Mawenge husababishwa na nini?

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
413
195
Wana JF,

Kuna hali huwa inanikuta ya kuhisi mawengemawenge na kama akili haikuwi sawa hivi. Kwa mfano nikitoka nyumbani kuja mjini ndio nikikuta magari,pikipiki,watu wengi inanikuta sana hali hii.

Hapa nilipo ndani ya masaa mawili yaliyopita hali hii imenikuta hadi nikaamua nitulie mahali pa utulivu ikapungua ndo nikapata na wasaa wa kuandika hili.

Hali hii siipendi mwenzenu mnisaidie tasafadhali.
 

Benokolongokonongose

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
213
0
Jaribu kujichunguza vizuri inawezekana labda unavuta bangi. Mimi kuna katoto fulani kijiji cha Lupaso kikajifanya kinaniweza kunipiga. Baadaye naambiwa akivutaga bangi huwa anajiona kama mkubwa zaidi ya wengine. Bangi mbaya
 

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,024
2,000
Jaribu kujichunguza vizuri inawezekana labda unavuta bangi. Mimi kuna katoto fulani kijiji cha Lupaso kikajifanya kinaniweza kunipiga. Baadaye naambiwa akivutaga bangi huwa anajiona kama mkubwa zaidi ya wengine. Bangi mbaya

Ben, mawenge hayo anasema hasa kama anakwenda mjini. Nahisi ana MAZIGAZI. Atafune tangamwizi mbichi kabla hajaenda mjini. Tawfiiq.
 

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,186
2,000
Wana JF, kuna hali huwa inanikuta ya kuhisi mawengemawenge na kama akili haikuwi sawa hivi. Kwa mfano nikitoka nyumbani kuja mjini ndio nikikuta magari,pikipiki,watu wengi inanikuta sana hali hii. Hapa nilipo ndani ya masaa mawili yaliyopita hali hii imenikuta hadi nikaamua nitulie mahali pa utulivu ikapungua ndo nikapata na wasaa wa kuandika hili. Hali hii siipendi mwenzenu mnisaidie tasafadhali.

Inaweza kuwa pia ni dalili ya msongo wa mawazo (stress).
 

Justin Dimee

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
1,146
1,225
Ni Mawenge Yapi Kupga Kelele Au Kufanyaje
Au Nikama Uki Ingia Super Markt Kila Kitu Kwako Kinakupagawisha Mpaka Wenge,
 

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
836
1,000
Kuna kipindi mazingira yanakubadilikia ghafla na ndipo ubongo unapambana kuyakopi

Mawenge kwa mawazo yangu mimi yanatokana na ubongo kuhamishwa kiutendaji na mazingira. Yaani kipindi ubongo unakuwa unashughulika kukopi na kusawazisha utendaji wa ogani mbalimbali ndipo tunaposema Mawenge

Japo kwangu mimi tangu nikiwa angali mdogo nilikuwa Kunapotajwa neno MAWENGE huwa najenga akilini vitu kama hivyo nilivyochora hapo na huwa vinanipata (naviona angani) katika mazingira haya;

1. Nikiamka kwa nguvu/ghafla
(a)kwa kusimama kutoka nilipokuwa nimekaa au
(b)kwa kuinuka kutoka sehemu niliyokuwa nimelala usingizi

2. Kutaka kubeba kitu kizito kisha nikashindwa (hasa kama nimelazimisha kutumia nguvu nyingi)

3. Macho (sina uhakika kati ya macho au ubongo) kuingia ghafla kwenye mazingira tofauti ya hali ya hewa (mfano kusoma kwa mda mrefu kwenye simu au makaratasi kisha ukaacha ghafla)

4. Baadhi ya vipindi vya homa
JPEG_20201023_113152_-836722092.jpg


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom