda nchi yako basi ungepigania haki na uhuru wa watu wa kutoa maoni yao. Yaani msukuma Pascal Mayalla katoa maoni kama Mtanzania wewe unatumia vyombo vya serikali kukandamiza chombo chake cha habari anachofanyia kazi kwa kosa la kuutumia uhuru wake wa kikatiba wa kutoa maoni bila matusi. Halafu unataka mwaka 2030 tukupatie nchi kweli??? Katiba mpya inahitajika ili kutoa mianya ya wachafuzi kama hawa kunajisi katiba yetu ya Nchi.

Imagine kutoka kuwaweka viongozi kwenye kitimoto chini ya Mayalla Paskali na kipindi chake cha Kitimoto mpaka watu kuogopa kutoa maoni mitandaoni.

Hivi haya ni maendeleo ama tunarudi nyuma? Ifike wakati Mahakama zetu na idara za serikali ziwe huru kutoka kwa wanaowateua bila hivi hili Taifa litakua katika hali mbaya sana na litazalisha MACHAWA wengi na sitashangaa kama vyuo vikuu vyetu vitaombwa vianzishe Mitaala ya kufundisha UCHAWA.

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibarikia tanzania
 
Back
Top Bottom