Mkuu naomba nirudi na feedback, Nashukuru kwa kweli wale vifaranga ulioniuzia wamekua sana na sasa baadhi wameanza kutaga,katika vifaranga 74 niliopata 8 walikufa na 66 ndio ninao mpaka sasa,naanza kufurahi ulaji wa mayai ya kwale kwa afya na tiba pia,na soon nitaanza kula nyama ya quail baada ya kutotoresha na mimi vifaranga vipya!wadau wengi wanaokuja kwangu wamevutiwa na ndege hawa,na nimeshapata order ya vifaranga na mayai baada ya baadhi kuzisoma na kugundua sifa na umuhimu wa mayai ya kwale!Kikubwa hapa ni kuleta SHUKRANI NYINGI KWAKO,kwa ushirikiano ulionipatia mwanzo mpaka sasa!Mungu azidi kukubariki
Mkuu nafurahi sana kwa kuleta mrejesho wenye mtazamo chanya,nami nafurahi na kushukuru sana kwa kuweza kutuamini,kuweza kukubali ku share some ideas naomba tuwe na tamaduni hii na muendelezo huu chanya kwa maendeleo yetu binafsi hata kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu!ahsante sana!
Niungane nawe kufurahi,
Umesikia kesi nyingine ya Kito, kuna mwenzetu tena kaingizwa king na Kito.
Niungane nawe kufurahi,
Umesikia kesi nyingine ya Kito, kuna mwenzetu tena kaingizwa king na Kito.
Ila kaka bila shaka huyu Kito aliweka contact zake humu,kwa nini victims wa utapeli wa huyu jamaha wasi mtrace,kumuaniaka wazi na hata kumchukulia sheria stahiki?haya mambo si ya kufumbia macho hata kidogo
Niliwahi kumpigia simu, alipokea, tatizo ni kwamba waliofanyiwa utapeli ndio hawasimami kidete kutaka hela zao zirudi.
Wakuu heshima kwenu!samahani kama nitawakwaza wadau wenzangu wale ambao wamestaarabika,ila naomba Watanzania tuwe wastaharabu na kuheshimu kile mtu afanyacho,kuna mdau mmoja toka last week alikua anawasiliana nami kua anahitaji tray saba za mayai,nikamkusanyie mayai na juzi tukapatana nimpelekee Goba,cha ajabu juzi tumewasiliana vizuri,mwenzangu akawasha gari na kumpelekea mzigo Goba,ila kufika kule huyo mdau kila akipigiwa simu hapokei,mpaka leo hii simu yake inaita tu haipokelewi,kilichonishangaza na kunisikitisha kulikua na umuhimu gani yeye kuweka order ya mayai huku akijua kua hayuko tayari kiffha/kununua?ameniingiza gharama zisizo za lazima wala tija!kama kuna mambo alitaka kujifunza juu ya Kwale na mayai yake si bora angeuliza tu kuliko kukunitia loss ya mafuta,muda etc!tujaribu kua serious na tustaharabike Watanzania wenzangu!
Mkuu mbona hizo tray 4 nilizokueleza uniifadhie naona unarusha kila siku?au kwale wako wamefikia ukomo wa kutaga?biashara haiendi hivyo ndugu,wajari wateja wako,kama hauna mzigo kwa sasa au una order kubwa bora useme hivyo,kuliko mambo ya subiri subiri!