Mawazo yenu jameni Hawezi kupata cheti?

Mawazo yenu jameni Hawezi kupata cheti?

Dogo G

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,052
Reaction score
440
Strait to the aim,nna mdogo wangu kamaliza chuo kimoja cha ualimu diploma ya ualimu wa shule za msingi(odpe) mwaka jana mwezi wa nane lakini alihitimu akiwa anadaiwa ada kidogo tu.Sasa mpaka sasa ni chuo chao tu hawajapewa matokeo na nacte kisa chuo kinadaiwa pesa fulani fulani ambayo mimi siijui na mkuu wa chuo anawaambia anategemea pesa toka kwa wanachuo ambao hawakumaliza wamalizie ndipo wapate matokeo.Na mbali na hivyo amesema anawachukulia matokeo wale waliomaliza tu.

Kilichonileta ni kuomba mwenye ufahamu na haya masuala ya chuo,je mwanachuo asipokamilisha ada hapati hayo matokeo moja kwa moja na cheti hapati mazima hata akilipa siku za mbeleni?.Sijajua utaratibu wa NACTE kwamba huwa wanatoa matokeo nusu nusu kweli au la.Hapa nimechanganyikiwa wakuu dogo kasoma miaka 3 leo asipewe cheti cha nacte kisa ada? Au huwa wanatoa vyote then unapata kwa utaratibu?

Kama kuna mjumbe wa nacte anisaidie hapa au yeyote mwenye ufahamu
Wa haya.(kwa sasa ni kuhusu matokeo)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu utapataje cheti kama haukumaliza ada?
maliza kwanza ada hayo mengine yatafuata baadae..
acha ujanja ujanja!
 
Iko hivyo maana huwa kuna malipo chuo inatakiwa walipe so wanafunzi ambao hawajalipia mitihani matokeo huwa hayaji kabisa hadi mwanafunzi alipie...Mkuu wa chuo anachosema yuko sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo pesa ya mtihani,ya mtihani ilishalipwa.ila ada ya chuo.je kutolipa ada ya chuo ndo usipate cheti toka barazan?
Iko hivyo maana huwa kuna malipo chuo inatakiwa walipe so wanafunzi ambao hawajalipia mitihani matokeo huwa hayaji kabisa hadi mwanafunzi alipie...Mkuu wa chuo anachosema yuko sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom