Mawazo........

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,513
11,276
Kichwa kimeanza choka, ebu niwaze Taifa...

1. Taifa ambalo binti zake wakimwona Mzungu wanadhani ana ela.
2. Taifa ambalo ukiongea kiingereza unaonekana umesoma.
3. Taifa ambalo bank haikutafuti we ndo unaihonga ikukopeshe.
4. Taifa ambalo ukifeli unakuwa mtangazaji wa kipindi maalumu kabisa.
5. Taifa mbalo simu kali ni dili . hata kama vocha waweka za jero jero.
6. Taifa ambalo unazaliwa umeme shida, unafika miaka 30 hata huna bajeti ya Jenereta/Solar, unailaumu tu TAAnexo!
7. Taifa ambalo warembo washajiona wao ni waomba kusaidiwa daima.
8. Taifa ambalo kila mtu anataka ajue bei ya kitu ulichonunua!
9. Taifa ambalo usipoiba unaonekana ----!
10. Taifa ambalo kila mtu analalamika hana ela, mpe dili sasa, anaanza longolongo
11. Taifa ambalo sanne lina foleni ya watu wanaenda makazini
12. Taifa ambalo ukisema upo ofisini satatu usiku unashangawa ila upo club sanane usiku unasifiwa
13. Taifa ambalo kusema jana nlikuwa bata sana ile mbayaaaa ni dili na waonekana mjanja
14. Taifa ambalo bila kuigana siku haijapita
15. Taifa ambalo kila anayehojiwa anasema "Naiomba Serikali iliangalie suala hili"
16. Taifa ambalo ukiwa na gari hutongozi unatoa tu lift kitu shaa
17. Taifa ambalo kulipa bili yako pekeako ukaruka za wengine ni vita
18. Taifa ambalo ikinyesha dakika 5 tu foleni masaa
19. Taifa ambalo viongozi wanajua "hawa watazoea tu" washazoea umeme, washazoea "haijajulikana", watazoea na hii
20. Taifa ambalo kijiMC kidonyo tu kinaweza kufariki Taifa zima likageukia Msiba
21. Taifa ambalo kuteswa ni kunyofolewa Meno na Kucha
22. Taifa ambalo viongozi wake wana mipasho ka taarabu
23. Taifa ambalo vijana wameombwa wasipondee bali wasifie nchi
24. Taifa ambalo hata bomu likilipuka Arusha, wa Mbagala anajichagulia jina la Mlipuaji
25. Taifa ambalo, dah, nmechoka, endelea.......
 
no.21..Taifa ambalo kuteswa ni kung'olewa meno na kucha.
Ulitaka wang'olewe na nini kingine..?nina mashaka na wewe..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom