Si ajabu asitoe nyongeza yoyote ile mpaka anaondoka madarakani, nasema hivi kwa sababu kuu zifuatazo;
1. Umuhimu na ukubwa wa miradi ambayo serikali ya awamu ya tano inaitekeleza; Kikubwa kuhusu miradi hii ni kuwa, inagharimu pesa nyingi. Hivyo basi ni vigumu kuwaongezea watu marupu rupu wakati bado miradi hii inahitaji pesa i.e standard gauge etc
2. Watumishi wa umma hawana athari yoyote kwa serikali ya awamu ya tano; Inawezekana kabisa serikali ika amua kuwa na msimamo ule ule kwa watumishi wa umma, kwa sababu inajua watumishi ni waoga, hawana uthubutu hivyo wataendelea kusononeka tu lakini kazi watafanya.
3. Watumishi wa umma hawawezi kuikwamisha serikali ya awamu ya tano kuendelea kutawala; Idadi ya watumishi ni ndogo sana ukilinganisha na wananchi wa kawaida, hivyo basi hata watumishi wasipo ipigia kura serikali ya CCM itapita tu kwani inapendwa na wananchi.
4. Udhaifu wa vyama vya kutetea maslahi ya wafanyakazi; vyama hivi vya wafanyakazi vinaongozwa na makada watiifu wa chama cha mapinduzi, lolote wanaloamua watawala viongozi wa vyama hivi wanatekeleza bila kuhoji. Kwa maana hiyo hakuna wa kuwaunganisha na kutetea maslahi ya watumishi.
5. Chuki, dharau, ubinafsi na kiburi cha viongozi wetu; Ni wazi kabisa kuwa wanaofaidi rasilimali za Nchi nyingi duniani ni wanasiasa. Wakati wakiwa wamejipangia mishahara minono bila kujali elimu walizo nazo, mtumishi mwenye elimu hata ya shahada tu hafikii mishahara yao. Kwa sababu ya dharau na kiburi chao, uki hoji wataishia kukwambia " kama mshahara ni mdogo, acha kazi".
6. Sera ya serikali ya awamu ya tank ya kubana matumizi; kwa kuwa serikali ya awamu ya tano inajinasibu kuwa inabana matumizi, ni ndoto za mchana mtumishi yoyote kutegemea ongezeko lenyetija, labda kama ni zile tsh 3000.
Lai yangu, wakati umefika kwa watumishi ku " mind their own business" (kuwekeza katika biashara au shughuli zingine ili kujipatia kipato), tofauti na hapo utaishia kukamua maziwa ya n'gombe, wakati wanao kunywa ni wengine.