Mawinga wa stationeries karibu na Msua Pharmacy mnaboa

Mawinga wa stationeries karibu na Msua Pharmacy mnaboa

Leo nataka niwachane mawinga. Hasa mawinga wa steshenari zilizopo eneo la phamasi ya Msua karibu na maeneo la Makoroboi.

Ukifika pale unakuta vijana kibao wako nje kwenye vibaraza. Ukikaribia wanakuvamia kama chui kukugombania upate huduma kwenye stationary fulani. Yaani unazongwazonga kama upo stend ya mabasi.

Pale pana huduma nzuri hasa ukiwa na kazi kubwa. Pia kuna warembo ambao hutaboreka kusubiri kazi yako. Lakini kero yake kubwa ni hao mawinga. Hii hali mimi hunikera sana mpaka nikaacha kwenda pale.

Usipokuwa mkali wanaweza kukushika kukuvuta huku na kule. Sasa hiyo inakuwa haina tofauti na stend ambako kumejaa wahuni.
Wanakera sana mkuu. Nitakupeleka chimbo flan lipo Mkolani kama una kazi kubwa discount utaipenda
 
Back
Top Bottom