Mayai yenye kiini cheupe: Ubora wake na madhara yake kwa mtumiaji

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
431
310
Jamani naombeni nielimishwe..

Mayai ya kuku yenye kiini cheupe. Je, ni salama kwa mlaji na ubora wake ukoje?

Sababu unachemsha yai kiini cheupe kabisa na ukikaanga yai lote jeupe. Hakuna unjano wowote katika yai.

Naombeni ushauri.
 
Mayai yenye kiini cheupe ndio hayo ya kisasa na yenye kiini cha njano ndio haya ya kienyeji.

Athali zake nyingi huwa naziona kwa mwanaume kama kuwa na matako makubwa.
 
Haina madhara yoyote. Kiini kuwa cheupe au cha njano haiwakilishi ubora wa yai. Kiini kuwa cha njano inasababishwa na chakula anachokula kuku na zaidi inatokana na kula majani.
kwa hiyo usitishike na kiini cha yai.
 
Mayai yenye kiini cheupe ndio hayo ya kisasa na yenye kiini cha njano ndio haya ya kienyeji.

Athali zake nyingi huwa naziona kwa mwanaume kama kuwa na matako makubwa.
Si kweli mkuu. Hata kuku wa kienyeji anaweza kuwa na kiini cheupe na wa mayai anaweza kuwa na kiini cha njano.
 
Nadhani kuwa na kiini cha njano ni kuwa yai hai yaani kuku jike aligegedwaa na jogoo. Kuku wa kisasa wengi hutaga bila kukutana na jogoo.
Ni mtazamo tu usijenge chuki
 
Nadhani kuwa na kiini cha njano ni kuwa yai hai yaani kuku jike aligegedwaa na jogoo. Kuku wa kisasa wengi hutaga bila kukutana na jogoo.
Ni mtazamo tu usijenge chuki
Huu ni mtazamo wako lakini kiutaalamu haiko hivyo.
Yai lililorutubishwa na jogoo laweza kuwa na kiini cheupe au cha njano. Kwa taarifa yako hata kuku wa kienyeji naye pia anataga bila ya jogoo.
 
Huu ni mtazamo wako lakini kiutaalamu haiko hivyo.
Yai lililorutubishwa na jogoo laweza kuwa na kiini cheupe au cha njano. Kwa taarifa yako hata kuku wa kienyeji naye pia anataga bila ya jogoo.
Asante kwa somo. Limeniingia. Nimefuta ujinga wa ujima
 
Back
Top Bottom