katika vitu ntapinga hadi nnakufa ni animal brutality. Usikubali kuwachoma kuku midomo kwanza kwa uzoefu wangu nikuambie tuu kwamba hiyo ya kuchoma midomo huwa haifanyi kazi, period. Kama unahisi wanakula mayai ni upungufu wa madini hasa calcium halafu jaribu kuwalisha chakula chenye uwiano mzuri (kuku wakubwa layers). Pia wakishajenga tabia ya kula mayai hata ukiwapa virutubisho wanavyokosa bado tabia wataiendeleza na kuwafunza wengine hivyo jaribu kuwa unaokota mayai mara kwa mara na kuyarudisha kiotani kipindi akionyesha dalili za kulalia mayai.