Mawazo huru: Kila kitu cha nje ya nchi kikatazwe!

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,487
12,113
Akaniambia;

Basi tumshauri apige marufuku magari yote maana yanatoka nje, ili baiskeli zetu za miti zipate soko.

Pia tupige marufuku viatu vyote vinavyotoka nje ili ung'ati (viatu vinavyotengenezwa kwa matairi ya gari) vipate soko.

Asisahau kupiga marufuku madawa yote ya kibinadamu yanayotoka nje ili waganga wetu wa jadi wapate soko.

Vyombo vyote vya habari vya nje vipigwe marufuku ili TBC ipate watazamaji.

Vyombo vyote vya baharini vilivyonunuliwa nje vipigwe marufuku ili wavuvi wetu wanufaike kusafirisha watu kwa vijidau vyao.

Konyagi zipigwe marufuku ili gongo ipate soko.

Katika kumalizia, kumeza dawa na kuchoma sindano ipigwe marufuku ili wauza majeneza na sanda hali yao kiuchumi ikae vizuri.

Hayo ni maneno aliyoniambia mwanangu punde tu ilipomalizika taarifa ya habari.

Nikaona ni swala la KIZALENDO.
 
Duh!
Mwanao nae!
 
Muanze kukataa kuagiza magari ya kifahar na mikopo yao out of that,,,,,muviii zinaibuliwa aka series,sasa wafungie na youtube.na cd empty
 
Back
Top Bottom