Jef Kirhiku
Member
- Dec 10, 2016
- 39
- 76
Wakati wa Sakata la kufungwa kwa kiwanda cha Dangote yupo kijana alijitokeza kueleza urasimu na usumbufu wa kupata makaa ya mawe yanayochimbwa na TANCOAL na kueleza namna inavyokwaza uzalishaji wa kiwanda na shughuli zao za kuyasafirisha kupeleka kiwandani .
Wapo mawaziri walijitokeza na kueleza hakuna tatizo lolote kuhusu upatikanaji wa makaa ya mawe nchini na kushangazwa kwao na viwanda vinavyoagiza makaa ya mawe nje ya nchi na kuacha ya hapa nchini yenye bei nafuu na ubora wa hali ya juu .
Leo mh Rais ameeleza uwezo mdogo wa TANCOAL ,urasimu na usumbufu wa upatikanaji wa makaa ya mawe kama alivyoeleza yule kijana mzalendo kisha kuagiza Dangote apatiwe eneo achimbe mwenyewe ndani ya siku 7.
Je wale mawaziri wanaaminika tena ?.
Walikuwa na maslahi gani kutetea uozo na udhaifu wa TANCOL unaokwaza shughuli za uwekezaji hapa nchini ?
Baada ya maelezo na hatua alizochukua leo mh Rais hawaoni ni wakati mwafaka wao kujipima kama wanatosha kubaki katika nafasi zao ?