Kwa mujibu wa Taarifa ya kamati ya bunge iliyoundwa na Bunge kwa ajili ya kuchunguza athari zilizojitokeza ktk operation tokomeza. Ripoti hii nimesikiliza, nimesikiliza pia michango ya wabunge. Kilichopo kwenye riport ni aibu kwa serikali ya CCM na huwezi amini kama walifanya haya ni Waatanzania wenzetu na kwa hisia za michango ya wabunge Kagasheki, Mkuchika, Nchimbi, Nahodha, Mathayo na Chikawe hawasameheki na hamna namna lazima waachie ngazi. Nchi hii ni ya ajabu sana, jama polisi wa nchi hii hawana aibu kwa walioyafanya. Na kama leo hawa mawaziri kama hawataachia ngazi bas tutaamini zaid kuwa tunaongozwa na vipofu.