Mwandishi wa muda mrefu Mayage S. Mayage ambaye aliwahi kuingia katika mvutano mkubwa na chama cha demokrasia na Maendeleo-CDM kutokana na makala zake leo amempa somo kubwa mbunge wa kigoma kaskazini Zitto Kabwe.
Katika makala yake ya leo amemshambulia mbunge huyo kwa hatua yake ya kutangaza kugombea Urais mwaka 2015.
Mwandishi huyo amesema anaamini Zitto hajui anachokifanya kwani viongozi wenzake wanahangaika vijijini kukijenga chama ili kuongeza mtaji wa kura lakini kwa makusudi Zitto analeta hoja ya Urais ili wanachama wahangaike kujadili Urais na kupoteza lengo la M4C.
Pili mwandishi huyo amedai Zitto ni mtu anayeonyesha dhahiri kudharau viongozi wakuu wa CDM na anajiona pekee ndiye ' Statesman' na ndiyo maana hashauriani na wenzake katika mambo makubwa kama kutangaza mambo ya Urais ili kuepusha mivutano chamani.
Mwandishi huyo amemalizia kwa kusema anaamini CDM haiwezi kufanya makosa kumuunga mkono Zitto Kabwe kwani kwa kufanya hivyo ni kukiandalia chama hicho anguko kuu kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Source:Raia Mwema Uk 8