Mawaziri wampa 5 Mnyeti ni baada ya kufanya ziara Mkoani Manyara

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Nyota ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti inazidi kung'ara kutokana na Mawaziri kuvunja ukimya na kueleza kilichopo Mkoani humo.

Waziri wa Tamisemi, Seleman Said Jafo akiwa katika ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan alisema, RC Mnyeti anaweza akawa Mkuu wa Mkoa wa tatu nchini ambaye ni mchapa kazi

"Kwa sababu niliwapa task ya kila Mkoa kuanzisha viwanda 100 na hapa naona ndugu yangu Mnyeti amenionyesha wewe ni miongoni mwa wapambanaji..katika wale watu watatu bora ambao wamesimamia vyema suala la viwanda wewe nakuombea unaweza kuwa miongoni mwao..."

Waziri Jafo aliyasema hayo alipokuwa katika kiwanda kikubwa cha madini ya GRIPHITE ambacho kipo Mirerani Wilayani Simanjiro
 
Back
Top Bottom