Mawaziri wanne Kenya wakalia kuti kavu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wanne Kenya wakalia kuti kavu

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by nngu007, Aug 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  NAIROBI,Kenya

  WAZIRI wa Elimu ya Juu,Bw.William Ruto huenda akatupwa nje ya Baraza la mawaziri wakati Waziri Mkuu, Bw.Raila Odinga atakapowaadhibu waasi ndani ya
  chama cha ODM katika mabadiliko ya baraza hilo ambayo yatafanyika baadaye wiki hii.

  Habari kutoka jijini Nairobi zilieleza jana kuwa, mbali na waziri huyo,pia fagio hilo huenda likawakumba Waziri wa Viwanda,Bw. Henry Kosgey,Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Profesa Hellen Sambili na Naibu Waziri wa Mifugo,Bw. Aden Duale wakati Bw. Odinga atakapoamua kuondoa uasi wa kisiasa kwa upande wake ndani ya serikali ya muungano.

  Vyanzo vya habari vya kuaminika ndani ya ODM vilieleza kuwa Waziri Mkuu huyo amelazimika kutumia mamlaka aliyopewa kikatiba ya kuteua Mwanasheria Mkuu na mawaziri wengine ili kuondoa wabunge waasi wanaotumikia baraza la mawaziri.

  "Endapo itakwenda kama ilivyopanga,hatua hiyo itachukuliwa wiki ijayo(wiki hii), Itakuwa ni kwa ajili ya kuwaondoa waasi na wale wenye kesi mahakamani.Viongozi wa ngazi ya juu wameshatoa maagizo, "alisema mmoja wa washauri wa Waziri Mkuu ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa akile alichosema itakuwa ni sawa na kutoa taarifa kabla ya bosi wake.


  Alisema, mabadiliko hayo yatakwenda sambamba na uteuzi wa Mwanasheria Mkuu ambaye atachukua wadhifa wa kiiongozi aliyetumikia wadhifa huo kwa muda mrefu,Bw. Amos Wako ifikapo Agosti 27 mwaka huu.

  "Inaonekana kukubalika wiki ijayo ili kutoa muda kwa ajili uteuzi wa Mwanasheria Mkuu mpya na baadaye aidhinishwe na Bunge kabla ya Wako kumkabidhi ofisi. Kuna maeneo mengine ambayo yanapaswa kuangaliwa na hatua hiyo itafikiwa baada ya wakuu kushauriana, "chanzo cha kuaminika ndani ya Ofisi ya Rais kililiambia gazeti la Sunday Nation.

  Chanzo kingine ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu kilieleza kuwa Bw. Odinga amefikia uamuzi wa kumtema Bw. Ruto na washirika wake kwa ajili ya maslahi ya chama.(Daily Nation).
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Why not TZ; What is JK waiting? he need to get ride of Stomach hungry Ministers; If he would like CCM to survive he will need to get ride of all of his Ministers... They have been there for a long time no changes no development
   
 3. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Sasa mkuu nngu007 hiyo atiko orijino ni ya kiswahili halafu wewe unakomenti kwa kiinglish chenye utata, iweje? Anyway, mada imekaa vizuri.
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  We have a lot of sensitive matters to be settled in our own side before engaging into analysing other's issues. So do we have anything to copy from Kenya? I reckon we are the one to help them with practising good governance.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mada Imekaaje Vizuri? Unasema Anaway????
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  How R we going to help them practicing good governance... If our Ministers always Makes a Mistakes no responsibilities, just moved from one to another for years...

  I would rather see some get really fired
   
Loading...