Mawinga wa stationeries karibu na Msua Pharmacy mnaboa

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,427
Reaction score
139,469
Leo nataka niwachane mawinga. Hasa mawinga wa steshenari zilizopo eneo la phamasi ya Msua karibu na maeneo la Makoroboi.

Ukifika pale unakuta vijana kibao wako nje kwenye vibaraza. Ukikaribia wanakuvamia kama chui kukugombania upate huduma kwenye stationary fulani. Yaani unazongwazonga kama upo stend ya mabasi.

Pale pana huduma nzuri hasa ukiwa na kazi kubwa. Pia kuna warembo ambao hutaboreka kusubiri kazi yako. Lakini kero yake kubwa ni hao mawinga. Hii hali mimi hunikera sana mpaka nikaacha kwenda pale.

Usipokuwa mkali wanaweza kukushika kukuvuta huku na kule. Sasa hiyo inakuwa haina tofauti na stend ambako kumejaa wahuni.
 
Nchi imejaa njaa kila kona
Sio njaa ni ujinga wa vijana wa Tanzania kutaka pesa rahisi, chukulia mfano huyo kafuata huduma inakopatikana, kakuta utitiri wa mavijana ya hovyo ambayo yanakwepa kazi za uzalishaji mashambani na viwandani kwenda kushinda vibarazani wasikokua hata na hisa kwenye hayo maduka , sawa na wapiga debe na masalange kwenye stand mbalimbali kazi yao kimsingi haionekani
 
Kazi za mashambani na viwandani hazilipi. Ni bora hata ya uwinga na upiga debe.
 
Mawinga wa usafiri ndo wanachosha jamani, mtu unaenda mahali unapajua unajua usafiri utapata wapi.....unafika kituo cha bajaji eti kuna booonge la spika mtu anatangaza bajaji za xxx ziko hapa.

🙌🙌🙌
Eeh hiyo ya kutangaza iko wap ndonasikia kwako.
 
Kiswahili kweli kinakua tumepata maneno mapya mawili CHAWA na MAWINGA

Tunaomba serikali iwatambue mawinga na iwe sekta rasmi ya kujipatia kipato yenye sheria na taratibu zake
 
Karume pale sipiti zaidi ya miaka 5 nyuma nilirushiwa nguo bila ya kujijua , wale jamaa wanasumbua sana na wengi ni wezi .
 
Leo nataka niwachane mawinga. Hasa mawinga wa steshenari zilizopo eneo la phamasi ya Msua karibu na maeneo la Makoroboi.

Ukifika pale unakuta vijana kibao wako nje kwenye vibaraza. Ukikaribia wanakuvamia kama chui kukugombania upate huduma kwenye stationary fulani. Yaani unazongwazonga kama upo stend ya mabasi.

Pale pana huduma nzuri hasa ukiwa na kazi kubwa. Pia kuna warembo ambao hutaboreka kusubiri kazi yako. Lakini kero yake kubwa ni hao mawinga. Hii hali mimi hunikera sana mpaka nikaacha kwenda pale.

Usipokuwa mkali wanaweza kukushika kukuvuta huku na kule. Sasa hiyo inakuwa haina tofauti na stend ambako kumejaa wahuni.
We mwenyew unajua uko ktk nchi ya aina gani hivyo vitu vingine ni ujiongeze mwenyewe na misimamo yako ww binafsi chief 😂😂
 
Watu wanataka pesa wakabeti.
 
Back
Top Bottom