Mawaziri watishiana kifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri watishiana kifo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by frema120, Apr 25, 2012.

 1. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  na Mwandishi wetu

  MAWAZIRI wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wako katika vita ya waziwazi ya kugombea kubaki madarakani kiasi cha kutishiana kifo.

  Ugomvi huo pia uko kati ya wabunge na mawaziri ambao umejionyesha zaidi katika mkutano wa Bunge wa saba, uliomalizika jana mjini Dodoma.

  Mawaziri walio katika vita hiyo ya kupigana fitna, vijembe ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu; na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, ambaye yuko katika mnyukano wa kisiasa na Naibu wake, Athuman Mfutakamba.

  Duru za siasa kutoka ndani ya wizara hizo, zinasema kuwa mawaziri hao licha ya kufanya kazi katika ofisi moja, wako kwenye uhasama kiasi cha kushindwa kusalimiana.

  Sababu kubwa ya mawaziri hao kugongana, imeelezwa kuwa ni uchu wa kutaka kubaki madarakani hasa katika kipindi hiki ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri.

  Mmoja kati ya mawaziri hao ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa, aliliambia gazeti hili jana kuwa waziri mwenzake amemtishia kifo.

  Waziri huyo kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, alisema kuwa waziri mwenzake (jina tunalihifadhi), amemtishia kifo na anatarajia kuripoti tukio hilo polisi mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam kutoka mjini Dodoma.

  “Nimesikia waziri mwenzangu anasema ataniua, nimepata taarifa hizi kupitia kwa watu wake wa karibu. Ni jambo zito sana, nalifanyia uchunguzi kisha nitoe taarifa polisi na kwa Rais Kikwete,” alisema waziri huyo ambaye kwa sasa tunahifadhi jina lake.

  Alipoulizwa ataendelea kuingia ofisini wakati kuna tishio hilo, waziri huyo alisema anapaswa kuchukua tahadhari kubwa kila aingiapo na kutoka ofisini kwani hajui adui yake atatumia mbinu gani.

  Mawaziri hao wako kwenye mgogoro mkubwa unaotokana na mitazamo tofauti ya kikazi hususan suala la Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Charles Ekelege.

  Katika sakata hilo, Chami anamkingia kifua mkurugenzi huyo anayekabiliwa na tuhuma nzito zikiwemo za utendaji mbovu wa shirika hilo, huku Nyarandu akitaka bosi huyo wa TBS asimamishwe kupisha uchunguzi dhidi yake.

  Kwa upande wake, Nyalandu ametoa waraka unaombebesha mzigo waziri wake, Dk. Chami, akisema alimpa ushauri wa kumsimamisha kazi Ekelege kupisha uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), lakini hakutekeleza.

  Katika barua hiyo ya Februari 10, mwaka huu, kwenda kwa Chami, alimweleza kuwa wabunge walikuwa wanashuku kuwa mkurugenzi huyo alitoa taarifa zisizo sahihi.

  “Kikao cha briefing cha CAG na waheshimiwa wabunge, TBS imeshutumiwa kuhusiana na ukaguzi wa magari nje ya nchi na mchakato wote unaohusiana na suala hilo,” inasomeka dokezo hilo la Nyalandu.

  Alisema wabunge walioshiki katika ziara ya nchi za Hong Kong na Singapore wametoa madai kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS aliwadanganya juu ya kampuni zinazofanya ukaguzi wa magari na bidhaa nyingine nje ya nchi na wakatoa madai kuwa TBS imetoa taarifa tofauti na yale waliyoyaona katika ziara.

  Dk. Chami alikiri kupokea ushauri huo lakini, akasema wakati anautoa kulikuwa hakuna tuhuma zozote za kamati kuhusu Ekelege.

  “Ushauri ulikuwa mzuri lakini Ekelege ni mteule wa Rais hivyo huwezi kwenda kwa Rais kumtaka amwondoe wakati hakuna taarifa yoyote inayoonyesha tuhuma zake. Kuna njia mbili za kumsimamisha kwanza, kumshauri Rais na hizo ripoti dhidi ya Ekelege zipelekwe kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya TBS na baada ya hapo wakitoa maazimio ndiyo waziri anaweza kwenda nayo kwa Rais,” alisema Dk. Chami.

  Alisema kukosekana kwa ripoti iliyomchunguza Ekelege inamfanya akose nguvu ya kumshauri Rais.

  Mawaziri wengine walioko vitani ni Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, ambaye amemtuhumu Naibu wake, Athuman Mfutakamba, akisema ndiye mhusika mkuu wa tuhuma za ufisadi zilizoelekezwa kwake kiasi cha wabunge kufikia hatua ya kumshinikiza ajiuzulu.

  Waziri Nundu alisema Mfutakamba amekuwa akishinikiza kampuni ya China Communication Construction Company (CCCC), ipewe kazi ya kujenga gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa ilimgharamia safari kadhaa kwenda nje.

  Pia alishangazwa na shinikizo la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya Mwenyekiti wake, Peter Serukamba, nayo kushinikiza CCCC ipewe kazi hiyo akihoji, “Kuna nini?

  “CCCC ilinipa mwaliko nikaangalie miradi yake mingine inayoifanya; nikakataa na ilipoona nimekataa ikamfuata naibu wangu, ikampeleka China ikamlipia gharama zote akaenda yeye na msaidizi wake tu, bila kibali changu,” alisema na kuongeza:

  “Waliporejea nikamwuliza wamekwendaje huko bila kibali changu? Akasema eti wakati wanaondoka mimi nilikuwa sipo, kwa hiyo kibali alikuwa amekipata ofisi nyingine lakini hizo tarehe alizodai sikuwepo mimi nilikuwepo ofisini!”

  Kwa mujibu wa Waziri Nundu, kampuni hiyo hiyo ilimpeleka tena naibu wake Mauritania na Equatorial Guinea na kumgharamia kila kitu na aliporejea nchini ndipo alipoandika ripoti akishinikiza ipewe kazi hiyo.

  “Naibu wangu alipoanza kupelekwa huko nje na CCCC tena kwa kugharamiwa kila kitu ndipo matatizo yalipoanza…, mtu niliyefanya naye kwa ukaribu, matatizo yakaanzia hapo mpaka nikajiuliza kuna nini hapa kati ya naibu wangu na hii CCCC?”

  Alifafanua kuwa walipotaka kuanzisha mradi wa upanuzi wa bandari hiyo kwa kujenga gati namba 13 na 14, ilijitokeza kampuni ya CCCC ambayo ni mjenzi na si mwekezaji wala mkopeshaji na kudai ingefanya upembuzi yakinifu wa mradi kwa gharama zake.

  “Alivyotafutwa haijulikani mpaka leo…, aliingia mkataba gani na TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) mimi sijui…, huo mkataba ulisema atafanya nini na nini hakuna hadi leo lakini, nashinikizwa tu ooh hiyo CCCC ndiyo ifanye kazi hiyo… mimi nashangaa!”

  Waziri Nundu alisema kwa kuwa yalikuwa yamejitokeza makampuni 11 ambayo ni wakopeshaji na wawekezaji, alishauri kampuni hizo zishindanishwe ili ipatikane moja itakayofanya kazi hiyo na ushauri huo ndiyo ulioanza kumletea maadui wengi ndani ya TPA na wizarani.

  Alisema miongoni mwa kampuni hizo, ipo ya China Merchant ambayo ilisema ingejenga kwa sh 300 bilioni lakini bado shinikizo likawa ipewe CCCC kwa sh 542 bilioni.

  Akijibu madai ya Waziri wake, jana Mfutakamba alikiri kusafirishwa na kampuni hiyo lakini akasema ilifuata taratibu zote za kiserikali…

  “Nimesafiri kwenye maeneo hayo uliyosema… CCCC ilitoa mwaliko na mimi nilifuata taratibu zote na kanuni za kiongozi kusafiri kwa kuomba ruhusa kwa mamlaka husika kwa vile niliona ni safari yenye manufaa kwa nchi na mamlaka ilinipa ruhusa.”

  Alisema katika safari hiyo alitembelea miradi mbalimbali ikiwamo ya ujenzi wa reli na magati na aliporudi aliieleza serikali uwezo wa kampuni ya CCCC na kwamba kampuni ya China Merchant si wajenzi, bali ni waendeshaji tu wa ndege.

  Alikanusha kuwa na maslahi yoyote na kampuni hiyo na kusisitiza kuwa kibali cha kwenda katika safari hizo zilizogharamiwa na CCCC alipewa na Waziri Mkuu na hakitolewi na waziri wake.

  Hata hivyo akifunga mkutano wa Bunge juzi, Spika Anna Makinda aliwataka mawaziri walioibuliwa tuhuma mbalimbali bungeni kutoweka kinyongo kwa wabunge walioibua tuhuma hizo.

  Alisema wabunge walijadili masuala mbalimbali kwa uwazi kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kazi katika wizara hizo hivyo kuwataka kuchukua masuala hayo kama changamoto.

  “Msichukulie hasira kuhusu yaliyozungumzwa humu mpaka mkapasuka mifupa… waziri utasemwaje kama hujahusika? Hiyo mliyopewa ni changamoto; mnatakiwa kufanya kazi vizuri zaidi,” alisema na kuwasihi waondoke bungeni wakiwa marafiki.

  Walioshinikizwa kujiuzulu ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

  Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya; na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.

  SOURCE; TANZANIA DAIMA LEO
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,476
  Likes Received: 19,872
  Trophy Points: 280
  wauane tu hawa wadudu
   
 3. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Serikali legelege haiwezi kuwa na Mawaziri wanaoheshimiana!

  Laiti tungekuwa na mtu mwenye uwezo na nia njema angeondoa wote tuanze upya.
   
 4. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Wasitake kuzengua watu, mtu anayekuwa na dhamila ya kuhua ASEMI - Watu walio kabidhiwa dhamana ya kuedesha
  Wazira ya Viwanda na Biashara wanalumbana kama watoto wa Primary, sasa mambo ya kusema utamwambia JK kwamba mwenzako alitishia kukuhua unadhani ndiyo utapata Public sympathy uendelee kuwepo madarakani! Mimi nakaa najiuliza, hivi uteuzi wa viongozi wa design hii kuna vyombo vya TAIFA kweli vyenye jukumu la kuwa - VET kwa umakini viongozi hawa kabla awajampelekea JK for approval!

  Mimi sikumbuki tangu tupate uhuru kama kumewahi kutokea vituko vya kufedhehesha TAIFA letu kama hivi vya juzi bungeni ,eh! Naibu Waziri anamwanbia Waziri kwamba alipata kibari cha kusafiri kutoka ofisi nyingine, na aoni tatizo kwa kuwa hata Waziri mwenyewe anapata kibali kutoka ofisi hiyo hiyo, kwa hiyo ngoma ni DRAW!! - sasa mambo ya kutunishiana misuri italipeleka wapi TAIFA letu.
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu nadhani sasa ni wazi kabisa kuwa serikali haina mtu anayeweza kuiongoza, kila mtu anasema analotaka hakuna anayefuata taratibu, na kila mmoja anaongea analotaka. Sasa hivi hakuna leadership, ajabu ni kwamba tunataka tusubiri hadi mwaka 2015. Upepo huu ukipita itakuwa poa.
   
 6. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Nyepesi nyepesi zinasema mmoja wa hao "waheshimiwa" anakabiliwa na kesi ya mauaji Marekani na kwa sababu hiyo anakwepa kwa udi na uvumba kusafiri kwenda huko pindi itokeapo safari.
   
 7. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Safi sana wajihukumu tu kwa kujitoa na kutoana roho. JK yeye hawamtishii?
   
 8. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hatuwezi kushangaa kuuana kwao maana hiyo ni desturi yao wanamagamba.LAKINI KWA KAWAIDA MKUU WA TAASISI ANAYO NAFASI YA KUEPUSHA HAYA YASITOKEE KWA KUFANYA RESHUFAL AU KUVUNJA BARAZA KWA MINAJILI YA KUEPUKA ROHO YA MTZ KUPOTEA HIVIHIVI TU.
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  natamani sana wauane hawa wanga
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Tuwaache wafu wauane wenyewe kwa wenyewe...
   
 11. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao Mawaziri waendelee tu kutoana roho kwani huu ni Upepo tu utapita. Hata wakiuana wakabaki wawili, mjue huu ni upepo tu unapita.
   
 12. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mi nilifikiri watasema Uwazi siyo mama yao na wanaweza ishi bila uwaziri!something pays for them ndiyo maana wapo tayari kuuwana!
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wauane tu halafu JK atahudhuria misiba yao yote!
   
 14. Mzee Msemakweli

  Mzee Msemakweli Senior Member

  #14
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Siku zote mtu mchafu hawezi kumfukuza mchafu mwenzake. Ndege wa aina moja huruka pamoja. Waziri na kiongozi wao wote ni wamoja.
   
Loading...