Mawaziri wachongewa; Kupelekwa Darasani na Marais Wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wachongewa; Kupelekwa Darasani na Marais Wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]Rais Jakaya Kikwete akijibu maswali kwenye Mkutano wa Uwekezaji wa Afrika unaoshirikisha pia wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza mjini Dar es Salaam. Wengine ni Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi (kushoto), Rais Mwai Kibaki wa Kenya (wa pili kulia) na Waziri Mkuu wa Rwanda, Bernard Makuza (kulia). (Picha na Robert Okanda).


  Imeandikwa na Joseph Lugendo; Tarehe: 18th April 2011

  MARAIS wa nchi wanachama wa Afrika Mashariki, wametakiwa kuwapeleka darasani mawaziri wao, ili mitazamo yao kuhusu uwekezaji na maendeleo ilingane.

  Akizungumza katika kipindi cha maswali kwa viongozi hao wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo katika Mkutano wa Tisa wa Uwekezaji Afrika, ulioanza mjini Dar es Salaam, mmoja wa wajumbe wa mkutano huo alisema viongozi hao wa nchi wamekuwa na mawazo mazuri lakini hawana watu wa kuwasaidia.

  "Mawaziri wamekuwa kikwazo kikubwa katika kufikia mafanikio kwa wananchi wao katika
  nchi zote tu za Afrika Mashariki. "Kinachotakiwa ni kuwapeleka shule na kuwawezesha mawaziri wenu ili wawe na mtazamo sawa na wenu, lakini ikiwa nyie wenyewe ndio wenye mawazo hayo, hamtafanikiwa," alisema mjumbe huyo ambaye jina lake halikufahamika mara
  moja katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na mawaziri.

  Akijibu hoja hizo, Rais Jakaya Kikwete alisema hakuna haja ya kuwapeleka shule kwa kuwa wana shule ya kutosha, ila tatizo ni katika kubadilisha mitazamo yao kuhusu uwekezaji ili kuongeza uwekezaji wa ndani na wa nje katika eneo la Afrika Mashariki lenye soko la watu bilioni moja sasa.

  Rais Kikwete alisema kwa nchi kama Tanzania, ambayo inatoka katika kipindi cha Ujamaa, kwenda katika mfumo tofauti na huo, watu wengi walifundishwa mbinu za kijamaa ikiwamo ya kuona biashara kama dhambi.

  Alisema kutokana na hali hiyo, moja ya njia ambazo Serikali imechukua katika kukabiliana na tatizo la kubadili mawazo, ni pamoja na kuteua mawaziri vijana ambao hawakukulia katika kipindi hicho na wazee ambao wamekulia katika kipindi hicho cha Ujamaa.

  Rais wa Burundi, Pierre Mkurunziza ambaye ni Mwenyekiti wa EAC, aliungana na Rais Kikwete kwamba mawaziri wana elimu ya kutosha lakini akaongeza kuwa, wanachopaswa ni kutekeleza wajibu wao huku wakijua kwamba kuna kuwajibishwa wakishindwa kufanya hivyo.

  Mbali na hoja hiyo ya mawaziri kupelekwa shule, marais hao akiwamo Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu wa Rwanda, Bernard Makuza, walitakiwa pia kuelezea wanachokifanya katika kuwezesha wawekezaji wa ndani.

  Katika hilo, wakuu hao wa nchi hasa Rais Nkurunziza na Rais Kikwete walilaumu sekta ya benki kwa kushindwa kuwasaidia wawekezaji wazalendo kushiriki katika kuinua uchumi wao.

  "Benki nazo zinakwamisha maendeleo ya wawekezaji wa ndani, wakitoa fedha wanatoza riba kubwa, kwa mfano Burundi, wanatoza zaidi ya asilimia 20, ni kubwa mno. "Pia hawa wamiliki wa benki wanapaswa kubadilika mawazo, imefikia mahali mwekezaji akienda benki anakuwa kama anaomba na kubembeleza mkopo, wakati benki zinatakiwa kuwatafuta na kuwabembeleza wateja," alisema Nkurunziza.

  Kutokana na hali hiyo, Nkurunziza alisema Burundi wameamua kupitia upya sera ya fedha hasa katika suala la riba na viwango vya kubadilisha fedha, ili kurekebisha tatizo hilo.

  Lakini Rais Kikwete alisema kwa Tanzania, wameamua kuiongezea mtaji Benki ya Rasilimali (TIB), ili iwe ya uwekezaji na kwa kuanzia, mwaka jana waliipa dola za Marekani milioni 50 na mwaka huu wataiongeza kiasi kama hicho.

  Rais Kikwete alifafanua kwamba lengo ni kuiwezesha benki hiyo iwezeshe wawekezaji wa ndani kwa kuwa iliundwa kwa nia hiyo, lakini katika miaka ya 1990 ilipata matatizo kutokana na sera za kupunguza thamani ya fedha.

  Baadaye katika mkutano wa nchi tofauti, kwenye mkutano wa Tanzania, mmoja wa wajumbe wa mkutano huo kutoka Kenya, James Moria, aliitaka Serikali ya Tanzania kurekebisha Sera na Sheria ya Ardhi, ili wana Afrika Mashariki, kama alivyowaita, wapate fursa ya kutumia ardhi ya Tanzania.

  Moria alisema ardhi ni moja ya vigezo muhimu vya uzalishaji na kwamba kurekebishwa kwa sheria hiyo, kutasaidia vigezo vingine vya uzalishaji kama mitaji kuingia Tanzania hasa katika sekta ya kilimo.

  Hata hivyo, Tanzania kwa miaka mingi imekuwa ikiweka wazi msimamo wake katika EAC kwamba ardhi ni moja ya maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya Watanzania.
   
 2. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo suala la uwekezaji tz halijakaa sawa,hivyo sio mawaziri tu wanaotofautiana kimtazamo bali hata siye wananchi wa kawaida.Miye kwa upande wangu nawaona wawekezaji ni watu wabaya sana kwa tz,kwa kuwa wamegeuza tz shamba la bibi, wanadharau kwa wananchi nk,yaani wameleta balaa zaidi badala ya manufaa tz.Fikiria kashfa zote za ufisadi zimeanza na haya maswala ya uwekezaji.
   
 3. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Rais Kikwete alisema kwa nchi kama Tanzania, ambayo inatoka katika kipindi cha Ujamaa, kwenda katika mfumo tofauti na huo"

  Mbona jana Bwana Mukama kasema CCM bado iko kwenye sera za Ujamaa na Kujitegemea? Mwenyekiti wa Chama na katibu wake hawawasiliani?
   
Loading...