Takribani sasa ni zaidi ya wiki tatu nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana sakata na kile kinachotaka kionekana kana kwamba kuna mgogoro ama mkwamo wa uendeshaji wa mradi wa basi yaendayo kasi "UDART" ambayo kimsingi huduma hii imeendelea kuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wengi wa kawaida na umeendelea kuongeza kasi yaw ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Awali niliwahi kusema na pongezi serikali kwa uamuzi wake wa kuanzisha mfumo wa malipo wa serikali wa kieletroniki - GePG (Government electronic Payment Gateway system) wakati wa uzinduzi pale Kijitonyama, lakini nikatahadharisha baadhi ya changamoto na hujuma watakazokutana nazo pindi Utekelezaji wake utakapoanza kwa sababu mafisadi yaliyokuwa yanaiibia serikali hayatakubali kirahisi kuruhusu hili litokee.
Kinachoendelea pale UDART ni mwanzo wa hujuma zinazosababishwa na kuanzishwa mfumo huu ambao sasa umefinya na kuziba mianya ya kuendelea kuiibia serikali yetu.
Hujuma ndani ya UDART inafanywa na taasisi/watu/makundi kama manne. Leo nitaanza na hawa waliokuwa wanakusanya fedha kwa niaba ya UDART, mosi hii taasisi imekuwa ikiibia sana serikali yetu kupitia uwakala wa ukusanyaji wa mapato ya taasisi mbalimbali za umma lakini kwenye hili la UDART wameamua kufanya hujuma baada ya kujua kwamba sasa ni lazima mfumo mpya wa GePG utumike.
Wanahujumu UDART kwa kuanzisha na kuchochea migogoro ya wafanyakazi, hawa wazabuni wa kukusanya malipo ndio wamekuwa ma_mastermind kwa kuonesha Udart imeshindwa kuendesha mradi ambapo kimsingi mradi umeendelea kuwa imara pamoja na changamoto za mafuriko ambayo yameikumba zaidi ya mara nne.
Hawa wazabuni ndio waliandaa mgomo wa wale wakatisha ticket kwa kuwaambia kwamba mfumo mpya ukija basi na wao watakosa kazi wakati jambo kama hilo linazungumzika na Udart naamini ilikuwa tayari na mipango kabambe ya kuangalia namna ya kuwa_accomodate watumishi wale.
Rai yangu ni kuiomba tena serikali yetu sikivu, kupitia vyombo vyake mbalimbali vya ulinzi na usalama na wawaangalie kwa umakini sana hawa wazabuni / wakala wa kukusanya malipo wa UDART na hujuma zao mbalimbali.