Mawaziri wa Ulinzi na Mazingira Ghana Wafariki Katika Ajali ya Helikopta ya Jeshi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mawaziri wa Ulinzi na Mazingira wa Ghana wamefariki katika ajali ya Helikopta ya Kijeshi katika eneo la kati la Ashanti, pamoja na watu wengine sita.

Mkuu wa Majeshi Julius Debrah aliuambia mkutano na Waandishi wa habari kwamba Waziri wa Ulinzi Edward Omane Boamah na Waziri wa Mazingira, Sayansi na Teknolojia Ibrahim Murtala Muhammed (50), waliuawa katika ajali hiyo, ambayo aliitaja kuwa janga la kitaifa.

Ilikuwa imeondoka katika mji mkuu, Accra, saa 09:12 kwa saa za huko (na GMT) na ilikuwa inaelekea katika mji wa uchimbaji dhahabu wa Obuasi.

Mamlaka haijathibitisha chanzo cha ajali hiyo.Mkuu wa Majeshi ameagiza Bendera za nchi kupepea nusu mlingoti.

Naibu Mratibu wa Usalama wa Kitaifa wa Ghana na Waziri wa zamani wa Kilimo Alhaji Muniru Mohammed pia alikuwa miongoni mwa waliofariki, pamoja na Samuel Sarpong, Makamu Mwenyekiti wa Chama tawala cha National Democratic Congress.
 
Wapumzike kwa amani
 
Wapumzike kwa amani marehemu wote
 
Na malawi kampeni zianze, watu watumie chopa

images (23).jpeg
 
Ndo maana watu wengi wanaojielewa hawatumii sana helicopter japo wana hela mingi
Ni rahisi sana kuzifanyia hujuma Helicopter, wahujumu ulegeza nut zinazo fungwa kwenye rotor ya nyuma - Rotor ya nyuma ikishindwa kufanya kazi au kung'oka hilo likitokea, basi huwa ni vigumu sana kui-control Helicopter itanguka tu na mara nyingi ajali za Helicopter usabashwa na hitirafu kwenye tail rotor na wakati mwingine hitirafu kwenye Main rotor.
 
Back
Top Bottom