Mayage S. Mayage amfundisha siasa Zitto Kabwe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mayage S. Mayage amfundisha siasa Zitto Kabwe.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Oct 3, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mwandishi wa muda mrefu Mayage S. Mayage ambaye aliwahi kuingia katika mvutano mkubwa na chama cha demokrasia na Maendeleo-CDM kutokana na makala zake leo amempa somo kubwa mbunge wa kigoma kaskazini Zitto Kabwe.

  Katika makala yake ya leo amemshambulia mbunge huyo kwa hatua yake ya kutangaza kugombea Urais mwaka 2015.

  Mwandishi huyo amesema anaamini Zitto hajui anachokifanya kwani viongozi wenzake wanahangaika vijijini kukijenga chama ili kuongeza mtaji wa kura lakini kwa makusudi Zitto analeta hoja ya Urais ili wanachama wahangaike kujadili Urais na kupoteza lengo la M4C.

  Pili mwandishi huyo amedai Zitto ni mtu anayeonyesha dhahiri kudharau viongozi wakuu wa CDM na anajiona pekee ndiye ' Statesman' na ndiyo maana hashauriani na wenzake katika mambo makubwa kama kutangaza mambo ya Urais ili kuepusha mivutano chamani.

  Mwandishi huyo amemalizia kwa kusema anaamini CDM haiwezi kufanya makosa kumuunga mkono Zitto Kabwe kwani kwa kufanya hivyo ni kukiandalia chama hicho anguko kuu kwenye uchaguzi mkuu ujao.

  Source:Raia Mwema Uk 8
   
 2. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Very interesting. Unajua Mayage S. Mayage na Zitto wote wanatoka Kigoma? Kwa hili namvulia kofia Mayage, hajatanguliza u-home boy!
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ningewashauri CDM na kina Molemo kutoshangilia Makala ya Mayage S. Mayage kisa eti kampa ZZK ukweli. Iwapo mtampa endorsement kwa Makala yake ya leo, muwe tayari kula matapishi yenu siku chache hii reputation itakapotumika kuwageuzia kibano!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Zitto ni mwanasiasa, au bishoo wa siasa?
   
 5. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto anatumikia mshahara kutoka kwa Mkama Wilson. Yuko kwenye Payroll ya CCM.
   
 6. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ukweeli utabaki kuwa ukweli tu, hata kama umesemwa na adui yako{e.g MPALESTINA NA MWISRAEL} huwezi kumshawishi mwanachadema aliyekomaa ambaye si mnafiki kuwa akifanyacho Zitto ni kizuri BIG NO! Binafsi nampenda sana Zitto, lakini kwa hili HAPANA!
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kama mshayajua hayo kwanini hamumfukuzi huyo mtu anazidi kuwapa headache?
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nadhani Katiba inasema mgombea urais sharti atimize miaka 40 na sioni uwezekano wowote wa kubadilisha hicho kipengele kwani hata CCM katika mapendekezo yao niliyoyaona wamependekeza umri wa mgombea urais ubaki hivyo hivyo.
  Nakubaliana na Mayage kitu kimoja kwamba hata mimi nadhani lengo kuu la Zitto ni kuvuruga M4C hasa nikirejea huko nyuma kwamba kila kukiwa na tukio kuu la CDM basi ni lazima Zitto aibuke na kutangaza mambo ya Urais ili kuhamisha mjadala.Hatujasahau alivyovuruga wanachama mwezi March katikati ya kampeni nzito za Ubunge Arymeru yeye akakimbilia Dar kutangaza kugombea Urais.Nadhani kilichookoa kampeni zile ni busara tu za viongozi wake wakuu.
  Ninachowashauri viongozi ni kumpuuza tu wasibishane naye wao waendelee kuimarisha chama vijijini.Mwisho wanachama ndiyo watakaoamua kwani wanaona yote yanayotendeka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  "Mzimu wa TISS na Jack Zoka ukikuandama utatamani kuhama nchi"
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Kamanda,sijakuelewa hapa.
   
 11. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Katika VYEO na NAFASI zote CDM walizompa au walizoshinikizwa kumwachia ZZK, hawajapatia kumpa NAFASI inayoendana na sifa, mapenzi na hisia zake. Zitto anafaa na ameonyesha kuwafunika watu wote Tanzania katika nafasi na vyeo vifuatavyo:


  • Mkurugenzi wa Habari za Bunge na Kamati Muhimu za Bunge
  • Muandishi wa Habari Binafsi na Makala za Ujiko
  • Makamu Katibu Mkuu-Mkurugenzi wa Ofisi ya Mtandaoni (Twitter, Facebook, and other Web 2.0 you name them)
  • Msemaji wa Kitengo cha Maafa, Dharura na Mambo Ambayo Hayajaamuliwa na Chama-CDM

  Iwapo iwapo mtahalalisha moja ya vyeotajwa hapo juu, basi mtakuwa mmempatia ZZK nafasi/cheo kinachoendana na wasifu, tabia, hisia na mwenendo wake
   
 12. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kwa nini usiungane na m..e mwenza mwezio mtatiro julius na lipumba, unaandika vitu visivyo na ushahidi ili mradi kujaza server ya JF
   
 13. n

  nyandaojiloleli JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni ushauli mzuli kwa zzk
   
 14. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  nimependa hitimisho la Mayage kuwa " kila mtanzania na hasa mshabiki wa chadema anajua ni mwana siasa gani ndani ya chama hicho amekifikisha hapa kilipo leo. hao ndio wenye kusema wanamtaka nani 2015 , kinyume cha hapo ni kutaka kuleta fujo tu kwa agenda iliyojificha" haya maneno mawili ya mwisho " AGENDA ILIYOJIFICHA" yanahitaji mjadala mpana kwa manufaa afya ya demokrasia ya chadema kama chama na taifa kwa ujumla.
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nimependa hii makala.Gazeti nimelinunua na nitalihifadhi kama kumbukumbu.
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli Mayage leo amefunguka kisawasawa.
   
 17. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  hii imenigusa sana. ukweli 100%
   
 18. M

  Molemo JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeniacha hoi.
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Huyo mwandishi hajuwi anachokisema, au hajitambuwi. Zitto anaweza kuwa 'rong' kutangaza nia nje ya utartibu, lakn kama zitto atagombea, ccm watapata kipigo cha mbwa-mwizi.
   
 20. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mwandishi njaa ambaye ameshindwa kuchambua mambo muhimu yanayoigusa nchi yeye anaona kumchambua zitto tena kwa majungu,hisia na kuwaaminisha watu uongo ndio suala la kuwahabarisha watanzania.Nimesoma makala yake na nimiongoni mwa makala ya kipuuzi kwa mwaka huu.Jamaa hajui siasa za Tanzania kabisa na ameandika maneno aliyoyasikia kijiweni.Sio mwandishi critical na anastahili kurudi shule kujua nini anachotakiwa kufanya.
   
Loading...