Mawaziri na wabunge wamiminika kumpa pole Kitwanga

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
583
Wabunge mjini Dodoma wamiminika nyumbani kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Charles kitwanga ,mawaziri na wabunge wamechukua hatua ya kwenda kumuona aliyekuwa waziri mwenzao na alisikika waziri mmoja akisema kuwa

" hili si jambo la kucheka kwani hii ni kama ajali ya kisiasa iliyomtokea mwenzetu kwani toka atenguliwe nafasi yake hayuko sawa lakini tunaimani atakuwa sawa tu, ndiyo maana tumekuja kumpa pole na kumfariji" alisikika waziri mmoja.

My take
Kufaana wakati wa shida na raha ndiyo utamaduni wetu watanzania tuendeleze utamaduni huu.
 
Bila shaka walevi wenzake, Hiyo siyo ajali ya kisiasa bali aliyataka mwenyewe, Hivi kama Waziri unaingia umelewa tena Bungeni hao unaowaongoza itakuwaje?Polis nae aende amelewa kaxini,Mwalimu nae aingie amelewa Darasani hali itakuwaje? Mi simpi pole, Walevi wenzake mpeni pole. Kwanza ni dharau kubwa sana kwa aliyemteua na kwetu wananchi unakuja unaongea na sisi wananchi huku ukiwa umelewa! Wakati huku kwetu ukiwa umelewa unafukuzwa kwenye kikao na unapigwa faini,
 
Tena kama ni ajali kaiunda mwenyewe,asitafute wa kumlaumu.
 
Hata mtoto akiumia licha ya kuwa umeshamuonya unamtandika kidogo halafu ndio unambembeleza na kumpa pole. Pole Kitwanga
 
Wameenda kumpa pole ya nini? Kwanza hao mawaziri na wabunge wanapokwenda kumtembelea ati kapata ajali ya kisiasa,wanapeleka ujumbe gani kwa Rais? Kamuonea?
Eti kaonewa au wanataka rais aruhusu mawaziri walevi
 
Back
Top Bottom