Mawazo tafadhali: Hizi Kompyuta nizifanyie nini?

Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
262
217
Salaam,

Wakuu naomba msaada wa mawazo. Mimi naishi Dar na Morogoro, Nina kompyuta zaidi ya hamsini (ambazo ni desktop), zimetumika (used) lakini zipo kwenye hali nzuri kwa maana ya processor (2.7Ghz) i5 na zina 4GB RAM. Nataka nisiziuze kama nitapata wazo la kibiashara ambalo litaonekana kuwa zuri.

Nimejaribu kufuatilia biashara ya internet cafe sijapata majibu ya kueleweka kuhusiana na kama biashara hii ya internet cafe katika zama hizi za watu kutumia simu kuperuzi mtandao inalipa ama la?

Lakini pia sijapata majibu ya kutosha kuhusiana na biashara ya kufungua shule ya kompyuta (computer training centre).

Je, una uzoefu na biashara hizi mbili na unaweza ukanishirikisha uzoefu wako?

Kama una wazo jingine mbali na internet cafe na shule ya kufundisha compyuta, tafadhali nisaidie kwa kuniandikia hapa.

Natanguliza shukrani
 
Niko Moro, nimekuwa nikitamani sana kufungua shule ya computer kwa ajili ya watoto wadogo kujifunza programming kwa kutumia kids programming languages.

Sijafanya feasibility study yoyote kuona utayari wa wazazi kuhusu kuleta watoto wao kujifunza programming ya computer!!

Sijui kama tunaweza kusaidiana katka hilo, ili tuweze kuandaa wakongwe wa programming tangu wakiwa na miaka 3+
 
Asante mkuu kwa wazo jipya, nilikuwa sijaliwazia. Wazo linaonekana lipo shwari lakini kama ulivyogusia mimi pia sina uhakika na feasibility yake kwa Morogoro. Naona kama kwa Moro mwamko wa wazazi kuwalipia watoto wao kwenye mafunzo ya programming unaweza kuwa mdogo sana, labda kwa Dar. Kama unauzoefu kidogo kwenye mambo haya niPM mkuu.
 
Kwa uzoefu wangu wa kufundisha computer chuoni naona kuna tatizo kubwa sana la programming basics!! (Hili tatizo hata mm nililipitia wakati nasoma). Kwahiyo tukilenga kuibua vipaji vya programming tangu utotoni inaweza kusaidia sana watoto wa taifa hili huko mbeleni. Tunaweza kupata akina Zuckerberg wa kutosha.

Hiyo centre iwe ni programming academy!
 
Nimekupata mkuu! Nimefurahi kuona umeweka ustawi wa watoto wa taifa hili mbele - this is awesome. Ngoja tuone wadua wengine wanasemaje, lakini nitakutafuta tuone namna ya kulikuza wazo.
 
Mkuu siwakatishi tamaa lakini kwa uzoefu wangu wa biashara ni bora mngeanza kwa kutoa course general mkiwalenga watu wazima ambao wangependa kujifunza computer. Baada ya hapo biashara ikichanganya na huku mmeshapata uzoefu wa kutosha ndio mnaweza kuongeza course nyingine kwa kuwa target watoto wadogo kwenye programming kama jamaa alivyoshauri hapo juu.
 
Asante mkuu kwa mchango wako. Ni kweli kabisa, hata mimi nilikuwa na wasiwasi kuwa huenda ikawa shida kuwaapata wateja wengi kama tukijikita kwenye kuwafundisha programming watoto. Lakini pia sina uhakika na soko la kufundisha general courses za compyuta kwa watu wazima. Kama unauzoefu mkuu usisite kushare. Siku njema
 
zina gpu? hio i5 ni aina gani?

kwa computer powerfull kama hizo mi naona upotevu wa rasilimali kuzitumia kama internet cafe au kwa ajili ya kufundishia vitu vya kawaida.

hizi hapa idea zangu

1. fungua sehemu ya kuchezeshea pc games kama zina gpu hizo machine.

2. fungua studio ya video/picha kama una camera au unaweza kununua camera
 
Naona bado anaweza kufungua studio na bado akawa na darasa la computer mkuu, ikumbukwe anamiliki computer zaidi ya hamsini, sifikiri kama atazitumia zote kwenye huo mradi wa studio.

Darasa la computer kwa watu wazima naona kama itafaa sana!
 
sikatai idea ni nzuri, ila akiuza pc mbili za i5 anapata hela ya kununua pc hata 10 za kawaida ambazo zinafaa kufanya darasa la watu wazima.

ila
 
zina gpu? hio i5 ni aina gani?

kwa computer powerfull kama hizo mi naona upotevu wa rasilimali kuzitumia kama internet cafe au kwa ajili ya kufundishia vitu vya kawaida.

hizi hapa idea zangu

1. fungua sehemu ya kuchezeshea pc games kama zina gpu hizo machine.

2. fungua studio ya video/picha kama una camera au unaweza kununua camera

Mkuu, sijazichunguza kama zina gpu, nilivyoandika i5 nilikuwa namaanisha intel microprocessor ya i5 na siyo i3 ama i7 (latest). Asante kwa ideas mkuu, sema sina uzoefu kabisa na mambo ya games na video/picha, ngoja nikusanye taarifa.
 
si kweli kwamba i7 ni latest na i5 zipo generation 6 tofauti hivyo itabidi ujue hio i5 yako ni ipi ili kujipanga
 
Naona kufungua course kwa ajili ya watu wazima imekaaa poa sana ila kwa moro naona tatizo la packeg za kihasibu ni tatizo si mbaya sana hii kitu ikihusika nko moro kwa ushauri zaid ni pm
 
Unaweza kwenda wizara ya elimu pia ukaomba kibali ukafungua darasa kwa shule za primary na secondary hapo morogoro (Hii inaruhusiwa kwa shule za serikali unapewa ofisi) kwa ajili ya wanafunzi na pia ukajiongezea kipato kwa kufundisha pia watu wazima kutoka nje. Computer Literacy for Primary and Secondary Schools.
 
Asante sana mkuu, ngoja niikalishe halmashauri ya kichwa kwanza nione mambo yatakwendaje.
 
Unaweza kwenda wizara ya elimu pia ukaomba kibali ukafungua darasa kwa shule za primary na secondary hapo morogoro (Hii inaruhusiwa kwa shule za serikali unapewa ofisi) kwa ajili ya wanafunzi na pia ukajiongezea kipato kwa kufundisha pia watu wazima kutoka nje. Computer Literacy for Primary and Secondary Schools.

Wow! hii nilikuwa siijui kabisa. Asante kwa kutake trouble kushare hapa hiyo idea. Ngoja nifuatilie nijue mambo yanakuwaje kwa sasa na mambo ya Magufuli ya elimu bure, lakini pia nijue taratibu za kuomba na za uendeshaji. Once again thanks.
 
Back
Top Bottom