Mawaziri waanza kujibu hoja zilizoibuliwa kwenye ripoti ya CAG

Cherenganya

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
2,309
1,775
Wakuu habari?

Nimepata taarifa leo asubuhi kwamba kuna takribani mawaziri watano ambao wametajwa imma kuguswa na taarifa ya CAG na leo watafanya mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma. Kwa taarifa zaidi ni kwamba Waziri wa Habari utamaduni na Michezo Mh. Dr . Harison mwakyembe ataongoza mkutano huo.

Mawaziri watarajiwa kwenye Mkutano huo ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, Waziri wa Habari utamaduni na michezo Bwana Dr. Harison Mwakyembe, Waziri wa Tamisemi Bwana Suleiman Jafo na wengine wawili ambao majina yao sikuyapata vyema.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema, mawaziri wote ambao wameguswa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka ulioshia Juni 30, 2017 kesho watatoa majibu kuhusu yaliyomo kwenye ripoti hiyo.

CAG Profesa Mussa Assad ametoa ufafanuzi kuhusu yaliyomo kwenye ripoti sitazilizowasilishwa leo bungeni mjini Dodoma.

Nawasilisha

========


Dodoma. Wale mawaziri waliotajwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wameanza kujibu hoja zilizoibuliwa katika ripoti hiyo leo.

Waziri wa kwanza kuanza kujibu hoja hizo ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo ambaye amesema watumishi wa Serikali 434 walichukuliwa hatua na tisa walifukuzwa.

“Wengine walishushwa vyeo, kupewa barua za onyo na wengine kufikishwa mahakamani, baadhi kama 13 hivi wanatakiwa kulipa fidia kiwango cha fedha walichopoteza,” amesema

Akizungumza katika mkutano wa mawaziri hao leo Aprili 12, Jafo amejitetea kuwa mwaka huu ukaguzi ukifanyika, sekta za wizara hiyo zitakuwa vizuri baada ya kufunga mashine za kielektroniki kwa kuwa kuna waliokuwa wanachota fedha za umma na kujenga majumba.

Mawaziri hao wanazungumza baada ya Ripoti ya CAG kuanika upungufu unaozigusa wizara zao jana bungeni.

Mawaziri waliokuja katika mkutano huo ni wa Habari, Dk Harrison Mwakyembe; Tamisemi, Seleman Jafo; na Viwanda, Charles Mwijage;

Wengine ni Waziri Sera na Uratibu wa Bunge, Jenista Mhagama; Ardhi, William Lukuvi; Mifugo, Luhaga Mpina; na Maji, Isaak Kamwelwe.

Pia, yumo Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako; naibu waziri Kilimo, Mary Mwanjelwa; na naibu waziri Muungano na Mazingira, Kangi Lugola.

Dk Mwakyembe, amesema leo watazungumza wachache na wengine wataendelea kujibu kila siku hadi wote waishe.


Chanzo: Mwananchi


===============




Akijibu hoja za CAG zilizoibuliwa, Mwijage, alisema taarifa ya CAG ilieleza sekta hiyo inachangia asilimia 35 katika Pato la Taifa kiwango ambacho si cha kuridhisha kulinganisha na matarajio ya asilimia 40.


Mwijage alisema kwa mwenendo uliopo, uchangiaji wa asilimia 40 kama ilivyotarajiwa utafikiwa ifikapo mwaka 2025 hasa ikizingatiwa mwaka 2012 mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa ulifikia asilimia 28 na mwaka 2017 ulifikia asilimia 35.

“Kwa kulinganisha mchango wa sekta hii kwa Tanzania katika Pato la Taifa na nchi nyingine bado nchi yetu inafanya vizuri. Kenya sekta hiyo inachangia asilimia 25, Uganda asilimia 20, Afrika Kusini asilimia 36, India asilimia 40 ikiwa imeajiri watu milioni 120 na Tanzania milioni sita. Malaysia asilimia 40, China asilimia 60 na katika nchi za Umoja wa Ulaya (EU) sekta hiyo inachangia asilimia 50 kigezo cha ajira ni watu 249 na Tanzania watu 99,” alisema.

Kuhusu kiwango cha asilimia nane cha kufungwa kwa shughuli za ujasiriamali zilizoanzishwa kama ambavyo CAG alivyobainisha, alisema kiwango cha Tanzania kufunga biashara ni kidogo.

Alisema wastani wa dunia ni zaidi ya asilimia 50 ya biashara zilizoanzishwa hufungwa katika kipindi cha miaka mitano.

“Hata katika nchi zinazoendelea Marekani na Canada, kiwango cha kufunga biashara zilizoanzishwa katika miaka mitano kinafikia asilimia 50,” alisema.

Pia alisema wizara itaendelea kuweka mazingira mazuri kutoa elimu za kuendesha biashara kwa wajasiriamali ili pengo la ufungwaji biashara zilizoanzishwa liendelee kupungua.

Kuhusu mchango hafifu wa asilimia moja katika mauzo ya nje kwa bidhaa za viwandani, Mwijage, alisema wizara inaandaa mkakati wa kukuza wajasiriamali watakaowezesha kukua kuwezesha kushiriki kuuza bidhaa za nje.

Alizitaja sababu nyingine ni bidhaa nyingi za wajasiriamali kuuzwa nje ya nchi bila kuwepo utaratibu rasmi, hivyo kukosa kumbukumbu sahihi za mauzo.

Hoja nyingi ya CAG ambayo Mwijage aliijibu ni uchakavu wa teknolojia za karakana za Sidon na alisema Serikali ilitambua mapema uchakavu wa karakana hizo katika mikoa saba kwa sababu zina zaidi ya miaka 30.

“Kwa kutambua hilo, wizara katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019, imetenga shilingi bilioni tano kuanza kuzifanyia maboresho karakana hizo,” alisema.

Mwijage pia alisema bajeti ndogo ya maendeleo inayoelekezwa Sido, kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ilitengewa Sh bilioni 14.1 ikilinganishwa na mwaka uliopita iliyotengewa Sh bilioni 26.8.


Chanzo: Mtanzania


 

Attachments

  • PIC 05.jpg
    PIC 05.jpg
    19.1 KB · Views: 23
Wa serikali za mitaa walitumbiliwa mapema sana bila kuongea na wanahabari wao wamepewa muda wa kuongea kuhusu uliji wao huu ni ujinga sana wote wanamakosa sawa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
CHADEMA na nyie toeni ufafanuzi mapema iwezekanavyo.
Wakati unawahimiza watoe UFAFANUZI mapema NA PIA HIMIZA MWENYEKITI AKANE TUHUMA ZA KUWA ANAKIKOPESHA CHAMA kwa riba kubwa mno.....na aseme kwanini anashiriki kufanya BIASHARA NA CHAMA anachokiongoza????.....NA PIA ASEME ANAWEZA VIPI KUTOLEA HOFU SISI WATANZANI YA KUWA KAMA CHADEMA WAKIFIKA IKULU SIJUI NI LINI HAWATAFANYA BIASHARA IKULU????
 
Wakati unawahimiza watoe UFAFANUZI mapema NA PIA HIMIZA MWENYEKITI AKANE TUHUMA ZA KUWA ANAKIKOPESHA CHAMA kwa riba kubwa mno.....na aseme kwanini anashiriki kufanya BIASHARA NA CHAMA anachokiongoza????.....NA PIA ASEME ANAWEZA VIPI KUTOLEA HOFU SISI WATANZANI YA KUWA KAMA CHADEMA WAKIFIKA IKULU SIJUI NI LINI HAWATAFANYA BIASHARA IKULU????
Mkuu
Ndo wajinga waliwavyo!
Wakiambiwa kunja ngumi ,wanakunja kisha wanapiga hewa, miaka nenda rudi!
 
Namkubali Jaffo, yuko makini kwenye kazi tatizo yeye sio dereva ni abiria wa siti za nyuma, utafanya nini??
 
Kwa mujibu wa Mh. Harison Mwakyembe, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo leo pia wataendelea na zoezi la Mawaziri wengine wawili kutoa maelezo juu ya Ripoti ya CAG. Aidha mawaziri sasa wameongezeka na kuwa 6 badala ya watano (5) niliotaarifiwa hapo mwanzo.

Tafadhali Modereta tupia video za majibu ya mawaziri wataohojiwa leo.

Nawasilisha
 
Ripoti ya CAG imekwisha toka baada ya kupitia taratibu zote za halali ikiwemo kuwahoji watendaji mbalimbali wakiwemo Mawaziri na watendaji wa wizara , Halmashauri na kila anayehusika , kilichobaki ni kuijadili bungeni na kwingineko na kuchukua hatua.

Chakushangaza tunasikia taarifa za mawaziri nane , ambao walipewa nafasi na CAG kufafanua haya na yale kabla ripoti haijakamilika eti nao wanaitisha waandishi wa habari na kumjibu CAG , Maajabu ya karne !
 
Wakati unawahimiza watoe UFAFANUZI mapema NA PIA HIMIZA MWENYEKITI AKANE TUHUMA ZA KUWA ANAKIKOPESHA CHAMA kwa riba kubwa mno.....na aseme kwanini anashiriki kufanya BIASHARA NA CHAMA anachokiongoza????.....NA PIA ASEME ANAWEZA VIPI KUTOLEA HOFU SISI WATANZANI YA KUWA KAMA CHADEMA WAKIFIKA IKULU SIJUI NI LINI HAWATAFANYA BIASHARA IKULU????




Acha kupiga ramli kwa chama ambacho hakijakabidhiwa dola,hebu tuambie mlimfanya nini Mkapa alipoanzisha kampuni ya ANBEN na kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira huku akiwa rais wa nchi?
 
Kwa nini wanajibia nje ya bunge hizo hoja (kuongea na waandishi wa habari)? Kuna haja ya kuzijibu? Kama ipo, si wangejibia ndani ya bunge?
 
Back
Top Bottom